Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,842
- 31,076
Tumeshuhudia kwa majirani zetu wa Kenya, uchaguzi ukihitimishwa kwa amani bila umwagaji wa damu yoyote, kwa maamuzi ya Mahakama ya upeo, baada ya kuidhinisha, matokeo ya Tume yao huru kabisa, kwa kumpa ushindi William Ruto.
Watanzania tuliokuwa tukiufuatilia kwa Karibu Sana, uchaguzi huo wa Kenya, tumejifunza mambo mengi mazuri ya kwa uchaguzi huo wa Kenya.
Nitaje mambo machache ambayo sisi watanzania ni lazima tujifunze, kwa hao majirani zetu.
1. Uchaguzi wao wa u-Rais, uliamuliwa na Mahakama ya upeo, jambo ambalo hapa nchini, haliwezekani kabisa, kwa kuwa kwenye Katiba yetu, imeelezwa kuwa Tume yetu ya uchaguzi ikishayatangaza matokeo ya u-Rais ndiyo uamuzi wa mwisho.
2. Kwenye uchaguzi wa Kenya, kuna wagombea binafsi, jambo ambalo hapa nchini kwetu, ndani ya Katiba yetu limepigwa marufuku.
3. Kwenye uchaguzi wa Kenya, waliruhusu vyama kuungana na kuweka mgombea mmoja wa u-Rais, jambo ambalo hapa kwetu halipo.
4. Hatujasikia kwenye uchaguzi huo wa Kenya, majina ya wagombea wa vyama vya upinzani yakikatwa na Tume hiyo, Ili kuruhusu wagombea wa chama tawala, wapite bila kupingwa.
5.Kwa majirani zetu wa Kenya, hatukuona yombo vya ulinzi, kama vile Polisi, wakiingilia uchaguzi huo, jambo ambalo ni tofauti Sana na hapa kwetu, ambapo tumekuwa tukishuhudia Polisi wakiingilia chaguzi zetu, kwa hiyo kufanya uchaguzi wetu usiwe huru.
6. Mahakama za nchi hiyo ziko huru kabisa, kama tulivyoshuhudia namna Mahakama ya upeo, ilivyoamua rufaa ya mgombea u-Rais Raila Odinga, ambaye alipinga matokeo hayo ya u-Rais kama yalivyotangazwa na Tume huru ya uchaguzi wa nchi hiyo.
7. Vyombo vya habari vya huko Kenya viko huru Sana, kiasi ambacho hata Kesi za kupinga matokeo ya u-Rais, yanaonyeshwa live kupitia vyombo hivyo.
Tumepata funzo kubwa Sana kutokana na uchaguzi wa Kenya na tumethibitishiwa bila ya shaka yoyote, kuwa nchi inapokuwa na KATIBA bora ya nchi, ndiyo suluhu ya Kudumu ya kuepuka nchi hiyo na machafuko ya kisiasa yanayoweza kutokea kwa nchi kuwa na Katiba inayokipendelea chama kimoja pekee cha kisiasa, ambacho ni chama tawala.
Ni vyema wananchi tukapewa Uhuru wa kuwachagua viongozi wetu wanaotuwakilisha, badala ya watawala wetu "kuwasimika" viongozi wetu.
Mungu ibariki Tanzania.