Watanzania tusiogope bali tuwekeze. Kuna Fursa za biashara zenye faida katika sekta ya mafuta na gesi Katika Taifa letu

Jambo zuri but kwa wauzaji rejareja wa mitungi umesema kuanzia mitungi 25 kwa makisio natakiwa niwe na angalau kiasi gani cha pesa.?
 
Jambo zuri but kwa wauzaji rejareja wa mitungi umesema kuanzia mitungi 25 kwa makisio natakiwa niwe na angalau kiasi gani cha pesa.?
Chukua bei ya mtungi mmoja wenye gesi zidisha na 25 unapata mtaji unaohitajika hapo.
 
Petroli na diesel ni biashara pekee ambazo ni surebet..
 
Unaweza kuwekeza kuanzia kiwango cha shilling ngapi za kitanzania ?
 
Mtaji utakaohitajika kuwa na kituo kidogo cha kuuza mafuta ni wastani wa kiasi gani?
Kwa kijijini ujenzi ni arround 60M, kwa tanki za lita 10000. Chukua lita 10000 zidisha na bei ya jumla ya lita moja. Bei unayoipata jumlisha na ile 60M. Hicho ndicho kiasi cha kuanzia cha mtaji.
 
Unaweza kuwekeza kuanzia kiwango cha shilling ngapi za kitanzania ?
Kwenye gesi ya kupikia ukianza na mitungi 30, chukua bei ya mtungi mmoja uliojaa gesi zidisha na idadi ya mitungi jumlisha na kodi ya fremu.

Kwenye upande wa mafuta kama ni upande wa kijijini unahitaji angalau 60M za ujenzi kwa tanki mbili zenye jumla ya lita 10000. Pia unahitaji mtaji wa mafuta wa lita 10000. Ambao ni lita 10000 zidisha na bei ya jumla ya lita moja. Ukijumlisha 60M na kiasi cha pesa cha kununulia mafuta ndio jumla ya kiasi cha pesa unachohitaji kuanzisha biashara hiyo.
 
Big up mdau kwa mawazo mazuri!
Nimependa idea namba 2. Umesema wizara imeweka mazingira mazuri ya kupata mkopo!
1. Hebu weka wazi vizuri namna ya kupata mikopo hii.
2. Naomba kujua gharama ya pampu moja.

Ahsante.
 
Ndo maana nimesema unahitaji hela ili upate hela.kwa mfano nimeuliza kozi ya kubadilisha mfumo wa mafuta kwenda gesi nimeambiwa kozi Ada laki 8.usawa huu ulivyo mgumu.
Polee sana, utanitafuta PM tuzungumze vizuri kuhusu hili
 
Big up mdau kwa mawazo mazuri!
Nimependa idea namba 2. Umesema wizara imeweka mazingira mazuri ya kupata mkopo!
1. Hebu weka wazi vizuri namna ya kupata mikopo hii.
2. Naomba kujua gharama ya pampu moja.

Ahsante.
Soma hapa:
 
Unajua vizuri kabisa athari zake,sema basi tu majungu

Hata kama huumii wewe atleast act kama unafeel their pain basi...just for the sake of it!
 
Kwa majibu hapa !! tokana na matusi hayo !!! hakika kweli wewe ni Meneja ulioiva unastahili zaidi ya umeneja, Hongera kwa Busara yako

Bila hiyana muhudumie vema huyo mteja mtarajiwa wako ......
 
Kwa majibu hapa !! tokana na matusi hayo !!! hakika kweli wewe ni Meneja ulioiva unastahili zaidi ya umeneja, Hongera kwa Busara yako

Bila hiyana muhudumie vema huyo mteja mtarajiwa wako ......
Ahsante sana boss, kwakweli hili jukwaa linatufunza sana. Karibu sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…