Watanzania tumekuwa wajinga wa kuwatukuza Viongozi hata pale ambapo hapastahili. Kujipendekeza tu

Watanzania tumekuwa wajinga wa kuwatukuza Viongozi hata pale ambapo hapastahili. Kujipendekeza tu

Humu kuna thread inasema "Rais Samia atoa shilingi bilioni 300 kukamilisha ujenzi majengo ya Serikali Dodoma". Hii ilishamiri zaidi kuanzia awamu ya tano na hii ya sita ninaona kama inaendeleza kwa kasi sana.

Utakuta hata Diwani na Mwenyekeiti wa Serikali za Mtaa anapoongelea fedha zilizotolewa na Serikali au jambo lililofanywa na Serikali wanaliunganisha na kutendwa na Mheshimiwa Rais.

Hii kwangu mimi imekuwa inanisumbua. Badala ya kusema tu kuwa Serikali imefanya hili au imetoa fedha basi fashion imekuwa ni jambo hilo limefanywa na Mhe. Rais au kitu hicho kimewezeshwa na Mhe. Rais.

Watanzania tumekuwaje? Hivi tumeshindwa hata kuelewa kuwa wananchi ndiyo kila kitu na wapo juu hata ya Rais? We are the people to make or unmake the government.

Yaani kadri siku zinavyoenda tunashindwa sana kujitambua! Na Ndugai kuomba msamaha wa namna ile ndiyo katengeneza precedent mbaya kabisa.
Ulikuwa na miaka mingapi enzi ya utwala waNyerere?
"Zidumu fikra za Mwenyekiti wa CCM",
Naomba kuwasilisha,
RENEGADE.
 
Kinachotakiwa ni kufuata utaratibu wa bajeti. Haiwezekani kusema fulani ametoa kiasi fulani cha fedha kutekeleza mradi fulani HAPANA. Fedha zote zinazotumika zimepitishwa na wabunge kwa mwaka unaohusika. Ni vema tukafuata bajeti na usipofuata bajeti hapa ina maana kuna maeneo mengine wanakosa fedha iliyopitishwa kwenye bajeti yao. Sasa hivi kati ya Taasisi zinazopata taabu kwa kukosa fedha kutoka Serikalini kuendesha shughuli zao ni Halmashauri za Wilaya. Other Charges ni shida lakini fedha zipo kwenye bajeti na hawazipati. sasa ya nini kuwasumbua kutengeneza bajeti zao na huku fedha hizo haziwafikii?. Kitu cha maana hapa ni kufuata bajeti iliyopitishwa na Wahe. Wabunge. Yeyote atapata sifa kama anafuata sheria, kanuni na utaratibu kuhusu matumizi ya fedha za Serikali.
 
Humu kuna thread inasema "Rais Samia atoa shilingi bilioni 300 kukamilisha ujenzi majengo ya Serikali Dodoma". Hii ilishamiri zaidi kuanzia awamu ya tano na hii ya sita ninaona kama inaendeleza kwa kasi sana.

Utakuta hata Diwani na Mwenyekeiti wa Serikali za Mtaa anapoongelea fedha zilizotolewa na Serikali au jambo lililofanywa na Serikali wanaliunganisha na kutendwa na Mheshimiwa Rais.

Hii kwangu mimi imekuwa inanisumbua. Badala ya kusema tu kuwa Serikali imefanya hili au imetoa fedha basi fashion imekuwa ni jambo hilo limefanywa na Mhe. Rais au kitu hicho kimewezeshwa na Mhe. Rais.

Watanzania tumekuwaje? Hivi tumeshindwa hata kuelewa kuwa wananchi ndiyo kila kitu na wapo juu hata ya Rais? We are the people to make or unmake the government.

Yaani kadri siku zinavyoenda tunashindwa sana kujitambua! Na Ndugai kuomba msamaha wa namna ile ndiyo katengeneza precedent mbaya kabisa.

Kwani tatizo Liko wapi. Wewe unapata Shida gani. Kama lawama zote unampa Kiongozi why not kumpa na maneno matamu na tena unaweza Kuta hata afuatilii.

Nachoona hapa, usiyejitambua Ni wewe, unahangaika na Minor things. Fanya kazi mkuu. Ishi maisha yako. Acha kuteseka. Tumwombee baba „ Mandela“ wa Tanzania. By the way kuna watanzania Pia wana Mandela wao. Vipi hujakereka.
 
Du. Hata imekuwasha kweli kweli!
 
Utasikia mama ametoa pesa kukamilisha mradi, wakati kimsingi ni pesa zetu ni Kodi zetu. Tulimtukuza sana Raisi aliyepita na kumvika umungu matokeo yake yalikuwa mabaya hata huyu tusipoacha kumtukuza tutapata matokeo yale Yale.Mungu hawezi kushiriki utukufu na miungu mingine.
 
Hakuna kiongozi wa kisiasa wa chama chochote mwenye vision ya kizazi kilichopo au kijacho viongozi wa kisiasa vision Yao ni uchaguzi ujao ndio maana tutaendelea kuwa masikini pamoja na utajiri huu mkubwa tuliopewa na Mwenyezi Mungu. Fanya research ....
 
Watanzani ni wa hovyo mda mrefu tu,,, wewe tu umechelewa kujua
Nashangaa kwa nini rais anawapenda wanaojikomba kwake?Mh Rais nilimsikia, na mimi najua kuwa urais ni Taasisi. Anatakiwa rais akanushe hadharani kuwa hana mfuko binafsi alipoweka fedha kuleta maendeleo. Kama hakemei basi anapenda kusifiwa sana
 
Back
Top Bottom