Watanzania tunapowasifia Kenya kwa Demokrasia pevu, pia tutafakari na hili


We huna hoja bali una nongwa. Naona hiyo demokrasia ya Kenya imekuuma ukifananisha na hii ya hapa.
 
VIONGOZI WA TANZANIA UNAUUJUA UKWASI WAO? WATAJE NA WAO TUFANANISHE
 
Bora Wakenya wanasema utajiri wa viongozi na kuweka wazi. Hawa wa Tanzania nani anajua wana ukwasi wa kiwango gani? Kwa vile wapo kimya ndiyo unadhani siyo mafisadi? Siku wakitaja utajiri wao si utazimia. Fikiria tena mara 2.
Hata kama hawasemi wana ukwasi kiasi gani, bado wanasiasa wa Tanzania wana kiasi cha mboga tu ukilinganisha na wanasiasa wa Kenya. Watu walisema Edward Lowasa ni fisadi lakini ukiwaambia wakuonyeshe vitu anavyomiliki au alikoweka fedha hawajui. Kuna kipindi Ridhiwani JK alihusishwa na kila jengo kubwa la biashara au malori long safari. Lakini baada ya kuja Magufuli Ridhiwani alikuwa mtu wa kawaida tu ambaye hana fedha zile tulizokuwa tunaambiwa.

Kenya Ufisadi na Siasa ni kama kifuniko na mdomo wa chupa. Tajiri ni tajiri kweli
 
Kwa hapa Tanzania hao wenye ukwasi na ulaghai hawapo?wewe ndugu yetu unaongea nini?
 
Uchumi wenu ni mdogo mtapata wapi matajiri wakubwa kulinganisha na matajiri wa kenya kwenye uchumi mkubwa?

Kutokua na matajiri wakubwa haiondoi ukweli kuwa hao matajiri wenu mlionao ni mafisadi ndio maana wanaficha taarifa za utajiri wao.
 
Hiyo 800 sio madafu ya kitanzania brother.

Ni kenya shilings.....

Kwa Tanzania hiyo ni sawa na 16 B.

Hiyo hela haifiki 20b tshs kama sikosei, sasa wingi wake ni upi? Kumbuka wengi wa hao wanasiasa wa Kenya ni wafanya biashara. Achana na hawa akina Mwigulu hapa wanajificha kwenye tai ya bendera ya taifa kumbe ni wezi uchwara.
 
Utajiri unaosemwa na watu dhidi ya mtu na anaousema mtu mwenyewe ni vitu viwili tofauti.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Bora hao wanaojiweka wazi kuliko hawa wakwetu wanaoiba kimya kimya!pia ni hatari sana kuongozwa na masikini
 
Sasa tuorodheshee na ukwasi wa wanasiasa wa Tanzania! Si afadhali hao wameweka wazi kuliko akina Mwigulu na Makamba ambao wameficha na haujulikani!
 
Kwani Watanzania tunakamuliwa kidogo?
 
We huna hoja bali una nongwa. Naona hiyo demokrasia ya Kenya imekuuma ukifananisha na hii ya hapa.
Siongelei kuhusu Demokrasia hapo,bali naongelea ukwapuaji wa mali za umma kwa watu wanaopewa nafasi za kutuongoza katika taasisi zetu za umma.
Hiyo pesa huwa siyo ya serikali bali ni jasho la walipa kodi.

Demokrasia haimsaidii mtu aliye taabani kwa njaa.mfano upo hapo hapo Kenya.

Na pia sijasema kwamba Tanzania hatuna wezi,hapa kuna wezi wengi na ndio hao wamefanya "State Capture" na tukiwasema mnatuambia tunasumbuliwa na njaa....
 
Sasa tuorodheshee na ukwasi wa wanasiasa wa Tanzania! Si afadhali hao wameweka wazi kuliko akina Mwigulu na Makamba ambao wameficha na haujulikani!
Na hiyo ndio unasikia ikiitwa 'state capture"
 

Hao watu wana pesa na wanazitaja wala hawafichi ili kama una mashaka na vipato vyao liwekwe zuio. Kama unaona hakuna zuio ina maana wafu wameridhika na vipato vya hao wazee.

Unasema demokrasia haimsaidii mtu mwenye njaa, kwani udictator ndio unamsaidia mwenye njaa? Si bora hapo Kenya mtu anaweza hata kuchagua amtakaye na sio kuwekea ? Muwakilishi na mtawala?
 
Mbona walimchagua Raila lakini wakawekewa Rutto na Chebukati kwa nguvu ya Pesa?

Unapokuwa huru lakini una njaa,ni tatizo kuliko kuwa umeshiba ila hauko huru.

Demokrasia inayotafutwa ni kwa lengo la kupata uhuru wa kila mtu kuishi,kusema na kupata haki ya kusikilizwa bila kujali tabaka lake.
Na hivyo kufuragia maisha yake,huku akipata huduma zote za kijamii kwa mujibu wa katiba ya nchi.

Lakini kwa wanasiasa katiba wanayoitaka ni e itakayowarahishia njia ya kupata madaraka na kuendeleza uporaji na kujitajirisha.

Kenya kuna demokrasia ya majukwaani ndio.
Lakini yule commonnwananchi kuleashinani anaishi kwa tabu balaa!
 
Wewe umechanganyikiwa
 
Sasa Bro unategemea mwanasiasa wa Kenya tajiri mwenye ukwasi awe sawa na Watanzania kweli? Hauoni hata tofauti ya uchumi wa Kenya na Tanzania?

Mwizi anayeiba Oysterbay hawezi kuwa sawa na mwizi wa Tandale maana hata malengo ya waibe kitu gani ni tofauti
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Umenirahisishia lunch time yangu kabisa!
 
halafu pia ujue kenya ni nchi ya kibepari.wakati sisi tunahangaika na ujamaa uchwara wenzetu tayari walikuwa wanahangaika na ujasiriamali hivyo hao wameanza biashara miaka mingi.wakenya ni matajiri kweli kweli si kama tanzania na la msingi wenzetu wako wazi kutaja mali zetu lkn kwetu mawaziri hawataji mali zao hadharani na ukitaka kuzijua unaambiwa utaje sababu na utalipia ili kuona hizo mali.hayo ni mambo ya ajabu sana na bora sasa tukawa na katiba mpya itakayofanya hao mawaziri wafike mbele ya bunge ili wataje mali zao na wananchi tuwahoji walizipataje.
 
Huwezi kuwa tajiri ilhali umechagua njia ipelekayo kwenye umasikini.

Watanzania kwa utamaduni,siasa na sera wamechagua umasikini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…