Watanzania tusipoikataa CCM kwa nguvu zote tutaendelea kuchezewa na kutwezwa

Watanzania tusipoikataa CCM kwa nguvu zote tutaendelea kuchezewa na kutwezwa

fazili

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2011
Posts
17,994
Reaction score
24,902
Watanzania tumefika mahali pa kuonekana hatuna akili nzuri na majirani zetu. Juzi nimekutana na mtu kutoka taifa jirani anashangaa sana kwa jinsi siasa za Tanzania zinavyoendeshwa kibabe huku Watanzania wakiwa hawana la kufanya mbele ya kikundi kidogo cha wanasiasa.

Kwa kweli tuliongea mengi ila la msingi ni kwamba inaonekana katika ukanda wa Afrika Mashariki Watanzania tumekuwa watu wa kuburuzwa zaidi na wanasiasa japo tupo wengi kuliko mataifa mengine.

CCM ndio tatizo. Hiki ni kikundi kinachojinadi kama chama cha siosa ila kilishabadilishwa na kuwa genge la kupata maslahi binafsi na hao wanaojiita wanasiasa. Tuwakatae watu hawa sasa kwa nguvu zetu zote la sivyo utu wetu utatwezwa sana.
 
Back
Top Bottom