Dan Zwangendaba
JF-Expert Member
- Apr 25, 2014
- 6,607
- 9,171
Katika kitabu cha Qur'an, aya ya 80, katika Sura ya 20 inasema:
"Enyi Wana wa Israili! Hakika tulikuokoeni na adui yenu, na tukakuahidini upande wa kulia wa mlima. Na tulikuteremshieni Manna na Salwa"
Kwa kiingereza:
O ye Children of Israel! We delivered you from your enemy, and We made a Covenant with you on the right side of Mount (Sinai), and We sent down to you Manna and quails:
Kwamba, Mungu aliwaneemesha mnoo wana wa Israel kiasi cha kuwapa chakula cha Manna na Salwa. Lakini wapii, hawa watu hawakuwa na shukrani hata chembe. Kilichotokea na kuwakuta, wana historia wanajua zaidi.
Mfano wa Wana wa Israel hauna tofauti na watanzania wa sasa hasa hili kundi la watu wa kipato cha kati na wapenda vyeo katika nchi yetu. Kundi hili linajumuisha watumishi na wafanyabiashara, na ndani yao kuna wala Bata. Lakini pia wamo wanasiasa.
Sote ni mashahidi, tangu Novemba 2015 Hadi Machi 2021, kulikuwa na chuma kilikuwa madarakani na kilikitumia kisawasawa cheo cha raia Na. 1 wa nchi. Watumishi wa umma walipigwa pini zote, hakuna cha mishahara wala nini. Wanasiasa ndio kabisa, na nchi walikimbia. Kwenye biashara huko ndio usiseme. Kila uchao ni kikosi kazi kimefunga ofisi. Kariakoo was almost dead! Wakulima nao hawakuachwa nyuma, kulegalega kwa diplomasia hakukuwaacha salama wakulima. Uuzaji wa nafaka nje ulizuiwa na hivyo mahindi yalikuwa gunia Hadi 20,000; mchele haukuwa na bei na wale wenzangu na mie wa kusaini hawatasahu jinsi walivyokata mitaji yao mbele ya macho ya mabarangabaranga.
Na sisi wa kaskazini pia hatukubaki salama na sekta yetu ya utalii. Arusha ya Oktoba 2015 kurudi nyuma sio Arusha ya baada yake. Mahotel makubwa yaligeuzwa hostel mbele ya macho yetu. Vitisho vya bastola mbele ya media halikuwa jambo la maajabu. Hamo rapa huenda ni shuhuda halisi wa hali hii maana wengine hatukujua kama ana kipaji kingine cha riadha. Wanufaika wa Loan Board hawatasahau jinamizi la retention fee. Kwa kifupi kila mmoja alipata size yake.
Pamoja na kumpenda sana Raia Na 1 wa awamu ya 5, Mungu alimpenda zaidi huenda kwa ajili ya kwenda kutimiza ile ndoto ya kuchunga Malaika huko mbinguni. Mwanamama kutoka Kizimkazi Mkunguni alichukua nafasi kama Na. 1. Huku mtaani tunajiambia, familia akifa baba itayumba ila itasimama na kutembea ila akifa mama, familia inaparaganyika. Kweli, pamoja na kuyumba hapa na pale kama nature inavyosema ila kiukweli familia ilisimama na inaenda.
Miradi yote ambayo mtangulizi alihofu kama itatekelezwa pasipo yeye, baadhi imeisha na mingine inaendelea. Hakuishia hapo, akaweka rekodi zake mwenyewe kwa kuamini kuwa kujenga Tanzania kunahitajika vijana waende shule. Mama akajenga shule ambazo hatujawahipo kuziona. Sisi watu wa vijijini tulizoea madarasa ambayo tukichelewa tunapangua matofali, tunazama ndani. Lakini leo vijijini kuna madarasa yenye fani. Huko mahospitalini ukiandikiwa kipimo cha MRI, basi ilikubidi kusubiri miezi Lau kama una haraka uende Nairobi. Madokezo huko maofisini ndio kazi pekee inayofanywa kwa nguvu zote. Wakishamalizana na madokezo na kuongeza zero, wanaenda kukaa kwenye viti virefu na kumtoa mama akili. Kariakoo imerudi tena ikiwa na soko kingine jipya.
Huduma za maji zimeboreshwa kuliko wakati wowote wa historia ya Tanzania. Lakini watanzania ukiwakuta wanavyomsema mama, utadhani huko nyuma walikuwa na kila kitu bora ila tarehe 17 Machi yalipotea yote. Wanasiasa waliokuwa uahmishoni wakarejea na wanaendelea na maisha yao ingawa wengine walilipa fadhila kwa kutukana matusi na kashfa. Yes, hatufanyi wema kwa ajili ya kusubiri malipo ila inauma kwa unayemtendea wema asipoona wema wako.
Kule mwendokasi, alianza na kubadili ma CEO kila uchao, lakini alipoona sio tiba, kaleta maono yake ambapo kwa dalili tu kuna muelekeo wa kuboreka kwa huduma hii.
Mama alikuwa na jambo moja kubwa katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wake: kutekeleza ilani ya CCM ya 2020 ikiwa ni pamoja na kukamilisha miradi ya mtangulizi wake. Jambo hilo amefanya kwa kiasi kikubwa japo mapungufu yanaweza kuwepo. Kwa kifupi, mama amewafanyia watanzania kila kitu bora ambacho raia Na. 1 bora yoyote angefanya. Sekta zote amegusa ikiwemo ile sekta ya kukuza vijiwe vya kuponda uongozi( Bar, na avijiwe vya kitimoto).
Lakini kama nilivyoanza hapo juu, maombi ya shari huwa yanajibiwa haraka kuliko heri. Watanzania mmepata bahati ya kuwa na rais ambaye hana "class mates" huko. Uchumi wenu unakwenda. Cha jioni kinapatikana japo kwa mbonde. Mungu akishusha gharika, mama anawajengea nyumba mpya. Tupo hapa, tutamkumbuka sana mama baada ya kumaliza kipindi chake 2030 na kutamani style ya uongozi wake. Mungu Ibariki Tanzania.