Watanzania tuwe makini na vyombo vya habari vya Kibeberu. CNN wazusha kukamatwa kwa Freeman Mbowe ni amri ya Rais Samia!

Mabeberu kuna kitu wana wanatakakuficha kwenye mauaji ya viongo wa serikali.
 
Kinacholeta matumaini ni:
Atakamatwa mtu,
mtu huyo atashikiliwa kwa muda (Haijalishi muda gani) kisha ghafla mbeleni anatokea mtu mwingine mwenye mamlaka,
ambae yeye kwa namna moja ama nyingine anahusika kabisa katika mchakato wa kumshikilia mtu huyo,
anatokea na kiusema hatuna nia ya kuendelea na kesi,
Na picha linaishia hapo,
Kisha maisha yanaendelea, Wapi kama Afrika ya Tanzania? Makofi tafadahali.
 
Duh Kaka Paschal kwa akili ya kawaida ya mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa chuo za uandishi wa habari kweli Polisi yetu hii inaweza kupata wapi nguvu za kumkamata Mbowe kwa vigisuvigisu hizi za kubumba bila mkono wa mtu? kweli wewe ni wa kuandika huu upupu?
 
You are not trusted inside circles of power neither outside.
 
Well presented Pascal Mayalla
 
Bwashee waliita press na kisema Mbowe ni gaidi,, msemaji wa jeshi la polisi.
Vyombo gani tena vya habari? Hawa Ccm kazi yao ni kuzima matukio kwa kuanzisha tukio. Hivi Mbowe huo ugaidi kaufanyia wapi? Hivi Mbowe na Makonda ni nani gaidi? Maana Makonda aliteka kituo cha Clouds na hamkumuita gaidi
 

Sasa mkuu unataka Tuachane na hawa CNN halafu unaturudisha kumsikiliza Ayoub Rioba TBC !!!!

Lengo lao nini hawa Mataifa ya Kibeberu?

Kama hatuwakubali mbona tunawatembezea Bakuli kila kukicha na kuwaambia tuna utawala wa kidemokrasia, unaofuata katiba na hakuna uonevu nchini kwetu (utawala wa sheri). Kwa nini tusiwe kama Korea Kas ?


 
Mtoa post Una toambwa nyuma
 
Shida yako unavitaka vyombo hivyo vifuate mapenzi yako katika uandishi wao. Wao wamesema walichosema na kama serikali inaona imeonewa ina haki ya kuwashtaki au kudai nafasi ya kusahihisha hizo habari. Huko waliko kuna mabalozi ambao tungetegemea kuwa mpaka sana wangeisha toa masahihisho. Kwa bahati mbaya, inadaiwa aliyewakamata alisema kuwa ameelekezwa kufanya hivyo na mamlaka ya juu. Kwa vile mpaka sasa hajapingwa basi watu wana haki ya kuspeculate huyo mamlaka ya juu ni nani? Nadhani kama angekuwa hajapokea maagizo angeisha chukuliwa hatua kwa kuwasingizia viongozi wake na angeamriwa awaachie alio wakamata. Badala yake, tuna ona baadhi yao wakizungushwa nchini chini ya ulinzi wa polisi. Mabeberu si watu wa kulaumiwa. Makosa ni yetu sisi wenyewe.

Amandla...
 
Bwana Mayalla.... kama Rais ndie Amiri Jeshi Mkuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama, effectictely anahusika na matendo yote ya vyombo vyake. Na kama hapendezwi alipaswa kuchukua hatua, kuacha mambo yaendelee hivi maana yake amekubali kuwa ni sawa.
 
Hivi kwa hizi hoja zako nyingi za kinafiki na uchumia tumbo , una haki wewe kujijumuisha kwenye kundi la wazalendo? Unafiki siyo sehemu ya uzalendo.

Huyu prof anavyofanya analysis na argument zake kuhusiana na Tanzania na utawala wake, inaonekana ni mtu mwenye uelewa mkubwa na sahihi sana kuhusiana na yanayoendelea Tanzania.

Uelewa wake na akili yake, ukilinganisha na wa Mayala wetu, ni sawa na kufananisha kibaba na gunia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…