Watanzania wakati umefika wa kuamka na kumpambania Lissu na katiba mpya

Watanzania wakati umefika wa kuamka na kumpambania Lissu na katiba mpya

Mdaiwa

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2025
Posts
1,147
Reaction score
2,919
Ni dhahiri hawa wauaji wamepanga kumfunga Tundu Lissu na hawana mpango wa katiba mpya ambayo itawaondoa madarakani.

Sasa kwa umoja wetu tuamke na tuingie barabarani kuhakikisha haki inapatikana Tanzania.

Tundu Lissu ameonyesha dhamira ya kweli na kutupigania watanzania, tunapaswa tusimuangushe. Nchi inaliwa hii. Na watawala wamejipanga kummaliza yeyote anayewapigania na kuwafumbua macho watanzania. Polepole, wamempoteza, Nchimbi japo alikuwa upande wao ila baada ya kutaja katiba mpya wakamvua umakamu fake wa rais na mpaka sasa hajulikani alipo. Hivyo unaweza kuona hawa mashetani walivyojizatiti kuhakikisha haki haipatikani Tanzania.

Watanzania wenzangu, Tundu Lissu pekee, au Polepole pekee hawezi kuwaogopesha wauaji wakaruhusu haki na katiba mpya ikapatikana. Watanzania kwa wingi wetu ndio nguvu pekee ya kuwalazimisha hawa wauaji kutupatia haki na katiba mpya itakayolinda raslimali za nchi yetu zinazokwapuliwa na haya mashetani mauaji. Haki haitakuja kwa kuombwa, ni lazima tuipiganie. Wakati ndio sasa, hatuna muda wa kupoteza tena. Tuamke wote tuipambanie nchi yetu.

Mungu wa Mbinguni awabariki wote kwenye kuipigania haki na katiba mpya.
 
Back
Top Bottom