ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 66,537
- 75,687
Waalimu ni Kati ya Watumishi wenye mishahara mikubwa labda useme wawe na poshoI say, waalimu wana kazi sana. Waongezewe mishahara jamani!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Waalimu ni Kati ya Watumishi wenye mishahara mikubwa labda useme wawe na poshoI say, waalimu wana kazi sana. Waongezewe mishahara jamani!
Mwijage aliandika pia "The Dark Side of Nyerere's Legacy". Nilikisoma.
Kumbe wale kina Sheikh Yahya Hussein wote walikuwa ma informer wa Usalama wa Taifa. Mtu unaenda kwa mnajimu akutengenezee mipango yako, kumbe mwenzako anaenda kutoa taarifa kwa Usalama.
Amequote hapo Kiranga , ipakue usome mimi nilibahatika kusoma hard copy ya vitabu viwili vya LudovickUnaweza nisaidia pdf yake ?
Hitler is the third rail of political comparisons.Kuna mambo uwezi kulinganisha you know nothing about NAZI concentration camps and they were about.
Kufananisha masahiba waliyopitia Jews kwenye utawala wa NAZi with their Aryan race obesslon; jumlisha hizo baseless accusation zako za Magufuli umeonyesha kiwango cha ujinga wako.
Hitler kabisa unaweza kutoka mbele ya dunia na kumsifia, you must be very stupid.
Nilichokuja kugundua ni kwamba kuna ukinzani kwa waliompenda na wasiompenda na hakuna pande inakubali upande upi ni sahihiKwa nini Magufuli kukumbukwa inawaumiza watu? Kwa nini inakuwa kitu kibaya kwao?
Mimi ningekuwa mtu ninayempenda sana Magufuli, ningekuwa na kila sababu ya kumkumbuka Magufuli, ili kukumbuka na kudumisha mazuri yake ninayoyapenda.
Mimi nikiwa mtu nisiyempenda Magufuli, nina kila sababu ya kumkumbuka Magufuli, ili kukumbuka mabaya aliyoyafanya na kuhakikisha hatuyasahau, yasijirudie.
Mimi ningekuwa mtu neutral ambaye najua Magufuli ana mabaya na mazuri yake, na nataka kuchukua mazuri yake na kuacha mabaya yake, bado ningeona umuhimu wa kumkumbuka Magufuli na kumchambua ili tujue mazuri yake ni yapi na mabaya yake ni yapi.
Hivyo hapo utaona watu wote wana sababu za kumkumbuka Magufuli.
Mwanafalsafa wa Kimarekani George Santayana alisema "Those who cannot remember the past are condemned to repeat it".
Sasa, kwa nini watu fulani wanaumia sana Magufuli akikumbukwa?
Magufuli ni sehemu ya historia ya Tanzania. Huwezi kumkwepa bila kuikwepa historia ya Tanzania.
Precisely ndio namshanga huyu poyoyo does he understand the NAZI atrocities for him/her to compare to anything today.Hitler is the third rail of political comparisons.
Ukishamlinganisha Hitler na mwanasiasa yeyote wa sasa tayari ushafeli hata kabla ya kwenda kwenye detail.
Nilisoma kitabu cha Ludovick Mwijage kuna mengi aliyaandika nilikuwepo wakati wa utawala wa mwalimu ila mengi tu sikuyajua hadi baada ya kusoma hiki kitabu na baba yangu aliyekuwa mtumishi katika utawala ule aliponiambia mengine mengi baadae.
Ukiangalia aliyoandika Ludovick ni 90% yalijirudia katika utawala wa Magufuli walau tu zama hizi za miaka 6 kutokana na teknolojia ndio tulifahamu mengi na watu kupata mahali pa kusemea.
Nyerere pengine kwa kujua au kutokujua kuna madhila mengi sana alituachia kuna familia hawataki hata kumsikia je ni watu walifanya kwa amri yake au walifanya bila yeye kujua??
Nyerere kipindi cha mwishoni mwa uongozi wake alikiri katiba hii inampa madaraka makubwa sana na tusipokuwa makini mbeleni huko kuna mtu ataitumia vibaya (japo naye aliitumia vibaya pengine hakuwa anajiona anaitumia vibaya)
Rai yangu kama watu hawakujifunza na kufanya reform za katiba hii kutokana na nyakati ngumu nchi ilipopita 2015-2021 basi watanzania wajiandae kwa tufani nyingine pengine tunaweza kushuhudia au tusishuhudie kutokana na kutokuwa hai.
View attachment 2959595
Muhimu sana historia kuandikwa, kujadiliwa na kutumika kama nyenzo ya mafunzo. Hii tabia ya watetezi wa utawala wa Magufuli kututaka tusiandike, kujadili, kutafakari hata kuandaa dokumentari au kuandika vitabu ikemewe ili isije kukubalika kulazimishwa kusahau historia.
Ndio maana nashangaa kuleta mfano huo? Umefananishia vitu visivyofanana. Hata ukifanya analysis ya kitu kimoja baadaa ya kingine upati vinasaba vyake.Unafananisha sura au philosophy? Mie niko kwenye mentality, na usije ukaniambia mbona Magufuli hakuanzisha gari kama Hitler. Nitakuambia nenda shule kasome.
Aah poa.Ndio usipotoshe sasa, eti mpinga ufisadi ilihali wezi wa mali za CCM hakuna hata mmoja alidakwa
Hata yeye kawindwa mara kibao.Hitler kapigana vita ambavyo vina faida kubwa kwa nchi kwa dunia, lakini huyu wakuwinda wakosoaji vinaleta faida gani?
Moi anavyotajwa na udikteta wake na zile torture chambers za Nyayo , mtu hawezi kuamini Nyerere naye alifanya kama Moi licha ya yeye kuwa msomi zaidi kuliko Moi alipaswa awe tayari kukubali mawazo tofauti na yake hata kama hayapendi.Muhimu sana historia kuandikwa, kujadiliwa na kutumika kama nyenzo ya mafunzo. Hii tabia ya watetezi wa utawala wa Magufuli kututaka tusiandike, kujadili, kutafakari hata kuandaa dokumentari au kuandika vitabu ikemewe ili isije kukubalika kulazimishwa kusahau historia.
Kala pilauUmefananisha Simba na Nyani.
Mifano yako Haina uhusiano sawa.
JPM awe kama Hitler kweli? Au unahadithi za vijiweni?
📝🆒🔊👍👌👊👏🤝🙏💐🎁🗼🎖️🏆👑🛡️Sidhani kama kuna Mtanzania ambae hajui mazuri ya Magufuli akiwa raisi wa Tanzania, atapinga kwamba Magufuli hakuwa na roho ya uzalendo kwa Tanzania, alichukia ufisadi, alichukia watu ambao anawaona walikwamisha bidii zake za kuindeleza Tanzania. Hakuna Mtazania atakaepinga kwamba Magufuli alikuwa mchapa kazi kweli kweli, mwenye kupenda nchi yake na raia wa Tanzania, mzalendo namba moja.
Lakini hilo linakukumbusha nini?
Linatukumbusha kiongozi aliewahi kuwa na hulka ya Magufuli pale Germany, Adolf Hitler. Hitler alikuwa mzalendo kweli kweli. Alisimamia Germany na kuifanya Germany kuwa taifa lenye uchumi wenye nguvu kuliko mataifa yote. Alipenda uzalendo, alichukia ufisadi na usaliti dhidi ya nchi yake. Hitler alikuwa muasisi wa gari za VW, Volks Wagen (People's Car) ili kila raia wa Germany aweze kumudu kuwa na gari. Hakuna kiongozi katika Germany anaeweza kusemwa alileta maendeleo kwa nchi yake kama alivyofanya Hitler, mzalendo namba moja wa nchi yake.
Lakini sasa, nani leo unamsikia akimsifia Hitler kwa makubwa aliyoifanyia Germany? Hakuna, kwa sababu hakuna mtu aliyesahau machungu yaliyosababishwa na Hitler.
Hakuna mtu hapa Tanzania asiyejua machungu yaliyoletwa na Magufuli katika azma yake ya kuiendeleza Tanzania, machungu ambayo hayana utetezi hata uyaangalie kwa mtazamo upi. Hayana justification.
Hata hivyo, kwa tulio hai, kuwachukia Hitler au Magufuli, ambao tayari wamekufa, ni dalili kwamba tuna matatizo ya afya ya akili, tunahitaji psychiatric help. Kuwasifia pia ni tatizo, kwa sababu tunaumiza wale walioumizwa nao, ambao bado wapo hai pamoja nasi. Tutapanda gari za VW za Hitler, tutapita kwenye flyover za Magufuli, lakini hatutaimba sifa zao.
Kama Germany ilivyoamua kumsahau Hitler pamoja na mazuri aliyoifanyia nchi yake, Tanzania tunapaswa kumsahau Magufuli pamoja na mazuri aliyoifanyia nchi yetu.
Tuangalie mbele sasa. Tusahau yaliyopita, tuachane na kulinganisha uongozi wa sasa na uliopita. Tuvunje magenge. Tuanze upya.
The world and your country need YOU now, not Hitler, not Magufuli.
👑🛡️Magufuli ni sehemu ya historia ya Tanzania. Huwezi kukwepa kumtaja.
Umpende, usimpende, ni historia.
Historia haikwepeki.
Na kama humpendi Magufuli, ukikwepa kumtaja Magufuli, unaongeza nafasi ya mabaya aliyoyafanya Magufuli unayoyachukia yajirudie.
Na kama unampenda Magufuli, ukikwepa kumtaja Magufuli, unaonheza nafasi ya mazuri aliyoyafanya Magufuli unayoyapenda yasijirudie.
Kwa hivyo, watu wote, wanaonpenda na wasiomoenda Magufuli, wana sababu kubwa na nzuri kujifunza historia na kuepuka mabaya na kudumisha mazuri aliyoyafanya Magufuli.
Ndiyo maana Magufuki ataendelea kutajwa kwa miaka na miaka.
Hata Nero aliyemuua mama yake mwenyewe na kutuhumiwa kuunguza Roma na Caligula aliyemchagua farasi wake kuwa Senator wa Roma, bado wanatajwa mpaka leo, licha ya vituko vyao vyote.
👑🛡️Magufuli ni sehemu ya historia ya Tanzania. Huwezi kukwepa kumtaja.
Umpende, usimpende, ni historia.
Historia haikwepeki.
Na kama humpendi Magufuli, ukikwepa kumtaja Magufuli, unaongeza nafasi ya mabaya aliyoyafanya Magufuli unayoyachukia yajirudie.
Na kama unampenda Magufuli, ukikwepa kumtaja Magufuli, unaonheza nafasi ya mazuri aliyoyafanya Magufuli unayoyapenda yasijirudie.
Kwa hivyo, watu wote, wanaonpenda na wasiomoenda Magufuli, wana sababu kubwa na nzuri kujifunza historia na kuepuka mabaya na kudumisha mazuri aliyoyafanya Magufuli.
Ndiyo maana Magufuki ataendelea kutajwa kwa miaka na miaka.
Hata Nero aliyemuua mama yake mwenyewe na kutuhumiwa kuunguza Roma na Caligula aliyemchagua farasi wake kuwa Senator wa Roma, bado wanatajwa mpaka leo, licha ya vituko vyao vyote.
🤔🙄Kwa hii bumunda iliyopo madarakani tunaanzaje kumsahau?
View attachment 2959487
👏🗼🛡️Kwanza kabisa, Hitler ni sehemu ya historia ya dunia, alitaka kutawala dunia, akaanzisha vita ya pili ya dunia, si historia ya Germany tu.
Pili, huwezi kutenganisha historia na maendeleo. Ili uendelee inabidi uijue historia yako uendeleze mazuri, usirudie mabaya.
🤣 🤣 🤣Magufuli pia alitaka kuiweka Tanzania katika top tena za dunia. Kuifanya donor country. Kumbuka malengo yake? Dar es Salaam iwe kama Ulaya.