Watanzania tunaoishi nje ya Nchi ( Diaspora) Tukutane hapa

Watanzania tunaoishi nje ya Nchi ( Diaspora) Tukutane hapa

Mi naishi Nje ya Nchi tokea mwaka juzi tokea mwaka juzi (2016). Nilipata bahati ya kusoma master Nchini ubeligiji miaka ya 2013 baada ya hapo nikaja bongo nikatafuta kazi sikubatika, Kuna mwana mmoja Mghana tulisoma naye Ubeligiji akanipa mchongo za kaz kufundisha english China. Nikaaply kupitia wechat kwa maagent.wakapenda accent yangu nikaenda China..Nilianzia kufundisha Shanghai, baadaye HUbei, tena XIAN. Mungu siyo Ruge mwaka jana nikapata kazi nyingine nzuri tu siyo ya kufundisha tena. Wachina wengi hawajui english ukiweza kuongea english ya kimarekani yoyo yoyo, wasup wasup unapata kaz ya kufundisha.

Nipo pia nafanya mchakato wa kwenda Canada..niliomba visa yao kupitia Skilled worker but requirement zao zinahaji uwe na job offer kwanza..sasa nipo natafuta admission ya phd tu kupitia Canadian scholarship. Canada and Australia wanatafuta smart people hasa ukibahitika kufika huko kupata P.R ( Permanent Resident) siyo ngumu sana. Wanasayansi mnahitaji sana Canada. Pitieni hapo website ya immigration ya canada (Immigration and citizenship - Canada.ca )

Unaotaka kujaribu kazi za kufundisha China english fanyeni yafuatayo download wechat ( hii ni km whatsapp). Alafu zitembelee sites hizi China Jobs – Job Opportunities for Expats in China|外籍招聘网|外教招聘|招聘外国人|外国人招聘网|外籍人才网 - eChinaJOBs au the Beijinger | Newest Classifieds posted today | Beijing classifieds, forum, directory, blog, and more (kwa beijing tu) Kwanini udownload wechat kwakuwa maagent wengi wanaotafuta waalimu wanatumia wechat..sasa unachokifanya ni kumu add ( request friendship) then unamwambia natafuta kaz za kufundisha english..wengi wanataka Native usichanganyikiwe na hii, mwabie agent wewe ni Mtanzania but umekulia Canada/USA/U.K/AUSTRALIA AU new zealand....atakuambia mtumie intro video record..Hapo sasa ua kabsa..Ongea kwa swaga km mzungu(sema jina lako, unaishi wapi now, sema ushafundisha english watoto wadogo na adults, hakuna prove utahitajika kuonesha), make sure uwe wewe. Ile clip yako wakiipenda China umeingia mapema sana. ( waghana,cameroon, naigeria/wazimbabwe wanafanya sana kazi hizi). Maisha ya China yapo cheap sana Yuan 1400 tu kwa kula, usafiri, bia, kuhonga (hii subjective..hahaha), Yuan 1400 ni km laki 5 kasoro ya kitanzania. Huhitaji kuwa na masters/phd/ education degree kufundisha..unahitaji kuwa na english nzuri tu utapata kazi ya kufundisha.

Okay, kwa wale wanaotaka kuja kwa njia ya kusoma..ni simple tu,
tembelea tovuti hii SmartAdmin (AngularJS) kuna scholaship( sorry sijajua km deadline bado ipo kwa mwaka huu...), au hii MOFCOM Scholarship China 2018 - Chinese Government Scholarships ( hii unapitia pale Ubalozi mdogo wa china Tanzania upo Karibu na Kanisa la St.Peters, hahahah ukifika maeneo ya Jaa upigwe( Forex) pale Jangid Plaza) unakwenda mbele, na hii 欢迎访问国家留学网!

kwa schoralship za Nchi mbali mbali duniani check sites hizi...

1- Opportunities For Africans | Connecting Africans to the Latest Life Changing Opportunities
2- International Scholarships for International Students from Developing Countries 2017-2018
3- Scholarship Positions 2018 2019 for Undergraduate Masters PhD Courses

NB: Jamani Tanzania kuna fursa nyingi sana, but fursa hizo ili uweze kuzi tap lazma uwe na mtaji mkubwa sana. Mfano kuna fursa kubwa kwenye Kilimo but unahitajikaji uwe nauwekezaji mkubwa km wa tractor, irrigation system na masoko yawe stable..sasa hivi kimsingi unahitaji Mzigo wa/capital ya kutosha.Kukaa nje ya Nchi siyo kutokuwa mzalendo..Km hauna Ishu Tanzania bora uje upambane nje ya Nchi utapata Exposure, na hata mtaji ambao unaweza kuwekeza nyumbani..au kipato ambacho utasaidia Ndugu. Sisi vijana mama na wadogo zetu wanatutegemea sana, Binafsi mimi mama na baba yangu hawana uwezo nataka katika umri wao huu na wenyewe wa enjoy kidogo maisha.

Kujua jinsi ya kupata visa za aina zote kwa Nchi mbalimbali tembelea hii forum ya wanageria( jf yao) wanafunguka sana wenzetu Travel - Nigeria - Nairaland

Wale wanaoishi EUROPE/USA/ASIA/AMERICA njooni basi mfunguke njia gani vijana watumie ili waruke sehemu popote unapoona kuna fursa. Kama kunamtu yupo canada ebu funguka unayoyajua pia. Fungukeni au wekeni hata masites ya kijanja hapa:

najua uzi km hizi za maana huwaoni watu..ila ningeandika tuliowahi kufumaniwa tukutane hapa watu wangejaa..
Safi sna kiongozi watanzania wote tungekuwa km ww leo tungekuwa mbali sna kiongozi mie binafsi nipo Cape Town South Africa
 
Vipi kupiga box hakuna huko??,nataka nije mambo ya kufundisha sio issue
 
Ndege yenyew sijawahi kupanda.
Hongereni watanzania wenzangu mliopo nje ya nchi. Mmepona mambo mbali mbali yanayoendelea huku kwenye sirikali yetu.
Tuachane na hayo NAOMBENI MNITAFUTIE MCHUMBA HUKO na Mimi siku anitumie nauli nikamtembelee.
Kingereza nitajifunza.
Asanteni
Nitakupeleka mimi
 
Uzi mzuri isipokuwa kuna baadhi ya wachangiaji Kama vile hawapo serious. Jamani huu uzi tuwaachie wanaotafuta namna ya kwenda nje ya nchi kutafuta maisha,kama huna cha kuandika ni bora ukabaki kuwa msomaji na sio kuharibu uzi.
 
Back
Top Bottom