Watanzania tunapowasifia Kenya kwa Demokrasia pevu, pia tutafakari na hili

Na kwa maana yake halisi ya

"mpambanaji mwenye kutumia nguvu na akili yake kujitafutia,kwa njia za halali"

Hii haiko hivyo kwa hao woote walioko huko "UDA"

Tunawajua matajiri wa kenya ambao wametafuta na kutajirika kwa nguvu na maarifa yao halali, lakini hawa jamaa wa wheel barrow ni list ya wakwapuaji watupu.

Kwa mfano tu....Rutto-Youth kenya 92.
Mudavadi-Goldeberg scandal nk.

Usinitowe kwenye mada sababu ninaelewa target yangu,ila najuwa kwa wengi Tanzania vile hawapendi kuukemea wizi sababu ndio lifestyle yao kila siku.

Umaskini wa watanzania unasababishwa na "State Capture" ya vigogo wa CCM na washirika wao,wanaohakikisha mtanzania haelimiki na kujitambua haki zake ili wao waendelee kutajirika kwa wizi wa mali za umma.

Serikali imejaa "Asali Boyz tupu"

Hao ni wezi tupu!

Na hawatakasiki mpaka wanaingia makaburini,ingawa watakufa wakiwa matajiri,lakini watazikwa wakiwa mikono mitupu kama walivyoingia Duniani.
 
Hawa wakwetu siku wakisema zakwao hapatakalika hapa
 
Kuhangaika kwa aina gani?

Ruto na Rigathe wote ni vijana wa Moi, inawezakana hawakuzaliwa na wazazi aina ya Odinga na Kenyatta lakini nao ni matokeo ya wizi tu. Google kitu inaitwa YK92.
 
Kama Magufuli alimhonga ghorofa la bilioni 5 hawara wake pale Mwenge, imagine utajiri wake ulikuwa kiasi gani,
halafu anatuambia alikuwa rais wa wanyoge.

Hawa wanasiasa wanaojiita watetezi wa wanyonge ndio majambazi wakubwa
 
Kuhangaika kwa aina gani?

Ruto na Rigathe wote ni vijana wa Moi, inawezakana hawakuzaliwa na wazazi aina ya Odinga na Kenyatta lakini nao ni matokeo ya wizi tu. Google kitu inaitwa YK92.
Naijua hiyo "YK92"

Moi(R.I.P)aliingiwa na hofu ya kuupoteza uraisi wa Kenya pale ilipoanzishwa rasmi siasa ya vyama vingi nchini humo.

Na kwenye uchaguzi wa 1992,alimteua Rutto kuwa kiongozi wa Youth Kenya92.

Hiyo ilipewa jukumu la kuwatafuta na kuwashawishi vijana wengi waliokuwa na mlengo tofauti na KANU ya Moi,ili kuwashawishi wajiunge na KANUkisha kumpigia kampeni Moi nchi nzima dhidi ya wapinzani.

Rutto alilazimika kukatiza Masomo chuo kikuu cha Nairobi,na akaja kuanza jukumu hilo jipya(ingawa baadae alirudia na kuhitimu na kufikia PHD),akiwa amekabidhiwa mamilioni ya pesa ili kupenyeza pale anapoona kuna ugumu.

Huo ndio ulikuwa mwanzo wa umaarufu wa William Samoei Rutto Mwalimu wa sekondari kutoka Eldoret.

Na alipiga pesa ya kutosha,sababu shughuli ile haikuwa na Auditing yoyote kama zilivyo rushwa zote.

Hiyo fursa ndio ilimuwezesha kuijua kenya na kila kona na kuujenga mtandao ambao ameendelea nao mpaka leo hii.

Hii habari ya kuuza kuku ni ya nyuma zaidi, wakati huo akiwa shule za awali.
Ingawa mpaka leo anawaheshimu sana kuku,na anaendelea na ufugaji mkubwa.
 
Kwa ukwasi huo hapo juu ni wazi kwamba wakenya wameruka matope na kukanyaga maji.
Si afadhali wanao hata huo uhuru wa kuruka? Sisi tumezama moja kwa moja kwenye hilo tope na hatutoki kwani hata uhuru na uwezo wa kuruka hatuna.

Watoto wetu wamezaliwa kwenye tope, wamelelewa kwenye tope. wamekulia kwenye tope, wakakomaa kwenye tope na watazeeka kwenye tope!

Viongozi wanaoopolewa kwenye hilo hilo tope bila ridhaa zetu ndio hao hao wanaoapa kuhakikisha hatutoki kwenye tope hata kwa miaka mia!

Halafu kwa ujinga wako eti unaongelea utajiri wa viongozi huko Kenya! Masikini voicer, unaishi sayari gani? Au tope limekufunika huoni wala kusikia?
 
Ndio maana namshangaa huyo anayesema Ruto kahangaika
 
Kuandika kwangu ya huko Kenya,sio kwamba sielewi wizi ulivyotamalaki hapa kwetu.
Bali hii topic yangu kwa sasa imehusu ....treading story ambayo iko latest East Afrika mkuu!

Huwezi chambua ya jirani ukaacha kuyajua ya kwako.
Ninaelewa sana huku kwetu tunao "State Capture" na sasa wako kazini 100% wakiwatumia "Asali Boyz" wao chini ya Kinara "Rostam & Msoga Company"

Pia ninaelewa mpaka kiburi cha "GSM" Kinapotokea....
Ila hiyo ni mada ingine na wakati wakec bila shaka utakuwa mwingine pia.
 
Hueleweki point yako ni nini. Unataka kukanusha hawajatuzidi kidemokrasia? Unataka kutuambia wanasiasa wa Kenya wangekuwa masikini ndio kungekuwa na demokrasia? Unataka kutuaminishia Kila Mwanasiasa wa kenya aliye tajiri ni mwizi? Unataka kutuaminisha wanasiasa wa Tanzania sio wezi?
 
Bora Wakenya wanasema utajiri wa viongozi na kuweka wazi. Hawa wa Tanzania nani anajua wana ukwasi wa kiwango gani? Kwa vile wapo kimya ndiyo unadhani siyo mafisadi? Siku wakitaja utajiri wao si utazimia. Fikiria tena mara 2.
Bongo kila mstaafu anamiliki shamba na mifugo 😂😂😂
 
Huwezi chambua ya jirani ukaacha kuyajua ya kwako.
Ninaelewa sana huku kwetu tunao "State Capture" na sasa wako kazini 100% wakiwatumia "Asali Boyz" wao chini ya Kinara "Rostam & Msoga Company"
Hapo ndipo tatizo linapoanzia, kwako kunaporomoka unakimbilia ya jirani. Kenya wako kwenye right track, pole pole wanazinduka na kujitambua! Wanajua walikotoka na wanakotaka kufika na wanatambua njia ina visiki.

Sisi ni wapumbavu, hatujui kwamba hatujui. Tuko gizani na tunataka tuendelee kuelekezana humo humo gizani. Gizani hakuna tunachoona lakini hapo hapo tumekaza shingo tukidai tunajua tunakoelekea, really?

Are we being led by instinct like brainless animals or are we humans gifted with brains. Toka lini kipofu kaongoza kipofu na wakafika salama walikotaka kufika. Tuache kudanganyana, hatujui tuliko wala tunakoelekea.

Tumekazana kujenga miunguwatu na kutwa tunapiga vigelegele tukiwasifia viongozi wetu and for what? Wamefanya nini zaidi ya kutunyang'anya wananchi hata kile kidogo tulicho nacho? Who are we kiidding?
 
unafikiri viongozi went wa Tanzania hawala ukwasii huo? au kwa kuwa they fooling us around kuonyesha wao ni patriotics wakati ni mabeberu
 
Naona nia ya mleta huu uzi ni kuipaka matope demokrasia ya Kenya ili tusiione kuwa ni mfano wa kuigwa hapa Afrika. Kwani wagombea wote walikuwa mafisadi? Kama sio basi ni mfano wa kuigwa hata kama CCM hawataki tuwe na demokrasia.

President​

CandidateRunning matePartyVotes%
William RutoRigathi GachaguaUnited Democratic Alliance7,176,14150.49
Raila OdingaMartha KaruaAzimio la Umoja6,942,93048.85
George WajackoyahJustina WamaeRoots Party Kenya61,9690.44
David WaihigaRuth MutuaAgano Party31,9870.23
Total14,213,027100.00
Valid votes14,213,02799.21
Invalid/blank votes113,6140.79
Total votes14,326,641100.00
Registered voters/turnout22,120,45864.77
Source: IEBC
 
Ungesoma topic yangu yote ungenielewa,mimi nimelenga hasa jinsi wanasiasa wanavyotumia nafasi na madaraka kujitajirisha.

Kuwa na demokrasia huku ukiwa na wananchi maskini kuzunguka nchi nzima huko hakuna manufaa kwa mwananchi.
Manufaa yanabaki kwao hao hao mafisadi wakiwakaanga wananchi kwa mafuta yao wenyewe.

Hiyo Demokrasic ya Kenya iko kwenye majukwaa ya siasa tu,lakini sio kwenye maisha halisi ya mkenya.

Ukitaka kunielewa nenda huko kwa hustlers....Kawangwale,
Mathare,Kariobangi,kiritinithi,Kariokor na kwingineko koote mabandani kuzunguka Nairobi.
Ndio utajua ninachomaanisha!
 
unafikiri viongozi went wa Tanzania hawala ukwasii huo? au kwa kuwa they fooling us around kuonyesha wao ni patriotics wakati ni mabeberu
Ninajua jinsi viongozi wetu walivyo mafisadi,lakini leo nimeongelea hao wa huko kenya kwa sababu ndio Topic iliyoko mezani.

Ninaijua "State Capture" ya Tanzania inavyotunyonya na kututia umaskini watanzania.

Lakini thread yao itakuja tu!
 

Ww inaonekana una itikadi za kijamaa ambaye utajiri kwako ni kosa. Hao viongozi wa Kenya wameweka utajiri wao wazi na wanahojiwa. Mwenye mashaka na utajiri wao anapaswa kuwahoji. Sio hapa kumejaa majizi yanajiita mazalendo na wala mali zao hawazitaji.
 

Hauoni kwamba hao wanasema ukweli hawadanganyi ili bunge lifanye maamuzi sahihi, kuliko kudanganya. Hapa Tanzania hata kuulizia fomu ya kiongozi unakamatwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…