Watanzania tuombeni Mungu, OPEC huenda wakasitisha uzalishaji wa mafuta mwezi huu

Suzy Elias

JF-Expert Member
Joined
Nov 9, 2021
Posts
1,067
Reaction score
6,200
Opec wana kikao leo kitachojadili ama wasitishe uzalishaji wa mafuta ili kujibu tuhuma za nchi za Magharibi za wao kutokuzalisha mafuta kwa wingi ili wamlinde Urusi apate kuuza mafuta yake.

Vilevile Opec hawafurahishwi na bei ya chini ya mafuta iliyopo sokoni.

Ndugu zangu Watanzania tumwombe Mungu atuepushe na hilo.
 
Tumieni miili yenu kufanya shuguli zenu

Ova
 
Huwa tunajifanya wajuaji sana ingawa tunategemea kila kitu kutoka nje

Wakati dunia imeanza kutengeneza magari ya umeme na gas sisi hatuna hata akili ya kuwaza hayo
Nchi nyingi zinabadilisha mfumo wa magari
Sisi tunalalamika tu na kusema eti tumerogwa na nani

Hakuna ubunifu halafu tunajifanya kwenda na wakati
Good luck guys
 
Hahahahaha kwenda na wakati ni kupitia kuiga wanachofanya wenzetu ila nashangaa kwenye teknolojia tuko nyuma sana. Tunaiga fasheni za viatu na jinzi za kuchanika chanika ila mambo ya msingi hakuna 😂😂😂
 
Opec wasitutese sisi walaji tunaangamia hivihivi huku tunajiona tuko katika kipindi kigumu sana.
 
Aisee kwa Comments zako tu, una IQ ya kiwango sana.
 
Bei chini ya mafuta? Huku nani anapandisha bei?
 
Bora tu wasitishe uzalishaji turudi kwenye stone age
 
Hio gari ya kutumia umeme haiwezi safiri toma Dar kwenda nayo Mbeya au Mwanza...charge yake imeenda mbali sana ni 200KM inabidi uchaji tena
 
Endelea kuota....
 
Mkuu mbona DIT inabadilisha mfumo kila uchao?
 
sasa mbn hamna sababu ya msingi ya kusitisha uzalishaji hapo? kwanza wakisitisha wataishi vipi maana yakishuka bei tu huwa chumi zao zinatikisika sa wakisitisha kabisa itakuwaje? sema tu wantk kupunguza uzalishaji kwa mapipa 100000 kwa siku ili kuboost bei, yaan unakuta nchi zaidi ya asiliia 50 ya bajeti yake inategemea mauzo ya mafuta hio jeuri ya kusitisha kabisa uzalishaji anaipata wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…