Msukuma Original
JF-Expert Member
- Oct 2, 2018
- 928
- 3,330
Watanzania muda umefika wa kuweka pembeni tofauti zetu za kisiasa na badala yake tuungane kupinga uonevu na dhuluma.
Rais anasema watanzania wameridhika na tozo. Hakuna mtanzania aliyeridhika na tozo, tuungane tukatae kwa kauli moja hii dhuluma. Kama vyanzo vingine vya mapato hawavioni wasitubebeshe huu mzigo. Maisha yetu yanazidi kuwa magumu kwa maslahi ya watu wachache.
Ajira hakuna, wao wenyewe wanasema uchumi umeporomoka lakini badala ya kutafuta vyanzo vya mapato visivyodidimiza zaidi uchumi wa watanzania ndio kwanza tunabebeshwa mzigo tusioweza kuubeba. Watanzania tafadhalini sana tuweke kando itikadi zetu za kisiasa tukatae hizi dhuluma.
Gesi imepanda, Vodacom wamepandisha vifurushi, tigo wanapandisha vifurushi kuanzia tarehe 16 August, huko si kutaka tuikimbie nchi yetu wenyewe?