Watanzania! Tutapanda mti gani leo, ambao watoto wetu watakula matunda yake kesho?

Watanzania! Tutapanda mti gani leo, ambao watoto wetu watakula matunda yake kesho?

Jicho la Tai

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2012
Posts
1,458
Reaction score
617
Maono ya Waraka wa masaa 120 ya mwezi September 2026 kutoka kitabu cha wenye mamlaka (Waamuzi).
  1. Tazama, siku zitakuja ambapo watu wa nchi watakusanyika katika majira ya mashaka, na nyoyo zao zitajawa na maswali kwa sababu hawatajua yaliyo mbele yao.
  2. Nao watasema, “Ni nani atakayetutangulia? Ni nani atakayeshika nchi hii kwa haki na kuwalinda walio dhaifu?”
  3. Ndipo watu wataanza kutafuta wa kuwatawala, na watapita katikati ya mashamba na mabonde wakitafuta miti yenye matunda.
  4. Watauendea mzeituni na kusema, “Njoo utawale juu yetu.” Lakini mzeituni atajibu, “Je, nitaacha mafuta yangu ambayo huleta manufaa kwa wengi ili niende kutawala?”
  5. Watauendea mtini, nao watasema, “Njoo utawale juu yetu.” Lakini mtini atajibu, “Je, nitaacha utamu wa matunda yangu ili nitafute mamlaka?”
  6. Watauendea mzabibu, nao utasema, “Je, nitaacha kazi yangu ili niende nikatawale juu ya miti?”
  7. Ndipo watu watamwona mti wa miba, nao watasema, “Njoo wewe uwe mtawala wetu.”
  8. Na mti wa miba utasema, “Ikiwa kweli mnanichagua, basi mjifiche chini ya kivuli changu; lakini msiponifuata, moto utatoka kwangu na kuiteketeza misitu.”
  9. Nao watu watamwinua juu yao, wakisema, “Tumempata tutakayemtegemea.”
  10. Lakini baada ya siku nyingi, wale waliomwinua wataanza kuingiwa na mashaka, na waliokuwa pamoja wataanza kutengana mioyoni mwao.
  11. Mmoja atasema, “Je, huyu ndiye tuliyemchagua?” Na mwingine atasema, “Tulimpa mamlaka, lakini sasa tunamwogopa.” Wengine watasema, “Tumuondoe,” na wengine watasema, “Simameni pamoja naye.”
  12. Ndipo maneno yataongezeka katika nchi, na mioyo ya watu itagawanyika. Ndugu atamtazama ndugu kwa mashaka, na jirani atamtazama jirani kwa hofu.
  13. Hofu itatembea katika njia za miji, na watu watafunga milango yao mapema. Akina mama watawakumbatia watoto wao, na wazee watajiuliza, “Je, nchi yetu itaelekea wapi?”
  14. Wale wasiohusika katika migogoro watabeba maumivu ya mabishano ya wenye nguvu, na wengi watatamani kuona siku za amani zikirudi.
  15. Ndipo sauti itasikika katikati ya nchi, ikisema, “Tazameni matunda ya kile mtakachopanda; maana apandacho mwanadamu, ndicho atakachovuna.”
  16. Kwa maana hila itazaa hila, na chuki itazaa chuki, na kisasi kitazaa kisasi; lakini haki itazaa amani, na rehema itazaa upatanisho.
  17. Lakini katika siku hizo, watu wachache watasimama na kusema, “Hatutaki watoto wetu warithi hofu; tutatafuta haki, kweli na amani.”
  18. Nao watafundisha kwamba mamlaka si mali ya mtu milele, bali ni dhamana inayopaswa kutumiwa kwa uadilifu.
  19. Na watu watajikuta mbele ya njia mbili: njia ya hofu na njia ya tumaini; njia ya kisasi na njia ya upatanisho; njia ya mti wa miba na njia ya miti yenye matunda.
  20. Ndipo kila mmoja ataulizwa moyoni mwake, “Ni mbegu gani nitakayopanda leo?”
  21. Kwa maana siku zitakuja ambapo watoto watauliza, “Waliotutangulia walituachia nini?”
  22. Na jibu litakuwa wazi: ikiwa walipanda chuki, kizazi kijacho kitavuna chuki; ikiwa walipanda hofu, kitavuna hofu; lakini ikiwa walipanda haki, rehema na upendo, watoto wao watakula matunda ya amani.
  23. Basi swali litabaki juu ya kila kizazi:
“Mti msiopenda matunda yake ukianguka, tutapanda mti gani leo, ambao watoto wetu watakula matunda yake kesho?”
 
Very constructive opinion, since corrupt and selfishness leaders are leading the Nation, don't expect good things to happen

We have leaders who don't think of better tomorrow our kids except theirs

The foundation built from 1985 to date, has brought all these

Let's pray, perhaps things will change before 2030
 
Back
Top Bottom