Kusema eti TPDC ni madalali tu, SIO SAHIHI!
Gesi iliyoanza kuchimbwa kwa miaka kadhaa sasa, ni ya Mnazi Bay.... hii ilichimbwa wakati wa Mkapa, na asilimia kubwa za hisa zilikuwa zinamilikiwa na Artmas waliokuwa wanazalisha umeme hukohuko kusini kabla hawajafungasha virago na kuuza hisa zao!!
Baada ya Artmas kuondoka, kwa sasa mwenye share nyingi zaidi kwenye hiyo gas ni Maurel & Prom wanaomiliki 48.6% ya hisa, Wentworth Resource 31.4%, huku TPDC unaowaita eti MADALALI tu wakimiliki 20% ya hisa!!
Sasa kama TPDC na hisa zao 20% ni MADALALI, hivi ni akina nani wale waliokuwa wanafurahia 16% ya hisa za kampuni za madini?!
Kwahiyo ni sahihi kusema wanamiliki stake ndogo ya hisa lakini sio kweli kusema ni MADALI tu!!
Kama mnaamini Nyerere Dam itawapa umeme wa bei rahisi basi itakuwa MNAJIDANGANYA kupita kiasi!!
REMEMBER, trillions of TZS zinatumika kwenye lile bwawa, na kiasi kikubwa kikiwa ni pesa kutoka private banks!!
Sasa ikiwa Daraja la Kigamboni lililogharimu less than TZS 500 Billion mnalipia ili ku-cover gharama za ujenzi, tena za kumlipa NSSF mwenye pesa zetu wenyewe, who do you expect will carry the burden of trillions being used in Nyerere Dam?
Jibu ni wewe na wenzako mnaodanganyana Nyerere Dam itawapa umeme wa bei rahisi wakati hata kuvuka daraja tu, unakamuliwa hadi watu wanakwepa kupita pale!!
Kama ni ya Msimbati, ndo hiyo ambayo nimekupa percentage ownership na kama ni ya kina kirefu ambacho bado haijachmbwa, yenyewe bado!!
Na kwa mujibu wa Sheria ya Mafuta na Gas ya mwaka 2015, MMILIKI wa VITALU VYA GESI ni TPDC! Kampuni yoyote, iwe ya nje au ya ndani, ikitaka kuchimba gas inatakiwa KUINGIA UBIA na TPDC, and not otherwise!!
At the time, TPDC itakuwa inafahamika kama National Oil Company, na kwa mujibu wa Sheria ya Mafuta na Gesi, inatakiwa kumiliki AT LEAST 25% ya share! So that having been said, it's all about TPDC financial ability to acquire even MORE SHARES!!
Man,
Natural Gas Industry may offer more than you think!! The problem watu mnaangalia gas industry katika eneo la uchimbaji peke yake!
Natural Gas Industry is an engine for other sectors of economy, na pia ina maeneo makuu 3:-
1. Upstream
2. Midstream
3. Downstream.
Upstream is very expensive to run, na HAKUNA Mtanzania anayeweza... hapa ndipo pale Muhongo alikuwa anaonekana ni mtu wa ovyo lakini ndo ukweli wenyewe!!
Na ukitaka kufahamu ni namna gani ilivyo expensive ku-run upstream level of the gas industry, ni ile plant inayotoka kujengwa kwa matrilion ya shillings! Hapo ndipo mtu anatakiwa kujiuliza unahitajika uwekezaji wa namna gani kuweza ku-recover zile trillions zinazotaka kuwekezwa just kwenye processing industry!!
Kwa mujibu wa Sheria ya Mafuta na Gas ya 2015, National Oil Company wamepewa EXCLUSIVE RIGHTS ya ku-run Mid and Lower Stream!!
Wewe ukiweza kuwa na ONLY 10% Market Share of Midstream Level, trust me, utakuwa the biggest billionaire in the country!
What entails Midstream Level?
Kwa mfano, kwa mujibu wa Sheria ya Mafuta na Gas ya 2015, kabla hatujaanza kukimbilia kufanya gas export, ni lazima taifa liwe limejitosheleza na nishati ya gas!
Na katika mpango uliopo, National Oil Company wanatakiwa kusambaza mabomba ya gas Tanzania YOTE, ili hatimae gas ifike moja kwa moja kwenye nyumba za watu, viwandani, na vituo vya kujazia gesi kwenye magari!
Shughuli ya Usambazaji na/au Usafirishaji wa Gas ni one of the Midstream Activities ambayo sheria inampa National Oil Company Exclusive Right ya ku-run hiyo midstream!!
Upstream, ambayo ndiyo National Oil Company hawajapewa hiyo exclusively right is just about GAS EXTRACTION, and that's it!!!
It's unfortunately nipo safarini, ningeongea mengi kuhusu midstream and downstream, na pia kuongea kwa mapana kuhusu Local Content... yaani Sheria inavyotaka ushiriki wa WATANZANIA kwenye midstream and downstream!!
Na sina shaka mara kadhaa watu wamekuwa wakisema Sheria ya Mafuta ya Gas ya mwaka 2015 ni MBOVU huku am certain wengi wao kama sio WOTE, hawajaisoma hiyo sheria but TRUST ME, shughuli za uchimbaji zikianza, lazima kutakuwa na ATTEMPT kubadili sheria kwa sababu, Google Financial Statement of any Major Global Oil and Gas Company you know, utakuta nyingi ya kampuni hizi huwa zinafanya hadi Midstream Activities huko wanakoendesha shughuli za uchimbaji!
Do that homework!!
Lakini pamoja na hizo Midstream and Downstream Activities ambazo NOC wamepewa exclusive right ya kuziendesha, pia take anothe homework kuangalia byproducts zinazopatikana kutokana na natural gas processing!!
Kukupa mfano mdogo tu, pale Mtwara panataka kujengwa Kiwanda cha Mbolea ambacho thamani yake ni AT LEAST 50% ya gharama za ujenzi wa Nyerere Dam (about TZS 4 Trillion as at 2020)! Tanzania HAKUNA kiwanda chenye thamani ya angalau 25% ya hicho kiwanda kinachotaka kujengwa Mtwara!
Byproducts zinazotokana na Natural Gas Processing, moja ya matumizi yake ni uzalishaji wa mbolea, na ndizo zitalisha hicho kiwanda!!!
To cut a long story short, Gas Industry itashindwa kuwa Game Changer kwa SABABU TU nchi yenyewe hii imejaa viongozi na watendaji wezi!! Wale Waarabu wakati wanaaza wala usidhani kwamba eti walikuwa wanamiliki shares nyiiiiingi kwenye mafuta na gas, hell no but still gas and oil changed The Arab World!! Na wao, ni kama sisi, walikuwa hawana hata ubavu wa kuchimba hayo mafuta/gas, wenyewe!!
Tatizo letu, linaweza kuwa kama Angola na Nigeria. Nchi ni maskini lakini viongozi na watendaji ndo matajiri wakubwa!! Na kama mnadhani Tanzania kuna ufisadi, basi hamjawahi kuona ufisadi! Subirini uchimbaji wa gesi ya kina kirefu ianze kuchimbwa, hapo ndipo hasa mtakapofahamu ni kwanini NIgeria inaitwa ndio Kinara wa Ufisadi!!
In fact, hata Waarabu na wenyewe ni Mafisadi Balaa sema tawala za kifalme zinafanya ufisadi uwe wa wachache, na hao wachache pia wanawafanyia maendeleo wananchi!!
Chukulia mfano mdogo tu wa Ibara ya 219 (1) ambayo inasema:-
Sasa tuseme wewe umepewa tenda ya ku-supply mabomba tu kwenye mradi wa ujenzi wa gas distribution infrastructure nchini kote!!
Ulishawahi kujiuliza hiyo tenda itakuwa na thamani ipi kwako!
Lakini hata kwa ibara ndogo ya pili, inayosema:-
Sasa tuseme unamiliki ONLY 25% ya hiyo kampuni inayoagiza bidhaa kutoka nje, kwa zile bidhaa ambazo hazizalishwi TZ, na kwa kuangalia ukubwa wa gas industry, hivi ulishawahi kujiuliza utakuwa unafanya biashara yenye ukubwa kiasi gani kwa hizo hizo 25% kama kweli ni zako?!
Sasa nikupe tatizo KUBWA la Watanzania!
Tutaendelea kulia lia hivi hivi "tumeibiwa! tumeibiwa" badala ya kujipanga!!
Kuja kushtuka, shughuli zimeshafikia peak, kampuni za uchimbaji zinahitaji supply ya Goods X, lakini HAKUNA Mtanzania hata mmoja mwenye kampuni inayoweza ku-supply kwa sababu miaka yote walikuwa wanalilia tu!!
Kitakachotokea, wanakuja Wajanja Wakenya, wanakuambia muanzishe kampuni ya hiyo wakati pesa HUNA! Lakini kwavile sheria inataka Mtanzania amiliki at least 25% Shares, kwenye MoU na Article Association mnayopeleka BRELA anakuandika unamiliki 25% ambazo kimsingi sio ZAKO, bali ni za Mjanja Mkenya atakayekuwa anakulipa tu vipesa kidogo sijui labda commission from your fake 25% SHARES!!
Hiyo ndo ile Muhongo alikuwa anasema HATUTAKI MADALALI!!
Anyway, keep dreaming kwamba Bwawa La Nyerere will be very special for y'all but whether you like it or not, hamna kitu pale zaidi ya huo umeme!!
Sasa si bora hata huo mnaoita Mradi wa Kifisadi wenye uwezo mkubwa sana wa ku-stimulate other sectors of economies zinazoweza kutoa ajira na fursa ya kibiashara kwa Watanzania wengi zaidi!!
What about Bwawa la Nyerere?! Ndo kwa mfano, umeme huooooo, umeshaanza kuwaka kutoka Bwawa la Nyerere... WHAT NEXT?
Akili za Kuambiwa...