Watanzania tuige mfano wa Ujerumani, tunapaswa kumsahau Magufuli na kuweka bidii kusonga mbele

Watanzania tuige mfano wa Ujerumani, tunapaswa kumsahau Magufuli na kuweka bidii kusonga mbele

Kwa sababu suala la Magufuli Vs Samia linaleta mgawanyiko na makundi, hatujawa kitu kimoja. ndio maana tunapaswa kumsahau.

Hao kina Nyerere, Mkapa, Mwinyi tulishawasahau, tunachokumbuka kwa sasa ni historia zao. Na pia hawakuwa na issue za kuumiza au kufaidisha kama ilivyokuwa kwa Magufuli, kiasi kwamba vifo vyao vionwe kuwa sherehe kwa baadhi ya watu. Wewe ulishasikia katika zama hizi za Samia kuna watu wa kundi la Nyerere?
Unaonaje hapa?
Huoni kama sera zao zilikuwa ni moja?
Kuna ubaya gani watu wakilinganisha Rais wetu mrithi na mtangulizi wake aliyemrithisha?
Acha wanyonge wakumbuke Magufuli na mama akitoka matajiri nao pia watamkumbuka.
 
Mkuu,

Mimi huwa napenda kufanya "immanent critique". Yani kupinga kwa kuanza kukubaliana nawe, hata pale ambapo sikubaliani nawe, ili kuonesha ukubwa wa makosa yako, hata kama nataka kukubaliana nawe. Kuonesha internal contradictions katika hoja zako hata kama nataka kuanza kukubaliana nawe.

Hata kama nataka kukubaliana nawe kwamba Magufuli alikuwa rais mzuri (kitu ambacho sikubaliani nacho), Magufuli ali fail kuweka mabadiliko ya kimsingi ma kimfumo kuzuia mabaya anayoyafanya Samia.

Magufuli ndiye aliyesisitiza ukubwa wa Rais na kuponda utawala wa sheria.

Hata pale alipofanya marekebisho ya sheria kuweka ulinzi wa rasikimali za kitaifa kishwria, hakuondoa mfumo wa rais mwenye nguvu sana na uchawa uliosababisha Samia aweze kurudi bungeni na kutengua sheria hizo.

Tena Magufuli alikuwa anasema kabisa kwamba inawezekana rais anayekuja akaharibu mambo, lakininas long as yeye ni rais hatakubali mambo yaharibike. Hiyo ni kauki ya rais ambaye amekubali kuwa hawezi kuweka mfumo endelevu. Rais asiyeele2a kuwa urais ni taasisi na si mtu mmoja.

Hilo ni tatizo, hata kwa anayekubali mazuri ya Magufuli niblazima aone kuwa Magufuli hakuwa broad minded enough kuweka mabadiliko ya kimfumo, alikuwa anacheza na akiki za watu tu kufanya maigizo ya mabadiliko wakati kwenye mambo ya msingibkama katiba mpya kakataa mabadiliko.

Na ikiwa kuna mambo ya kimsingi Rais akikosea anakuwa si Rais mzuri, na hili la kujenga mambo endelevu ni miongoni mwa hayo, basi Rais Magufuli hawezi kuepuka lawama kwenye madudu yanayoendelea leo.
Umeanza vizuri lakini katikati ya mistari nimemuona Makamba jr na Mdude Nyagali
 
Umeanza vizuri lakini katikati ya mistari nimemuona Makamba jr na Mdude Nyagali

Siko hapa kukupendeza wewe. Hata sikujui. Usijipe umuhimu ambao huna.

Hujaweza kuitetea hoja yako.

Hujaweza hata kuielezea.

Which is typical for people who have no respect for a logic following exchange.

I have no respect for such people.

Mimi najadili hoja.

Wewe unanijadili mimi, kwa ad hominem fallacy, unajadili watu.

Kwa mtaji huu, hatutaelewana.
 
Unaonaje hapa?
Huoni kama sera zao zilikuwa ni moja?
Kuna ubaya gani watu wakilinganisha Rais wetu mrithi na mtangulizi wake aliyemrithisha?
Acha wanyonge wakumbuke Magufuli na mama akitoka matajiri nao pia watamkumbuka.
View attachment 2960206
Mimi nimegoma kumsahahu Magufuli.
Msahauni nyinyi kama mnataka.
 
Sidhani kama kuna Mtanzania ambae hajui mazuri ya Magufuli akiwa raisi wa Tanzania, atapinga kwamba Magufuli hakuwa na roho ya uzalendo kwa Tanzania, alichukia ufisadi, alichukia watu ambao anawaona walikwamisha bidii zake za kuindeleza Tanzania. Hakuna Mtazania atakaepinga kwamba Magufuli alikuwa mchapa kazi kweli kweli, mwenye kupenda nchi yake na raia wa Tanzania, mzalendo namba moja.

Lakini hilo linakukumbusha nini?

Linatukumbusha kiongozi aliewahi kuwa na hulka ya Magufuli pale Germany, Adolf Hitler. Hitler alikuwa mzalendo kweli kweli. Alisimamia Germany na kuifanya Germany kuwa taifa lenye uchumi wenye nguvu kuliko mataifa yote. Alipenda uzalendo, alichukia ufisadi na usaliti dhidi ya nchi yake. Hitler alikuwa muasisi wa gari za VW, Volks Wagen (People's Car) ili kila raia wa Germany aweze kumudu kuwa na gari. Hakuna kiongozi katika Germany anaeweza kusemwa alileta maendeleo kwa nchi yake kama alivyofanya Hitler, mzalendo namba moja wa nchi yake.

Lakini sasa, nani leo unamsikia akimsifia Hitler kwa makubwa aliyoifanyia Germany? Hakuna, kwa sababu hakuna mtu aliyesahau machungu yaliyosababishwa na Hitler.

Hakuna mtu hapa Tanzania asiyejua machungu yaliyoletwa na Magufuli katika azma yake ya kuiendeleza Tanzania, machungu ambayo hayana utetezi hata uyaangalie kwa mtazamo upi. Hayana justification.

Hata hivyo, kwa tulio hai, kuwachukia Hitler au Magufuli, ambao tayari wamekufa, ni dalili kwamba tuna matatizo ya afya ya akili, tunahitaji psychiatric help. Kuwasifia pia ni tatizo, kwa sababu tunaumiza wale walioumizwa nao, ambao bado wapo hai pamoja nasi. Tutapanda gari za VW za Hitler, tutapita kwenye flyover za Magufuli, lakini hatutaimba sifa zao.

Kama Germany ilivyoamua kumsahau Hitler pamoja na mazuri aliyoifanyia nchi yake, Tanzania tunapaswa kumsahau Magufuli pamoja na mazuri aliyoifanyia nchi yetu.

Tuangalie mbele sasa. Tusahau yaliyopita, tuachane na kulinganisha uongozi wa sasa na uliopita. Tuvunje magenge. Tuanze upya.

The world and your country need YOU now, not Hitler, not Magufuli.
Wewe jizi nyamaza,

JPM hatosahaulikana daima utakufa lakini JPM ataendelea kutajwa na wewe hutakuwa na nafasi yoyote ya kumbukumbu popote pale.

JPM aliwafanya mbaya majizi, wababaishaji, mafisadi, wahuni, wavivu nk sasa hivi yanajitokeza kuropoka ujinga. Huyo mama yako akiondoka hakuna mtu atakayemkumbuka kwa chochote.

JPM shall prevail in the citizens' memoirs for decades to come, and nobody from all fronts dares to stain his excellent record and survive the damage of his/her career as a politician, academician, renowned business figure, engineer, lawyer, successful entrepreneur, professional of any field, etc.
 
Wewe jizi nyamaza,

JPM hatosahaulikana daima utakufa lakini JPM ataendelea kutajwa na wewe hutakuwa na nafasi yoyote ya kumbukumbu popote pale.

JPM aliwafanya mbaya majizi, wababaishaji, mafisadi, wahuni, wavivu nk sasa hivi yanajitokeza kuropoka ujinga. Huyo mama yako akiondoka hakuna mtu atakayemkumbuka kwa chochote.

JPM shall prevail in the citizens' memoirs for decades to come, and nobody from all fronts dares to stain his excellent record and survive the damage of his/her career as a politician, academician, renowned business figure, engineer, lawyer, successful entrepreneur, professional of any field, etc.
Wewe ni shabiki, huhitaji kutumia akili
 
Kati ya watu wameongea kitu cha maana ni wewe watu wamebaki kuzungumzia mzoga kila siku unatusaidia nini mama ni Bora maraelfu ya maguful
Panya aliehai ni bora zaidi mara mia kuliko simba aliekufa, hata kama panya huyo anakutafunia mahindi yako ghalani!
 
Back
Top Bottom