Mama na serikali yako mnaulizwa na watanzania juu ya ule ujenzi wa meli mpya "MV Mwanza" Hapa kazi tu iliyokuwa ikijengwa pale Mwanza ni nini kinaendelea kwa sahivi. Ile meli ilitakiwa kubeba abiria 1200 na mizigo tani 400, ni meli ya safari kati ya Mwanza, Bukoba na Entebbe.
Tunajua ujenzi ulianza 2018 september na ilikuwa ni mkataba wa miaka 3 maana yake hadi 2021 mwezi wa september tulitakiwa kuwa na meli mpya ziwani ikifanya kazi na kurahisisha safari za abiria na mizigo. Leo hii hatusikii tena wala kuambiwa lolote na walioko Magogoni, tunaomba kujuzwa ujenzi umeisha kwa %??