Sitaandika mengi Leo,
Watanzania tujifunze kutoka Libya na pia tusisahau kufuatilia historia ya utajiri wa U.S.
Ila yangu ni haya,
Tusimsikilize U. S kwa lolote kwani U. S hajawai kuwa mtu mwema.
Huwa ni mtu wa ku take advantage nyakati za vita na nyakati za uchaguzi. Rejea vita ya kwanza ya dunia, vita ya pili ya dunia na vita za wenyewe kwa wenyewe katika nchi mbalimbali.
lakini pia msisahau kurejea hotuba zao kile kipindi cha mwanzo wakati China anapambana na corona huku wao wakichekelea kwamba uchumi wao utaoenda kupanda kwa kasi. Na wakawaahidi China watatengeneza dawa.
Hizi ndio dili za hawa jamaa kuuza silaha wakati sisi tumekorofishana huku wao wanachukua mali zetu.
Rejea Libya tuache ushabiki wa kuwashabikia angalia kizazi chako cha mbele.
Lazima tutumie mbinu zetu wenyewe kutoka nchi zilizo jipatia maendeleo kwa njia halali. Maendeleo yaliyopatikana kwa watu kufanya kazi kwa bidii.
Zipo nchi nyingi.
Na swala la maendeleo ni vitu ni muhimu sana kwani tunahitaji miundombinu imara ili watu wawe na maendeleo.
Lakini pia tukumbushe viongozi wetu kuwa mifano bora hasa katika kuwaunganisha watanzania badala ya kutumia kauli mbali mbali za KUWAGAWA WATANZANIA.
Kama kupigana vita basi tunapaswa kuungana ili tupambane na adui yetu ambaye kwa muktadha wa bandiko lako ni huyu U.S.
Kiukweli, mfumo wa sasa umeligawa Taifa kwa ITIKADI za kivyama, dini, na ukabila ukilinyemelea Taifa.
Katika hali hii, tunampa nafasi adui yetu ya kutuchonganisha, vongozi wetu waambiwe UKWELI.
Ifahamike kuwa kazi ya viongozi/uongozi si KUWAGAWA watu, ni kuwaunganisha watu ili maendeleo yanayodaiwa yapatikane.
Kauli za viongozi wetu, unyanyasaji wa wazi wazi unaofanywa na tabaka tawala dhidi ya watawaliwa na wenye mitazamo tofauti ni dhahiri shayir vinapsawa KUKEMEWA KWA NGUVU ZOTE.
LAZIMA TUPENDANE, TUSHIRIKIANE, TUAMINIANE, TUSHIKAMANE ili tuwe wamoja na kuepukana na adui yeyote, awe wa ndani au wa nje ya nchi anayeweza kupenyeza sumu ya kutugawa na hatimaye kuingia katika machafuko yasiyo ya lazima.
NB; KUHUBIRI AMANI HALI YA KUWA HATUTENDEANI YALIYO YA HAKI, ni sawa na kuitaka pepo hali ya kuwa unaogopa kifo