Watanzania, tuunge mkono 2025 ni zamu ya Mwanamke, ila sio lazima awe yeye bali yule aliyepangiwa na 'YEYE', kama ni yeye aliyepangiwa, then ni yeye!

Hujui unachoandika,wala hujui ulikotoka wala uendako.Nakuonea huruma sana tena pole.
 
Kwa heshima na taadhima ndg yangu paschal Mayalla hebu tujaribu kuwa fair kidogo mbona kwa upande mbadala wanaambiwa siasa ingoje wajenge uchumi lakini kwao wanaendeleza siasa ukizingatia Sasa ni 2021 mama ndio kwanza ana miezi 6 na bado kuna miaka karibu 4 mbele, kwanini Kuna haraka sana kutuaminisha hiyo agenda ukizingatia binadamu tunapanga ila mungu anahamua,au ndio mambo ya Demokrasia ya Uchina?
Mimi nadhani kiongozi anapimwa on merits na competency hauoni kigezo Cha jinsia kiko biased kwa kuzingatia haki sawa maana nanusa kurudi kwa zama za aongezewe miaka ya kuongoza kama kwa jiwe. Tanzania tunahitaji mifumo na taasisi zilizo bora na zinazojitegemea bila kuangalia kiongozi ni wa namna gani.
 
Nyongeza mshahara iwe haki na sio hisani ya mtu mmoja. Una hakika gani akishachaguliwa 2025 hamtakaa tena 6 years kupata nyongeza.

AMKA ww
Kumbe nyie mlishaongezwa,mbona wazee wastaafu hawajaona chochote au kwa vile hawana nguvu za kupiga kelele na wala hawana mtetezi wao hawastahili.Swala la kupandishwa mada
raja na mishahara ni haki ya wafanyakazi muda ukifika na sio ombi.
 
Kwani amekosea? Ni kweli kuwa tunaangalia sifa stahiki, kupima sera zao ikiwa zina tija na zinatekelezeka n.k, usimtishe kwani hajatukana. Ametumia haki yake kikatiba.

Ni sawa unachosema,, lakini atumie lugha nzuri mzee.
Ona mzee👇🏽
MAANA HAIWEZEKANI KBS RAISI WA NCHI AONGEE UTUMBO UTUMBO TU KAMA ULE....
 
Mawazo ya watanzania kufikiria akili zao na wanasiasa na watawala huwa ni miaka mitano mitano yaani ni madaraka tu hawanaga cha maana

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
 
Mzee Umetafuta TEUZI enzi ya MAGUFULI IMESHINDIKANA UMEONA UJARIBU KWA MAMA
JINSIA SIO SIFA YA URAISI MWISHO ITAKUWA ZAMU YA KABILA FULANI

Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app
 
 
Mimi namuombea Mpango naye apate bahati kama alivyopata Samia😂😂😂
 
Ile miezi mitatu ya kwanza ilikuwa mizuri sana.Matumaini yalikuwa mapya ya mwanzo mpya
 
Nakubaliana na wewe kuhusu hali ya 'news analysis' hapa nchini.

Ila unaposema 'YEYE' ndo anapanga napata mashaka juu ya malengo yako!

Wachambuzi waliobobea kwenye 'news analysis' wa DW, CNN, BBC, FRANCE 24, Aljazeera na vyombo vingine vikivyotukuka kwenye tasnia hii hawajawahi kusema 'YEYE' anahusika na chochote kwenye chaguzi za dola ya nchi yoyote ile hapa duniani.

Wao huongelea habari za nguvu ya ushawishi ya mgombea na chama chake, hali ya siasa katika nchi husika na matumizi ya 'PR' kidigitali katika chaguzi za hivi karibuni kuwa ndio vitu vinavyoamua matokeo ya uchaguzi.

Na wakizungumzia nchi kama za kwetu zenye tume ya uchaguzi ambayo sio huru, wao husema ni nguvu ya mgombea ama ya 'magod father wake kama sio mmoja' ndani ya chama ndio humpa tiketi.

Utaalamu wako wa 'news analysis' umeupata wapi mkuu? Pascal Mayalla
 
Anadai ya 2025 tumwachie Mungu, huku waziri mkuu anadai 2025 ataendelea Rais mwanamke. Katumwa na nani!? Kwa nini anawatisha makada wenzake wenye nia ya kugombea 2025!? Anajuaje huyo bibi atafika hiyo 2025!?
 
Twende na anayeweza bila kujali gender. Tutakaye kwenda naye awe na dhamira ya kweli kuinua hali ya maisha ya mtanzania, kudumisha amani na umoja, kujenga uchumi ulio imara usio tegemezi n.k. Ikiwa atakuwa ni mwanamke ni vizuri genderwise. Lakini hiyo isitubane kwamba ni lazima
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…