Wanabodi,
Kati ya maeneo magumu sana kwenye tasnia ya habari ambayo kwa sisi Tanzania tumelikosa, tunaendelea kulikosa, na kama hawatajitokeza watu wenye uwezo wa kulifanya, tutaendelea kulikosa, ni eneo la "news analysis" uchambuzi wa habari.
Kazi kuu za traditional media ni kuhabarisha, kuelimisha na kuburudisha, sasa katika hizo tatu, media ya Tanzania inafanya vizuri katika eneo la uhabarishaji, na kutoa burudani, lakini katika uelimishaji, bado tuna matatizo, na katika eneo la uchambuzi wa habari, news analysis ndio kabisa, media zetu nyingi hazina uwezo huo, kwasababu hazina watu wenye uwezo huo, matokeo yake, mtu akisema kitu, media zinachukua na kukirusha tuu hivyo hivyo kama kasuku, bila kukichakata na kukifanyia analysis.
Juzi kati hapa rais wetu Mhe. Mama kazuzungumzia need ya Watanzania kumchagua rais mwanamke mwaka 2025 kwa kusema tutamsimamisha Mwanamke, media zimelidaka kama lilivyo kikasuku kasuku na kuanza kulivurumisha, hivyo kuleta mjadala mkubwa kwenye media na mitandao ya jamii, mara kaanza kampeni mapema, mara kajiteua, mara ni ubaguzi wa kuwabagua wanaume, mara hivi mara vile, hivyo bandiko hili ni kuwasaidia kidogo, kuwafanyia a simple analysis ya alichokisema rais Samia.
Kwanza ni ombi kwenu Watanzania wenzangu, kwanza tuunge mkono msimamo wa rais wetu Samia kuwa uchaguzi mkuu wa rais na wabunge wa 2025, tuufanye, sio tuu ni zamu ya kuchagua mgombea mwanamke, bali tuifanye ndio zamu ya ukombozi rasmi wa mwanamke katika siasa, sio tuu tuchague rais mwanamke, bali tuchague wabunge na wadiwani wanawake kwa wingi na kuifikia ile 50/50 ya azimio la Beijing na hata kupita, ila kwenye urais, sio lazima ndio awe Mama Samia, anaweza kuwa yeye au mwanamke mwingine yoyote aliyepangiwa kwasababu mpangaji sio yeye, wala sio sisi, mpangaji na YEYE. Hivyo ikitokea, rais wa Tanzania kwa mwaka 2025 aliyepangiwa na YEYE, ni yeye Mama Samia, then who are we kusema no, kama ni yeye aliyepangiwa, na YEYE, then ni yeye!.
Hivyo mimi naunga mkono hoja ya rais mwanamke ile 2025, kwasabubu kiukweli kabisa, wanawake wana uwezo sana wa uongozi na wengine kuliko hata wanaume, ila siku zote, tumekuwa tukiwakandamiza kutokana na kutawaliwa na mfumo dume kwa miaka nenda miaka rudi, na mpaka Mungu alipoingilia kati. Kama Mungu asingeingilia kati na JPM akaendelea hadi 2025, CCM isingemsimamisha mgombea mwanamke, lakini baada ya Mungu kuingilia kati na Tanzania kwa mara ya kwanza tukapata rais mwanamke, na Mama Samia ameisha onyesha na kuthibitisha pasipo shaka kuwa wanawake wanaweza, then why not 2025 asiwe mwanamke sasa sio tena kwa kudra za Mwenyeenzi Mungu bali kwa chaguo la Mungu kwa Tanzania na kupata endorsement ya Watanzania kwenye sanduku la kura, kumchagua rais mwanamke na wabunge na madiwani wanawake wa kutosha. Na hili likifanyika na likakamilika kikamilifu, uchaguzi wa 2025 tukapata 50/50 ya wabunge na madiwani wanawake wa kutosha. Kazi ya kwanza ya Bunge jipya ni kufuta viti maalum, vitakuwa havihitajiki tena, vikiendelea kubaki ni wastage of time, money and resources.
Marais wa Nchi Hupangwa na Mungu, Hata JPM alikuwa ni Chaguo la Mungu kwa Tanzanzia, Hivyo Hata Samia ni Mpango wa Mungu kwa Tanzania hadi 2025. Kama Samia ni mpaka wa Mungu kwa Tanzania 2025 -2030, then Mungu atasema na sisi, kwasababu hata JPM. hakuna aliyejua Mungu alipanga nini, lakini kwa utaratibu wa CCM, urais huu wa Mama Samia ulioletwa kwa kudra za Mwenyezi Mungu, hii ni awamu yake ya kwanza, hivyo kila mtu anajua uchaguzi wa 2025 ndio awamu yake ya pili ya Mama Samia but only if ndivyo Mungu alivyopanga.
Kwa vile hili ya yeye kugombea 2025, rais Samia mwenyewe aliisha liweka vizuri kabisa ile siku anahojiwa na Salim Kikeke wa BBC, baada ya kuhojiwa kama atagombea urais 2025, rais Samia alijibu vizuri kabisa kuwa "kwa sasa tufanye kwanza kazi, ya 2025 tumwachie Mungu maana no one is shure kufika 2025", hivyo hata rais Samia aliposema 2025 tutamchagua mwanamke, hajamaanisha lazima ni yeye, ni busara kwa rais wetu Samia, hili la ugombea wa 2025, akaendelea na msimamo wake ule ule wa kwenye BBC kuwa ya 2025 tumuachie Mungu. Kwa sasa, rais aendelee ku deal na haya ya Kaizari, kwa kuchapa kazi na kazi iendelee na yale ya Kimungu tumuachie Mungu mwenyewe.
Swali linabaki, Jee Samia ndio mpango wa Mungu kwa Tanzania, 2025 ....
Nenda ukanisome in between the lines, nilisema nini kumhusu mtu anayeitwa Samia Suluhu Hassan, katika mabandiko haya.
Wanabodi, Leo ni Siku ya Wanawake Duniani, katika safari ya kuelekea usawa wa kijinsia, kuna wanawake wengi wenye sifa na uwezo, lakini wamenyimwa fursa za kushika nafasi za juu kisiasa kutokana na nyingi ya nafasi hizo, kuhodhiwa na wanaume, katika kitu kinachoitwa "mfumo dume!" Swali ni je...
Wanabodi, Leo asubuhi nimeangalia kipindi cha mahojiano ya Makamo wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumzia Siku ya Wanawake Duniani kwenye TBC akihojiwa na Shabani Kissu. Kwa Waliosikiliza kipindi hiki, kiukweli huyu ni mwanamke wa kupigiwa mfano, mtanisamehe sina maneno ya Kiswahili ya...
Wanabodi, Niko kwenye voluntariy lockdown, hivyo leo nimepata fursa ya kuangalia TV ya Zanzibar, ZBC, Mwandishi wa habari wa CCM Zanzibar, Daudi Ismail anamhoji Makamo wa Rais wa JMT, Mhe. Samia Suluhu Hassan anauzungumzia Muungano, kiukweli huyu Mama Samia anauzumguza vizuri muungano huku...
Ukiisha soma, kama una uwezo to read in between the lines, jibu utakuwa umelipata.
Sasa kama mpangaji ni YEYE, na ndie amepanga 2025 ni yeye, then who are we to say no?.
2025 Twende na Mwanamke!.
Paskali