Watanzania tuige mfano wa Ujerumani, tunapaswa kumsahau Magufuli na kuweka bidii kusonga mbele

Watanzania tuige mfano wa Ujerumani, tunapaswa kumsahau Magufuli na kuweka bidii kusonga mbele

Yeah Sheikh Yahaya alikuwa informer wa serikali na ile branch kipindi hicho bado inaitwa special branch au TIS aliyekuwa anaangalia mienendo ya watanzania waliokuwa wanaingia Swaziland kipindi hicho akitumia kivuli cha unajimu na kuwapa malazi katika hoteli ya hadhi kubwa aliyokuwa amepangisha watanzania waliokuwa wanafika Swaziland na kupewa malazi kumbe anawachunguza.

Na huyu Sheikh ndio aliiba document za Ludovick zilizokuwa na details na address za watanzania mbalimbali aliokuwa anawasiliana nao Nairobi na Swaziland akisaka asylum akazikabidhi kwa informer wengine waliokuwepo Swaziland .
Mwijage aliandika pia "The Dark Side of Nyerere's Legacy". Nilikisoma.

Kumbe wale kina Sheikh Yahya Hussein wote walikuwa ma informer wa Usalama wa Taifa. Mtu unaenda kwa mnajimu akutengenezee mipango yako, kumbe mwenzako anaenda kutoa taarifa kwa Usalama.

Kwa nini Magufuli kukumbukwa inawaumiza watu? Kwa nini inakuwa kitu kibaya kwao?

Mimi ningekuwa mtu ninayempenda sana Magufuli, ningekuwa na kila sababu ya kumkumbuka Magufuli, ili kukumbuka na kudumisha mazuri yake ninayoyapenda.

Mimi nikiwa mtu nisiyempenda Magufuli, nina kila sababu ya kumkumbuka Magufuli, ili kukumbuka mabaya aliyoyafanya na kuhakikisha hatuyasahau, yasijirudie.

Mimi ningekuwa mtu neutral ambaye najua Magufuli ana mabaya na mazuri yake, na nataka kuchukua mazuri yake na kuacha mabaya yake, bado ningeona umuhimu wa kumkumbuka Magufuli na kumchambua ili tujue mazuri yake ni yapi na mabaya yake ni yapi.

Hivyo hapo utaona watu wote wana sababu za kumkumbuka Magufuli.

Mwanafalsafa wa Kimarekani George Santayana alisema "Those who cannot remember the past are condemned to repeat it".

Sasa, kwa nini watu fulani wanaumia sana Magufuli akikumbukwa?

Magufuli ni sehemu ya historia ya Tanzania. Huwezi kumkwepa bila kuikwepa historia ya Tanzania.
 
Kuna mambo uwezi kulinganisha you know nothing about NAZI concentration camps and they were about.

Kufananisha masahiba waliyopitia Jews kwenye utawala wa NAZi with their Aryan race obesslon; jumlisha hizo baseless accusation zako za Magufuli umeonyesha kiwango cha ujinga wako.

Hitler kabisa unaweza kutoka mbele ya dunia na kumsifia, you must be very stupid.
Hitler is the third rail of political comparisons.

Ukishamlinganisha Hitler na mwanasiasa yeyote wa sasa tayari ushafeli hata kabla ya kwenda kwenye detail.
 
Kwa nini Magufuli kukumbukwa inawaumiza watu? Kwa nini inakuwa kitu kibaya kwao?

Mimi ningekuwa mtu ninayempenda sana Magufuli, ningekuwa na kila sababu ya kumkumbuka Magufuli, ili kukumbuka na kudumisha mazuri yake ninayoyapenda.

Mimi nikiwa mtu nisiyempenda Magufuli, nina kila sababu ya kumkumbuka Magufuli, ili kukumbuka mabaya aliyoyafanya na kuhakikisha hatuyasahau, yasijirudie.

Mimi ningekuwa mtu neutral ambaye najua Magufuli ana mabaya na mazuri yake, na nataka kuchukua mazuri yake na kuacha mabaya yake, bado ningeona umuhimu wa kumkumbuka Magufuli na kumchambua ili tujue mazuri yake ni yapi na mabaya yake ni yapi.

Hivyo hapo utaona watu wote wana sababu za kumkumbuka Magufuli.

Mwanafalsafa wa Kimarekani George Santayana alisema "Those who cannot remember the past are condemned to repeat it".

Sasa, kwa nini watu fulani wanaumia sana Magufuli akikumbukwa?

Magufuli ni sehemu ya historia ya Tanzania. Huwezi kumkwepa bila kuikwepa historia ya Tanzania.
Nilichokuja kugundua ni kwamba kuna ukinzani kwa waliompenda na wasiompenda na hakuna pande inakubali upande upi ni sahihi

Cha muhimu inatakiwa watu waruhusu yaongelewe yote juu yake iwe mazuri au mabaya.

Kwanini nasema hivyo , jibu ni kuwa kipindi cha utawala wake aliminya sana "civic space" critique wake walionjeshwa joto ya jiwe na vyombo vyote vya habari vilikubali kuimbishwa wimbo mmoja na ndio katika utawala wake tukapata hawa machawa na wanaosifia hata rais akipiga mihayo mvua ikinyesha wanamshukuru rais ilikua ni kosa kutoa habari inayokinzana na utawala ule ninaamini hata yule mpinzani wake mkuu Kigogo 2014 angekuwa anaishi bongo kwa ile miaka 3 angekuwa amepotezwa mapema sana.

Hivyo kwa kutokuwepo kwake walau waliopo hata Tanzania sasa ndio wanafungua makucha kuzungumza waliyoyapitia.

Mwisho tu kama unakumbuka Samia mwenyewe aliwahi kusema watu kwa miaka ile 6 sio kwamba walikuwa wachapakazi sana bali walifanya vitu kwa hofu sababu ya "Simba wa Yuda" sasa kwa kutumia msemo huo ni lugha ya picha tu Samia aliyekuwa VP alizungumza hivyo je waliokuwa chini huko hali ilikuwaje?
 
Hitler is the third rail of political comparisons.

Ukishamlinganisha Hitler na mwanasiasa yeyote wa sasa tayari ushafeli hata kabla ya kwenda kwenye detail.
Precisely ndio namshanga huyu poyoyo does he understand the NAZI atrocities for him/her to compare to anything today.

Leave alone the scientist who left Germany and took their knowledge to help build US.

Magufuli wasn’t perfect ile kuna hawa chawa wanaotumika indeipently na mafisadi na hawajui mipaka yao.

Wanakuja hapa kuropoka ujinga ambao they can’t defend.
 
Nilisoma kitabu cha Ludovick Mwijage kuna mengi aliyaandika nilikuwepo wakati wa utawala wa mwalimu ila mengi tu sikuyajua hadi baada ya kusoma hiki kitabu na baba yangu aliyekuwa mtumishi katika utawala ule aliponiambia mengine mengi baadae.

Ukiangalia aliyoandika Ludovick ni 90% yalijirudia katika utawala wa Magufuli walau tu zama hizi za miaka 6 kutokana na teknolojia ndio tulifahamu mengi na watu kupata mahali pa kusemea.

Nyerere pengine kwa kujua au kutokujua kuna madhila mengi sana alituachia kuna familia hawataki hata kumsikia je ni watu walifanya kwa amri yake au walifanya bila yeye kujua??

Nyerere kipindi cha mwishoni mwa uongozi wake alikiri katiba hii inampa madaraka makubwa sana na tusipokuwa makini mbeleni huko kuna mtu ataitumia vibaya (japo naye aliitumia vibaya pengine hakuwa anajiona anaitumia vibaya)

Rai yangu kama watu hawakujifunza na kufanya reform za katiba hii kutokana na nyakati ngumu nchi ilipopita 2015-2021 basi watanzania wajiandae kwa tufani nyingine pengine tunaweza kushuhudia au tusishuhudie kutokana na kutokuwa hai.

View attachment 2959595

Muhimu sana historia kuandikwa, kujadiliwa na kutumika kama nyenzo ya mafunzo. Hii tabia ya watetezi wa utawala wa Magufuli kututaka tusiandike, kujadili, kutafakari hata kuandaa dokumentari au kuandika vitabu ikemewe ili isije kukubalika kulazimishwa kusahau historia.
 
16 September 2021

Kesi namba 16 / 2021 ya Uhujumu Uchumi na Ugaidi : Watuhumiwa Freeman Mbowe na wenzie 3

Hali ilivyokuwa mahakama kuu Leo 16 September 2021 jijini Dar es Salaam. Shauri la kesi namba 16 / 2021 ya Uhumuju Uchumi

Unafananisha sura au philosophy? Mie niko kwenye mentality, na usije ukaniambia mbona Magufuli hakuanzisha gari kama Hitler. Nitakuambia nenda shule kasome.
Ndio maana nashangaa kuleta mfano huo? Umefananishia vitu visivyofanana. Hata ukifanya analysis ya kitu kimoja baadaa ya kingine upati vinasaba vyake.
 
Muhimu sana historia kuandikwa, kujadiliwa na kutumika kama nyenzo ya mafunzo. Hii tabia ya watetezi wa utawala wa Magufuli kututaka tusiandike, kujadili, kutafakari hata kuandaa dokumentari au kuandika vitabu ikemewe ili isije kukubalika kulazimishwa kusahau historia.
Moi anavyotajwa na udikteta wake na zile torture chambers za Nyayo , mtu hawezi kuamini Nyerere naye alifanya kama Moi licha ya yeye kuwa msomi zaidi kuliko Moi alipaswa awe tayari kukubali mawazo tofauti na yake hata kama hayapendi.
 
Sidhani kama kuna Mtanzania ambae hajui mazuri ya Magufuli akiwa raisi wa Tanzania, atapinga kwamba Magufuli hakuwa na roho ya uzalendo kwa Tanzania, alichukia ufisadi, alichukia watu ambao anawaona walikwamisha bidii zake za kuindeleza Tanzania. Hakuna Mtazania atakaepinga kwamba Magufuli alikuwa mchapa kazi kweli kweli, mwenye kupenda nchi yake na raia wa Tanzania, mzalendo namba moja.

Lakini hilo linakukumbusha nini?

Linatukumbusha kiongozi aliewahi kuwa na hulka ya Magufuli pale Germany, Adolf Hitler. Hitler alikuwa mzalendo kweli kweli. Alisimamia Germany na kuifanya Germany kuwa taifa lenye uchumi wenye nguvu kuliko mataifa yote. Alipenda uzalendo, alichukia ufisadi na usaliti dhidi ya nchi yake. Hitler alikuwa muasisi wa gari za VW, Volks Wagen (People's Car) ili kila raia wa Germany aweze kumudu kuwa na gari. Hakuna kiongozi katika Germany anaeweza kusemwa alileta maendeleo kwa nchi yake kama alivyofanya Hitler, mzalendo namba moja wa nchi yake.

Lakini sasa, nani leo unamsikia akimsifia Hitler kwa makubwa aliyoifanyia Germany? Hakuna, kwa sababu hakuna mtu aliyesahau machungu yaliyosababishwa na Hitler.

Hakuna mtu hapa Tanzania asiyejua machungu yaliyoletwa na Magufuli katika azma yake ya kuiendeleza Tanzania, machungu ambayo hayana utetezi hata uyaangalie kwa mtazamo upi. Hayana justification.

Hata hivyo, kwa tulio hai, kuwachukia Hitler au Magufuli, ambao tayari wamekufa, ni dalili kwamba tuna matatizo ya afya ya akili, tunahitaji psychiatric help. Kuwasifia pia ni tatizo, kwa sababu tunaumiza wale walioumizwa nao, ambao bado wapo hai pamoja nasi. Tutapanda gari za VW za Hitler, tutapita kwenye flyover za Magufuli, lakini hatutaimba sifa zao.

Kama Germany ilivyoamua kumsahau Hitler pamoja na mazuri aliyoifanyia nchi yake, Tanzania tunapaswa kumsahau Magufuli pamoja na mazuri aliyoifanyia nchi yetu.

Tuangalie mbele sasa. Tusahau yaliyopita, tuachane na kulinganisha uongozi wa sasa na uliopita. Tuvunje magenge. Tuanze upya.

The world and your country need YOU now, not Hitler, not Magufuli.
📝🆒🔊👍👌👊👏🤝🙏💐🎁🗼🎖️🏆👑🛡️
 
Magufuli ni sehemu ya historia ya Tanzania. Huwezi kukwepa kumtaja.

Umpende, usimpende, ni historia.

Historia haikwepeki.

Na kama humpendi Magufuli, ukikwepa kumtaja Magufuli, unaongeza nafasi ya mabaya aliyoyafanya Magufuli unayoyachukia yajirudie.

Na kama unampenda Magufuli, ukikwepa kumtaja Magufuli, unaonheza nafasi ya mazuri aliyoyafanya Magufuli unayoyapenda yasijirudie.

Kwa hivyo, watu wote, wanaonpenda na wasiomoenda Magufuli, wana sababu kubwa na nzuri kujifunza historia na kuepuka mabaya na kudumisha mazuri aliyoyafanya Magufuli.

Ndiyo maana Magufuki ataendelea kutajwa kwa miaka na miaka.

Hata Nero aliyemuua mama yake mwenyewe na kutuhumiwa kuunguza Roma na Caligula aliyemchagua farasi wake kuwa Senator wa Roma, bado wanatajwa mpaka leo, licha ya vituko vyao vyote.
👑🛡️

Kwanza kabisa, Hitler ni sehemu ya historia ya dunia, alitaka kutawala dunia, akaanzisha vita ya pili ya dunia, si historia ya Germany tu.

Pili, huwezi kutenganisha historia na maendeleo. Ili uendelee inabidi uijue historia yako uendeleze mazuri, usirudie mabaya.
👏🗼🛡️
 
Back
Top Bottom