Watanzania, tumpongeze Yusuf Manji kwa kuwa mzalendo na kurudi nyumbani. Rais Samia asichelewe, amuite Ikulu wazungumze

Nini kilimsibu Manji mpaka ahame nchi? Au ni yule yule marehemu aliowakimbiza akina Lissu na Lema?
 
Huyu ndio alimbambikizia mtoto wa Mengi drugs kwa Kua alikua na ugomvi na dr Mengi ili kijana akauliwe India , alichofanyiwa na jiwe ni karma

sasa ameludi Nchini Atatii sheria bila shurti kuna kipindi hii Nchi ilikua kama yake jiwe alijua kumnyoosha huyu muhindi fisadi
 

Kwa ajila zipi za mishahara ya elfu 80 ni bora vijana wakauze line kwenye mitandao ya Simu wanapata zaidi kuliko ajila za huyo tapeli
 
alipe kwanza kodi ya quality cenre. muhindi tangu lini akawa mzalendo africa. hao watu nimefanya nao kazi nawajua vzr sana. nenda kwa mo uangalie mishara ya wahindi na waswahili. ngozi nyeusi mnapenda sana kushoboka na ngozi nyeupe.
 
Naunga mkono hoja. Wakulima wa mbaazi, ufuta, alizeti na mazao mengine huko Mtwara, Lindi, Singida, Dodoma hii ni habari njema kwenu.
 
🤝🤝🤝
 
Rostam alikuwa na upekee gani hadi akaigeuza Ikulu kama sebule yake kipindi cha Mwendazake? Yeye ndiye alikuwa Mfanyabiasha pekee nchi hii? Na akaamrishwa kabisa na Mwendazake akagombee ubunge Morogoro
 
Kwahiyo Mama Samia amemrudisha mwizi?
 
Roho ya kimaskini, kwa nini watu maskini mnawachukia sana watu waliofanikiwa?
 
Kama ni mwizi Mahakama zetu zimeshindwa nini kum convict? Manji yupo Tanzania na yeye ni kizazi cha tatu katika ukoo wao.

Babu yake alikuwa ndiye mmiliki wa Quality Garage pale Pugu Road ilivyokuwa inachonga mabodi ya mabasi yote nchini kuanzia UDA, KAMATA, SCANDINAVIA nk.

Mpaka mwaka 2015 makampuni ya Yusuf Manji chini ya Quality Group yalikuwa yanaajiri Watanzania zaidi ya 2000. Na alikuwa ndiye mnunuzi na exporter mkubwa wa mbaazi na ufuta.

Kama alikuwa na matatizo Basi yalipaswa yatatuliwe kwa maongezi na siyo kwa kumuundia kesi FAKE ili tu aishi rumande.

Unam traumatize Manji, anaondoka, wafanyakazi 2000 wanapoteza kazi, wakulima wanashindwa kuuza mbaazi, unakosa Kodi hata kama ni Kodi kiduchu. Je hiyo ni akili au mavi?

Hizi chuki za Mwendazake dhidi ya matajiri ndizo zimemkasirisha MUNGU wetu, ndiyo maana Mwendazake amekufa licha ya kuwa chini ya ulinzi wa hali ya juu na Madaktari full-time.
 
Chuki na visasi ni ugonjwa mbaya sana.
Chuki ni dhambi inayomua muhusika haraka Sana.RIP usimpenda kaja
 
Ndani ya Utawala wa shetani tza imepoteza jumla ya matajiri 6 kutokana na msongo wa mawazo.
 
Tuliambiwa MANJI anauza madawa ya kulevya
Anauza madawa ya kulevya wapi ? Yako wapi hayo madawa
Hii nchi Nani sio mwizi?? Haya Sawa , Manji alibanwa watanzania tulipata nn sasa zaidi ya Kila kitu kuwa terrible na uchumi kushuka huku tukidanganywa umepaaa....katika wizi huo aliokuwa anafanya Manji maisha yalikuwa mswano Sana ...... Kusema mtu Fulani anaibia nchi na kumbana vilivyo inatakiwa impact yake ionekane Kwa wananchi, tofaut ya kuibiwa na kutokuibiwa iwe wazi ...Kwa Tz ni vise versa..... Heri kipindi cha mafisadi na majambazi kuliko kipindi cha shujaa
 
Kama ni mwizi walishindwa nini kumfunga jela wakati Magufuli mwenyewe ndio alikuwa ni DPP na Jaji vilevile aliyewafunga jela watu wa Chadema kiuonevu kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…