Watanzania twendeni Congo tukawekeze Sekta ya Usafiri wa majini na mafuta

Watanzania twendeni Congo tukawekeze Sekta ya Usafiri wa majini na mafuta

Ndio tunafanana wao wana kichwa kimoja na miguu miwili kama sisi au wao wana vichwa viwili na miguu kumi?
Sawa Mkuu, kawekezeni nje ya nchi na nje ya bara kabisa.

Maendeleo hayana chama!
 
Hujui kitu na unaishi Tanzania?.Hivi wewe unaishi ubelgiji au? Hujui Tanzania kuwa shirika la reli linamiliki meli pia zote zilizoko ziwa Tanganyika,Ziwa Nyasa na Ziwa VICTORIA? Hujui kuwa wameshaunda meli mpya hapahapa nchini kwa ajili ya huko maziwani? Au wewe unavyojua na ujuaji wako TRC haina meli?

Hakuna kitu kibaya duniani kama kusoma kwa kukariri kama wewe ulivyokariri nyie ndio mnatufanya watanzania wote tuliosoma tuonekane hopeless
Mkuu TRC ilikuwa na Meli zake kipindi cha nyuma kabla ya ubinafsishaji kwa ile kampuni ya India (RITES) na kuwa TRL.

Hizo Meli hazipo mikononi mwa TRC zipo chini ya Marine Service Company Limited (MSCL) na zinapatikana katika ziwa Victoria na Tanganyika.

Ebu nitajie meli iliyotengenezwa na TRC hii unayoijua mpya ya 2017???

Sent from my TECNO LC6a using JamiiForums mobile app
 
Mkuu, Umeandika mengi lakini hayana maana. Jifunze kwanza MARINE SERVICES COMPANY LIMITED (MSCL) ni nini.

Baada ya kuvunjikwa kwa East African Railways and Harbours Corporation mwaka 1977, TRC ilisimamia na kutoa huduma za reli na meli nchini, 1997 TRC iligawanywa na kuundwa MSCL.

MSCL ni shirika linalojitemea kama ilivyo kwa posta na TTCL (simu) baada ya kugawanywa 1993/94.
Upo sahihi kabisa hivi ndivyo ilivyo jamaa kaja spidi kumbe hana uelewa na anachokiandika Bongo bana.

Sent from my TECNO LC6a using JamiiForums mobile app
 
Sawa Mkuu, kawekezeni nje ya nchi na nje ya bara kabisa.

Maendeleo hayana chama!
Wakati watu wanalamika ajira angalia Mama RADIATOR mwanamke toka Kenya fundi radioator KONGO

 
Kila msaka fursa angalia hii clip uone mwenyewe fursa zilipo za biashara ya usafiri wa majini na mafuta Congo
Hizo baadhi tu lakini ukitizama hii Clip waweza gundua nyingi zaidi.


Naipenda Afrika yangu


Ulienda huko ni muhimu sana uende na walimu wa kuwabadili wateja mind set
 
Shirika la reli pia lianze kufikiria kuwekeza nje ni fursa kubwa Congo liunde meli lipeleke kule
Naomba namba ya huyo Sadali, hio stiki uliochoma baada ya lunch ni ya level za kimataifa.
 
I wish mngeondoka wafuasi na wanachama wote wa CCM! Mngehama nchini mwetu moja kwa moja na kwenda kuwekeza huko DRC, na kuchukua kabisa uraia wa huko.
Nyie CHadema mumepewa miaka kibao ruzuku mabilioni mumeshindwa kujenga hata ofisi ya makao makuu chumba kimoja mkiachiwa nchi ndio mtaweza kuijenga?
 
Kwenye TRA sijaelewa
Tumechelewa kampuni zote zinazojenga mabarabara Tanzania na Africa nzima ni kampuni za serikali ya CHINA .China inamiliki hisa asilimia 100.Ikitokea tenda popote duniani wana bid.Ndio wamejenga hadi Reli ya SGR ya kenya

Kenya wenyewe kampuni yao ya umeme kama ilivyo yetu ya TANESCO huwa inabid Tenda za miradi ya umeme nje ya nchi na imeshashinda Tenda za mabilioni ya dola ikiwemo ujenzi wa miradi ya umeme Djibouti

Mashirika yetu ya umma yanatakiwa kuanza kuvuka mipaka ya nchi kutafuta tenda mashirika kama TTCL,Bandari ,Tanesco nk Hata TRA yaweza tafuta tenda za kuendesha mifumo ya kodi mataifa mengine
 
Taasisi hizi za umma zinazojenga majengo yenye makorongo kama bonde la ufa kisha wanaita expansion joints tu ?
 
Mkuu TRC ilikuwa na Meli zake kipindi cha nyuma kabla ya ubinafsishaji kwa ile kampuni ya India (RITES) na kuwa TRL.

Hizo Meli hazipo mikononi mwa TRC zipo chini ya Marine Service Company Limited (MSCL) na zinapatikana katika ziwa Victoria na Tanganyika.

Ebu nitajie meli iliyotengenezwa na TRC hii unayoijua mpya ya 2017???

Sent from my TECNO LC6a using JamiiForums mobile app
Uko sahihi mkuu.
 
Jamii forums kuna maajabu ukiweka kitu cha maana hupati wachangiaji ila ukiweka cha kisiasa hata cha kubuni tu mfano Lisu apigwa rungu na kichaa ubelgiji michango itafurika hiyo hadi basi.Hii mada limekosa wachangiaji wengi nimejua kwa nini jamii forums members wengi humu maskini wa kutupwa!!!
 
Back
Top Bottom