Its orchestrated na viongozi wetu wenyewe,...anae hujumu mwafrika ni mwafrika mwenzie, hamna mtu mwingine, wewe umejiuliza hilo swali, mimi nakupa swali gumu zaidi, kwann waafrika tunaishi maisha ya ajabu sana despite miaka 60 ya uhuru? Bado zaidi ya asilimia 70 ya watu wanaishi umasikini wa kutisha sana, nyumba za ajabu, maji ya shida, miji yetu haijapangwa, elimu duni that will never transform us or our mindset, uharibifu wa mazingira, etc, just ask yourself why?
Mungu ametupa resources nyingi sana, zimetusaidia nini? Zaidi sana viongozi wanaingia mikataba ya kuumiza vizazi na vizazi kikubwa wao wamepata 10%, kila bara duniani wamefanya progresses kubwa sana, waarabu, asians, etc except ngozi nyeusi tunahangaika na matatizo yale yale!!!!!! dhahabu, gas, ardhi, na resources zitakazo patikana in future hazitatukomboa. Ndio nature yetu, ni ngumu sana kupata viongozi wanaumia kuona vijana hawana kazi, watu mamillion wnaishi nyumba za tope, it doesnt bother them, political position kwao ni jackpot kutajirika. Ila mimi nasema tu Ole wao, sababu hawa masikini wanavyohaingaika na kufa maisha ya shida wakati Mungu aliweka resources hapa ziwasaidie, Ole wao, sababu kila nafsi pumzi itamtoka na hukumu inatusubiri, machozi ya hawa watu hayatapita bure.
after all, miaka 50 au 100 ijayo nani atakuwepo???, kiburi chao na kujiona wao wanafaa sana kuliko hawa masikini kitakuwa wapi? lakini hukumu ya Mungu haitawaacha, kila dawa feki au pesa ya kununua dawa unayokula, masikini anakufa kwa kukosa huduma hiyo damu inakusubiri. Furahi leo una madaraka lakini adhabu ya kaburi haitakuacha.