Watanzania tunapaswa kuambiwa na kujua ukweli kwamba Gesi inayochimbwa Mtwara si yetu

Paskali Bhana...sasa ulipoamua kugombea ubunge ulitaka ukaibadili hii janja ya Chama chenu sio??
 
Nyie ndio mnaliponza hili Taifa kwa kundelea kutetea CCM iliyotufikisha hapa.

Hiyo sheria iko tu ila sidhani kama hata inasimamiwa
 
Paskali Bhana...sasa ulipoamua kugombea ubunge ulitaka ukaibadili hii janja ya Chama chenu sio??
Mkuu mkulima gwakikolo , please hear me sababu zangu
Naa baada ya kutupa karata yangu, na nilichoambulia, kwanza nilikubali matokeo
Na kisha nikatoa maoni yangu
Na kweli mwisho wa siku, hicho nilichokizungumza hapo juu, ndicho kimekwenda kutokea, mkono mtupu haulambwi, wenye mikono mirefu ndio walioptishwa with few exceptions, hivyo sasa tusubiri
2025.
P
 
Nyie ndio mnaliponza hili Taifa kwa kundelea kutetea CCM iliyotufikisha hapa.
Mkuu Kishina cha Mshahara, Salary Slip , humu duniani hakuna kitu kizuri kama ukweli, the truth, na ukiwa mkweli mno sometimes, there is a price to pay!. Mimi ni kada wa CCM, ila ni miongoni mwa makada wachache ambao ni makada contemporary toka kundi la ma lumpen proletarians wakati CCM kama chama kimeshikwa, na kundi la ma bourgeoisies ambao ndio huamua kila kitu kwa ajili yetu. Japo ukweli huu ni mchungu ndio ukweli wenyewe, CCM ndio kila kitu!, CCM ndio Tanzania!, bila CCM hakuna Tanzania!. Nakuomba na wewe kuwa tuu mkweli toka ndani ya nafsi yako kwa ukweli kabisa wa dhati ya moyo wako, kuwa ni kweli CCM ndio imetufikisha hapa, lakini kwa vyama vilivyopo, hivi hivi vilivyo, kuna chama gani credible cha kuikabidhi ikulu yetu?. Nakuhakikishia, hakuna!. Sasa kama kilichopo ni CCM only na hakuna kingine, then what?. Jibu ni CCM only!. Kubali, kataa!.
P
 
Kuna vitu eidha unachanganya ama unaandika kishabiki.

1. Nisaidie kujua hao artmas walikua wanazalisha umeme kisha wanaupeleka wapi na plant ya kuzalisha umeme ilikua imejengwa wapi?

Kwa kumbukumbu zangu kampuni iliyosaini HGA ni Wentworth mwaka 2004. Kampuni hiyo ikauza hisa zake 51% kwa M&P mwaka 2009 ila hadi kufikia 2015 M&P walikua na 60% na hao Wentworth wakiwa na 40% za exploration ownership ya Mnazi Bay.

Kwa kumbukumbu zangu pia ni kwamba Wentworth anamiliki 31% shares, M&P 48% na TPDC anamiliki 20% ya operations.

Kuna tofauti kati ya exploration ownership na operations ownership.

2. Unalinganisha vitu 2 tofauti, kwamba nani atabeba gharama za bwawa. Ukatolea mfano daraja la kigamboni.

Daraja la kigamboni limejengwa kwa hela za wafanyakazi waliokua wanachangia hela zao NSSF hivyo zile hela sio za nchi, ni za wafanyakazi hivyo lazima zilipaswa kurudishwa. Bwawa la Nyerere linajengwa kwa kodi za wananchi walipa kodi, hizo serikali ina mamlaka ya kuzitumia itakavyo kwa maslahi ya watu wote ama ya nchi.

Hivyo gharama za bwawa tayari zinabebwa na wananchi wote sio kama hela za NSSF hizo ni za wafanyakazi wamekatwa kwenye mishahara yao na sio kodi ile.

Kuna mambo umeandika kishabiki hadi inatia shaka jinsi unavyofikiri. Huoni faida ya bwawa zaidi ya umeme, ila husemi ni umeme wa bei nafuu, umeme wa maji Duniani kote ndio wa bei nafuu kuliko kitu chochote, sasa wewe huelewi kwamba kukiwa na umeme wa kutosha na wa bei nafuu kutasisimua sekta nyingine za uchumi?

Hilo la kwanza, bwana wa mtera lilijengwa anablengo lake ilikua kudhibiti mafuriko ndio baadae ikaja wazo la kuweka ama kuzalisha umeme, je toka Mtera imejengwa umewahi kusikia mafuriko hilo eneo?

Kwa msingi huo bwana la Nyerere litasaidia kuzuia mafuriko kama yale yaliyotokea mwaka jana huko Rufiji, huoni hii kama ni faida, wewe unaona umeme tu?

Ukiachia kudhibiti mafuriko, kuna uvuvi, utalii, kilimo cha umwagiliaji kwani kunakua na uhakika wa maji ya kutosha maeneo ya jirani, hilo huoni kama ni faida, wewe faida unayoiona ni umeme tu.

Jambo la tatu ni kwamba bwana linategemea kuwepo zaidi ya miaka 50 ijayo, hiyo gesi unayoisema ikianza kuchimbwa kwenye large scale haiwezi kuwepo zaidi ya miaka 20, itaisha ila maji hayaishi Duniani.
 
Yanekuwa hayo tena! Looooooohhhhhh!
 
Aseeeeeee! Yaani umemalizia kishabiki kweli! Mungu anakuona lakini MCCM mwenzangu!
 
Nakuelewa sana kaka, ndio maana nasema mwendazake hakuwa na nia njema. Angeamua kutulia na kusikiliza ushauri tungekuwa mbali sana..
Hao watu ni wapotoshaji na genge lao issue ipo hivi.

Chukulia wewe una shamba pori hekari 10000 huna hela za kuliendeleza.

Anakuja mwekezaji na offer ya kukodi matumizi ya shamba faida mgawane mpaka arudishe hela yake.

Sasa akianza kulima hilo shamba kuna economic benefits maana atanunua mbolea, pesticide, ataajiri watu na faida zinazotokana na kilimo.

Upande wa pili ni makubaliano yako na mwekezaji let’s say kuwekeza inabidi atumie billioni 10 ambazo kutoka mfukoni kwake 3 na 7 kakopa bank kwa miaka 15 high interest. Ambapo kila mwaka anatakiwa arudishe million 800 za bank na yeye billion 3 yake kaigawa kwa 15 ambapo kila mwaka anataka millioni 200.

Mavuno ya shamba faida kila mwaka ni billioni 1.8, sasa kabla amjafanya chochote inabidi kwanza mlipe bank million 800 + na millioni 200 yake. Baada ya hapo kwa sababu wewe umetoa hela yako unataka upate millioni 500, yeye apate millioni 300.

Mwaka ambao mavuno sio mazuri labda mmepata billioni 1.4 utaratibu ni uleule bank na yeye lazima watoe billioni 1 yao; na hiyo millioni mia 400 inayobaki kwa sababu aifikii zawadi yake anaweza sema mwaka huu nachukua 300 nakupa 100. Ila 200 iliyobaki mwakani inabidi tufidie on top of 500.

Ni hivi serikali sio kwamba aijui economic benefits, majadiliano yapo kwenye makubaliano kati ya mwekezaji na mwenye shamba wanagawana vipi na ukikosea utaumizwa sana and those finance are more complicated kuliko huo mfano wa shamba.

Hao watu wakiongozwa na Zitto wanapotosha na kutumia hoja za economic benefit za jamii kama pressure serikali iingie kichwa kichwa na kuingia mkataba mmbovu.
 
Doo na mradi wa umeme wa MWALIMU NYERERE H.E.P naona unaenda kutupa hadithi zile zile
 


Shida ni elimu yetu ya sayansi na teknolojia ni ndogo au ya kukopi au hatuna wataakanu competent katika nyanja nyingi na hatuna UZALENDO toka kwa viongozi hadi sisi wananchi wa kawaida.

Ngoja nikupe mfano hai; hivi sisi kama nchi hatuwezi kuwa na kampuni ya ujenzi inayoweza kutandika mataruma ya reli ya SGR??----- tufanye hatuna hayo makampuni, basi je ilishindikanaje hiyo kampuni inayojenga SGR kupewa Contract ya kujenga kutoka Dar hadi tuseme Moro tu ambapo katika umbali huo Makampuni yetu au wataalamu wetu wa ndani waweze kujifunza namna ya utandikaji ili utandikaji kutoka Moro--- Mwanza---Kigoma tufanye sisi wenyewe!!! , lazima kutakuwa na changamoto, mfano ujenzi wa madaraja na mahandaki, kazi hizo tuna subcontract.

Kifupi ni kwamba Ubinafsi na ujinga vimetuandama mno sisi Waafrika na ndio maana Wazungu wana take advantage.
 
Ok, hao wageni walitupa nini hadi tukawapa hiyo gesi wachimbe? Bila shaka kuna makubaliano na sisi tumefaidika.
Wageni a.k.a Beberu hawana shida na wewe, wao humaliza tu wenye dhamana.


Kwa Africa Viongozi ndio wenye nchi...ndio maana utasikia Nchi inawaambia Viongozi "mkiwa rafiki na sisi hatutaingilia mambo yenu"....na hakuna pepo wanayoipenda Viongozi kama kuachwa huru wafanyie Wananchi wanavyotaka.
 
Kama hujawahi kumiliki alamsiniliyo Mwadui, au Tanzanite iliyo Mererani...

Hata kwa gesi iliyopo Songosongo, Msimbati n.k itakuwa hivyo hivyo
 
TPDC wapewe tu kitambulisho cha machinga, ila na machinga walianzia Mtwara kwa hiyo ni sawa tu hata gesi tukiipata kwa mfumo wa kimachinga[emoji38]
Mnawaonea tuu hao TPDC.. Hivi tuna uwezo wa kuchimba na kusimamia visima vya gesi sisi kweli? Umeme tuu hapa miaka 60 bado unatuhenyesha ndiyo tutaweza visima vya gesi? Hata Waarabu na mafuta yao lakini kuyachimba walitafuta makampuni, sema wenzetu hawakuingia mikataba ya kindezi kama sisi.
 
If thst is the case hatuna haja ya kudrill gas yenyewe. Hi ni rasilimali ya maana safi katika maendeleo ya nchi. Shida kama ni utaalamu wa kuchimba gas yenyewe basi tusubiri mpaka tutakapokuwa na wataalamu wetu wenyewe. Kama ni gharama za uchimbaji na mitambo basi pia tusubiri mpaka tutakapokuwa tumekaa vizuri kiuwezo. Hakuna maana wala tija kuyaacha makampuni ya nje kujimilikisha hii rasilimali. Haiozi itasubiri tukiwa tayari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…