Watanzania tumezidi sana kumuonea mnyama Kenge

Watanzania tumezidi sana kumuonea mnyama Kenge

The Mongolian Savage

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2018
Posts
9,265
Reaction score
20,526
Mzuka wanaJF,

Mnyama Kenge kati ya wote anaonewa kudharauliwa na kuchukiwa sana na jamii nchini. Hii inaniuma kichizi.

Kenge hana madhara yeyote kwa Mtanzania lakini anaonewa na kudharauliwa wakati hana time na binadamu yeye anamind maisha yake in the wild.

Bado najiuliza hii dhana ya Mtanzania kumdharau na kumchukia mnyama kenge ilianzia wapi na lini? Kwasababu sioni kabisa ubaya wa Kenge na hana madhara yeyote.

Kenge kageuzwa tusi sasa unajiuliza kwa nini? Kenge siyo fisadi, kenge haibi, Kenge habaki, Kenge siyo Jambazi why why why this beautiful reptile is treated unfairly?

Tubadilikeni jamani tumtendee haki huyu mnyama ikiwezekana hata awe nembo yetu ya taifa!
 
Nadhani watu wanamuandama sana Kenge kwa sababu anakuwa anaingilia misafara ya mamba wakati hata haimuhusu.

Siku ambayo atakaa mbali na msafara wa mamba nadhani atakuwa salama zaidi na hata semwa tena!!
 
Kuna siku nakatiza mitaa ya Kwamtei Moshi, naona kundi kubwa sana la watu wazee, vijana na watoto pamoja na kina mama hawakuwa mbali!

Hata kupita nilishindwa maana walijaa barabarani sana, ikabidi niulize kuna nini hapa?

Jibu lilinichosha kabisa! Eti kwenye huo mti mkubwa kuna kenge wawili ndiyo vijana wanahangaika kuwaua na watu waliojaa hapo wapo kushuhudia!

Nikaendelea kudodosa, wamefanya uharibifu gani? Jibu ni hakuna, wanauliwa tu!

Naona ndicho ulichoandika, umeona mbali!

jon-stephano
 
Kwetu ni karibu na mto.
Siku nacheza namaliza kumlisha mtoto sebuleni nikiwa nimeacha mlango na geti wazi, he si walikuwa wametoka kumfurumusha huko akaingia mpaka ndani.

Nilijifungia chumbani na mtoto tena nikambeba tukapanda juu ya kitanda[emoji28][emoji28]

Raia wakaingia wakamfurumusha na kumuulia nje kuja mmoja akambeba na kudai anampeleka kwa wachina wamle maana alikuwa mkubwa na amenona nona sana.
 
Kenge ni kenge tu, mnyama ana mishe mishe kibao mara majini mara nchi kavu.Mla nyoka yeye,mla watoto wa mamba yeye nahisi ni mnyama anaeongoza kwa kula mayai kwa viumbe vyote vinavyotaga.

Kenge hafugiki ni kiumbe hakina shukurani ndo mana ukizingua kwenye jamii utaitwa Kenge.
 
Back
Top Bottom