Nkerebhuke
JF-Expert Member
- Nov 1, 2021
- 796
- 2,026
Ukifuatilia kwa makini mijadala ya vijana wengi kwenye majukwaa makubwa hasa siasa utagundua kuna kitu hakipo sawa ( something amiss ). Katika hali isiyo ya kawaida maoni mengi yamejikita sana kuzungumzia watu badala ya masuala muhimu yanayopaswa kuwekwa wazi. Tatizo hili limezaa machawa, opportunist na wanafiki wanaojifanya wazalendo huku wakitimiza agenda zao binafsi.
Aina ya siasa ya nchi yetu kwa sasa inaenda sambamba juu ya uelewa mdogo wa masuala muhimu juu ya taaluma ya siasa. Vijana wanapenda majungu kuliko kufanya tafiti kujua kwanini hili linatokea. Tatizo lipo kwenye mitaala yetu ya shule au ni uumbaji?
Inaumiza sana mpaka kwenye chombo cha wananchi kama bunge unakuta mijadala ya kishabiki yaani kuna watu wanataka Rais asifiwe tu bila kukosolewa kwa jambo lolote. Tatizo ni nini jamani?