Watanzania wako tayari kuchangia harusi, sio gharama za matibabu ya Mtoto - Dtk. Mollel

DogoWaNjombe

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
3,284
Reaction score
7,708
WhatsApp Image 2025-06-12 at 13.23.27_fc4fe19f.jpg
Serikali imetoa wito kwa wananchi kubadilika na kuwekeza katika bima ya afya kama njia ya kujiandaa na changamoto za kiafya, ikiwemo gharama kubwa za matibabu ya magonjwa kama saratani.

Wito huo umetolewa Bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel, alipokuwa akijibu swali la nyongeza kutoka kwa Mhe. Ester Matiko (Viti Maalum), ambaye alitaka kufahamu kama Serikali haioni haja ya kuweka kifurushi cha saratani kwenye bima ya afya ya chini ili kuwezesha wananchi wa kawaida kupata huduma, kutokana na gharama kubwa za matibabu ya ugonjwa huo.
WhatsApp Image 2025-06-12 at 13.23.25_cc22a147.jpg
Akijibu swali hilo, Dkt. Mollel amesema jamii inapaswa kubadilika na kuwekeza kwenye bima ya afya ili kuimarisha afya zao.

"Watu wako tayari kuchangisha Milioni 100 kwa ajili ya harusi, lakini mtoto anapozaliwa hakuna anayechangia hata kwa ajili ya matibabu. Hii inaonyesha kwamba jamii inathamini sherehe kuliko afya,” amefafanua Dkt. Mollel.

Aidha, Dkt. Mollel amebainisha kuwa Serikali imetenga zaidi ya Shilingi Bilioni 200 kwa ajili ya msamaha wa matibabu, ikiwa ni sehemu ya kuhakikisha wananchi, hususan wasio na uwezo, wanapata huduma za afya bila vikwazo vya kifedha.

Naibu Waziri amesisitiza kuwa Serikali itaendelea kuboresha mifumo ya bima ya afya ili kuhakikisha huduma za afya, zikiwemo za magonjwa yasiyoambukiza kama saratani, zinapatikana kwa wote kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa bima ya afya kwa wote unaotarajiwa kuimarika zaidi katika utekelezaji wa sera mpya ya afya.
 
Yaani mbunge anaomba VIP iliajiokoe na foleni 🚮 Huku wananchi tukisota masala sita kwenye foleni
 
Hapo bila kupepesa macho angalao Leo mzee kaongea point. Jamii kwakweli inapaswa kubadilika lakini pia serikali nayo utekelezaji uwe serious sio watu wanachangia mfuko wa bima wao kazi yao inakuwa kuweka makada ambayo wataruhusu serikali kwenda kujikopea fedha na hata kurudisha shida, mfuko ukianza kuyumba wanaanza masharti kwenye mnufaika kupata matibabu. Na kwakweli kuepuka huo mtego ni sawa na haiwezekani
 
Serikali imetoa wito kwa wananchi kubadilika na kuwekeza katika bima ya afya kama njia ya kujiandaa na changamoto za kiafya, ikiwemo gharama kubwa za matibabu ya magonjwa kama saratani.

Wito huo umetolewa Bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel, alipokuwa akijibu swali la nyongeza kutoka kwa Mhe. Ester Matiko (Viti Maalum), ambaye alitaka kufahamu kama Serikali haioni haja ya kuweka kifurushi cha saratani kwenye bima ya afya ya chini ili kuwezesha wananchi wa kawaida kupata huduma, kutokana na gharama kubwa za matibabu ya ugonjwa huo.
Akijibu swali hilo, Dkt. Mollel amesema jamii inapaswa kubadilika na kuwekeza kwenye bima ya afya ili kuimarisha afya zao.

"Watu wako tayari kuchangisha Milioni 100 kwa ajili ya harusi, lakini mtoto anapozaliwa hakuna anayechangia hata kwa ajili ya matibabu. Hii inaonyesha kwamba jamii inathamini sherehe kuliko afya,” amefafanua Dkt. Mollel.

Aidha, Dkt. Mollel amebainisha kuwa Serikali imetenga zaidi ya Shilingi Bilioni 200 kwa ajili ya msamaha wa matibabu, ikiwa ni sehemu ya kuhakikisha wananchi, hususan wasio na uwezo, wanapata huduma za afya bila vikwazo vya kifedha.

Naibu Waziri amesisitiza kuwa Serikali itaendelea kuboresha mifumo ya bima ya afya ili kuhakikisha huduma za afya, zikiwemo za magonjwa yasiyoambukiza kama saratani, zinapatikana kwa wote kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa bima ya afya kwa wote unaotarajiwa kuimarika zaidi katika utekelezaji wa sera mpya ya afya.
Ni kama vile wengine wapo tayari kuuwa ili walinde ugali wao na wa bosi wao.
 
Watafute video ya Mnazi mmojq inayosambaa mitandaoni.

Imagine mtu anaenda hospital iliyopo katikati ya jiji. Tena hospital kubwa usiku A&E imefungwa hakuna daktari wala nurse.

Bado hazards zilizopo, hakuna taasisi inayotakiwa kuwa safi kama hospitali kwenyewe mifuko ya cement ipo kwenye entry way ndani ya hospitali na imejaa vumbi balaa.

Taa usiku zimezimwa wagonjwa wanatembea giza huku wanasukuma vyuma vyao vya drips.

Ni mungu tu anajua huko wards kuna hali gani au hata quality ya huduma.

Sasa huko mikoani au maeneo ambayo hata viongozi kustukizia sijui vituo vya afya zina hali gani mbaya.

Wanatia aibu halafu sio kwamba serikalini hakuna watu wenye uwezo wa kusimamia huduma ya afya; isipokuwa ni mijitu mijinga tu iliyopo CCM kila kwao mzaha.

Kuna mambo Tanzania yanakera sana.
 
Back
Top Bottom