Watanzania waliokwama kwa lockdown Afrika Kusini warejea nchini

Watanzania waliokwama kwa lockdown Afrika Kusini warejea nchini

mkiluvya

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2019
Posts
809
Reaction score
729
1590485430428.png


Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini Meja Jenerali (Mst) Gaudence Milanzi Jumatatu Mei 25, 2020 amesimamia zoezi la repatriation (usafirishaji) wa dharura) ya Watanzania pamoja na raia kadhaa wa nchi hiyo waliokwama kutokana na Lockdown na kusitishwa safari za ndege inayoendelea huko, kutoka Johannesburg kuja Dar es salaam.

Taarifa kutoka ubalozi wa Tanzania nchini humo zinasema kwamba Balozi Milanzi aliratibu na kusimamia zoezi hilo ambapo Watanzania hao walikwama nchini humo kwa miezi miwili kufuatia Lockdown hiyo. Raia kadhaa wa Afrika Kusini nao wakajiunga kwenya msafara huo baada ya kuona ni afadhali warejee Tanzania ambako hakuna Lockdown ili kuendelea kufanya kazi kwenye makampuni na taasisi za nchi hiyo.

Akiwasindikiza abiria hao ambao walionesha nyuso za furaha kwa kupata fursa ya kuondoka nchini humo, Balozi Milanzi aliwapa pole kwa kuwa katika Lockdown ya miezi miwili na kuwatakia safari njema na maisha ya furaha watapowasili Tanzania ambayo ni nchi pekee ambayo imekuwa na msimamo thabiti wa kupambana na gonjwa la COVID 19 lililosababisha nchi zingine kufungia kila mtu ndani.

Hili ni tukio la tatu la repatriation tokea gonjwa hilo liikumbe dunia na kusababisha sintofahamu kila pembe, kufuatia zile safari za India na Falme za Kiarabu ambapo serikali ilituma ndege maalumu kwenda kuchukua wananchi wake waliokwama huko kutokana na Lockdown katika nchi hizo. Zoezi hilo limekuja wakati Tanzania imefungua rasmi anga lake na kuruhusu utalii na safari za ndege za kimataifa viendelee kama kawaida, ambapo tayari mamia ya watalii wameendelea kumimimika nchini, huku wengine wakitarajiwa kuwasili kwa wingi baada ya mashirika ya ndege ya kimataifa kuanzisha safari zao.
 
Watz wote toka Sauz na wageni wengine wajue tu ya kwamba TANZANIA IS NOT THAT MUCH SAFE FROM COVID-19....They must take all possible measures to avoid any viral infection from the killer disease!
Otherwise Karibuni nyumbani😁
 
Uongo mwingine hauna faida mimi mbona bado niko huku? na siji kufa huko hta kwa kutambikia yaani wa-South waende Tanzania kufa njaa, ungejua wanavo idharau hiyo nchi usinge panua domo!
 
Back
Top Bottom