Watanzania waliopata umaarufu wa ghafla mitandaoni na kisha kupotea…

Watanzania waliopata umaarufu wa ghafla mitandaoni na kisha kupotea…

The Sheriff

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2019
Posts
747
Reaction score
2,112
Mitandao ya kijamii imetoa fursa kubwa sana kwa mtu yeyote ‘kwenda mjini’ chap. Hii ni orodha ya baadhi ya watu ambao kusingekuwa na intaneti, wasingepata umaarufu walioupata.

DKT. LOUIS SHIKA
Shika.JPG

Dkt. Louis Shika alijipatia umaarufu baada ya kutangaza dau la kununua nyumba za mfanyabiashara Said Lugumi. Alifahamika zaidi kwa msemo wa “900 itapendeza” baada ya kupiku watu wengine waliokuwa kwenye mnada huo. Shika alifikia hatua ya kuwa balozi wa makampuni kadhaa na stori yake ya kutekwa Urusi ilikuwa ni moja ya mada muhimu katika mahojiano mengi aliyofanya na vyombo vya habari. Kwa sasa Dkt. Shika ni marehemu. Alifariki Agosti, 2020.

PIERE LIQUID
Piere-Liquid-1.jpg

Konki Liquid. Pierre. Mama nakufa. Chii. Ni utambulisho wa jamaa aliyeishika mitandao ya kijamii wakati fulani. Huyu jamaa jina lake halisi ni Peter Gumbo, na amejizolea umaarufu baada ya video iliyomuonesha akisema “mama nakufa” kuzagaa mitandaoni mwishoni mwa mwaka 2018. Katika wakati wake akiwa juu ya kilele cha umaarufu, Liquid amebahatika kuwa balozi wa suehemu za starehe na kutumika kupromote baadhi ya bidhaa.

CHIKUMBALAGA
Chikumbalaga.jpg

Jamaa huyu alikuja kuwa maarufu sana kwenye mitandao ya kijamii. Chikumbalaga, aka Sukariyao, alitokea nyumbani kwao huko Tunduma Mkoani Mbeya hadi kufika Dar es Salaam ambapo umaarufu ulizidi kukua. Umaarufu wake ulitokana na muonekano wake na namna alivyokuwa akijibu maswali kwenye interviews mbalimbali. Katika moja ya mahojiano na Millard Ayo TV, Chikumbalaga aliulizwa ana miaka mingapi akajibu, “Sabini na tano” na alipoulizwa amezaliwa lini alijibu “2005”.

Sukariyao pia alpata umaarufu kwa njia ya wasanii kumtumia kwenye upande wa kuchekesha pale anaposhea video na audio akizisapoti kwa kucheza au kuimba nyimbo za wasanii hao kisha kupost mitandaoni.

Jamaa hayupo sana kwenye spotlight kwa sasa. Je, yupo wapi?

MZEE WA MJEGEJE
Mzee wa Mjegeje.jpg

Unakumbuka msemo wa"kata simu, tupo site"? limekuwa maarufu sana kwenye majukwaa ya mtandaoni nchini Tanzania ambapo watumiaji mara nyingi walilitumia. Katika video iliyosambaa sana, Mzee wa Mjegeje alionekana akiongea kwenye simu ndogo, akisema "Kata simu, kata simu, tupo site."

Tangu wakati huo, maneno hayo ya kuchekesha kutoka kwenye video hiyo yamekuwa yakitumiwa sana katika vichekesho, na baadhi ya wasanii hata wameyajumuisha katika nyimbo zao. Mzee Mjegeje, aliyejulikana pia kama "Raisi wa Bagamoyo," alikuwa mkazi wa Bagamoyo katika mkoa wa Pwani. Umaarufu wake ulivuka mipaka, ukifikia umaarufu wa kimataifa, haswa nchini Kenya mnamo 2022 wakati video yake "Kata simu, tupo site" ilipovuma kwenye mitandao ya kijamii. Sasa hivi Mzee wa Mjegeje ni marehemu.

MAJALIWA MVUVI
Majaliwa.jpg

Majaliwa Jackson ni mvuvi aliyefanikisha kuufungua mlango wa ndege na kufanikisha kuokolewa kwa abiria 24 waliokuwa ndani ya ndege ya Precision Air iliyotumbukia Ziwa Victoria Jumapili ya Novemba 6, 2022 karibu na Uwanja wa Ndege Bukoba, Mkoani Kagera. Baada ya tukio hilo Majaliwa alipokea zawadi mbalimbali kama vile shilingi milioni moja kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera kwa wakati huo, Albert Chalamila.

Baadaye kijana Majaliwa alipokelewa katika Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ikiwa ni utekelezaji wa maelekezo yaliyotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan. Alielezwa kujiunga na Chuo cha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kilichopo Chongo Wilaya ya Handeni Mkoa wa Tanga. Je, kuna mwenye taarifa zaidi kuhusu Majaliwa?

MZEE MPILI
Mzee Mpili.jpg

Shabiki na mwanachama mwandamizi wa Yanga SC Mzee Haji Omary Mpili ni mkazi wa Rufiji Pwani katika kijiji cha Ngomboloni. Mzee Mpili ajipatia umaarufu mkubwa siku za karibuni baada ya kauli yake ya ‘Sisi Tuna Watu, Hatuwezi Kufungwa na Simba’ kutafsiriwa kama kauli iliyowapa nguvu Wana Yanga kuibuka na ushindi katika pambano la ligi kuu bara Julai 3, 2021. Mzee Mpili huonekana kama mzee mtata na mwenye uchu wa mafanikio kwa timu yake (Yanga).

STEVE “KULIALIA”
Steve Kulialia.jpg

Wakati Yanga ilipofungwa na Simba mabao 5-0 wakati fulani Steven alilia sana, akapigwa picha mbalimbali, akahojiwa na redio na televisheni huku akiwa anabubujikwa machozi, akawasimanga waamuzi kuwa ndiyo chanzo cha klabu yake kufungwa. Alipata umaarufu baada ya video zake kuzagaa mitandaoni. Leo hii Steven ni shabiki mkubwa wa Azam.

KUNZE NA DOTTO
Kunze na Dotto.PNG

Hawa bwana waliotrend mtandaoni na video yao moja ambapo mmoja anajichukua video akisema, "Oya, Jafe! Mbona hujatokea, sisi tunamaliza mjomba!”. Inaonekana walikuwa wakimpigia mshikaji wao ambaye hakutokea kwenye gradu, hivyo wakawa wanamuonesha mambo yalivyokuwa yamenoga. Hawa jamaa walikuja Dar kutoka kwao huko na wakajaribu kuingia kwenye uchekeshaji. Sina hakika kama walitoboa.

KARIM MANDONGA
Mandonga K.jpg

Miaka kadhaa iliyopita ungemwambia Karim Mandonga ‘Mtu kazi’ bondia mwenye maneno na mbwembwe nyingi wa Tanzania kwamba, angewahi kupata fursa ya kupigana kwenye ulingo nje ya nchi yake, angekubishia. Sidhani kwamba pia kama alikuwa na ndoto au aliwaza ipo siku angekuwa bondia anayetajwa zaidi Afrika Mashariki kuliko mabondia wengine wote.

Kilichompa umaarufu Bwana Mandonga ni maneno yake mengi na misemo kadha wa kadha ambayo ilionekana kurudisha hype ya masumbwi Bongo na Afrika Mashariki. Alifikia hatua ya kumchapa bingwa wa zamani wa taji la Afica Boxing Union (ABU), Daniel Wanyonyi kwa TKO (Technical Knock Out) huko Nairobi nchini Kenya. Na Wakenya walimshangilia vibaya mno. Mandonga alikuwa anajulikana sana na kila kona alitajwa.

Ukitaja mabondia wakali na wenye rekodi za kufurahisha duniani, Karim Mandonga ‘Mtu Kazi’ hawezi kuwemo. Ukitaja mabondia wakali wa kiwango cha kufikirisha Afrika Mashariki Mandonga hayumo. Na hata ukitaja mabondia wakali watano wa Tanzania hakuwemo. Na umaarufu wake ulikuja kwa kupigwa katika moja ya mapambano yake baada ya kutamba sana kwa maneno.

Alizipa ngumi zake majina kama vile 'ngumi mpya Sugunyo kutoka Ukraine' au ngumi ya Peresu peresu' ama ndoige'. Hivi viliwabamba wengi. Lakini pia, jamaa alikuwa anapigana mapambano mengi sana ndani ya muda mfupi.

Hata hivyo, aliitumia nafasi yake vizuri na ameonekana kwenye matangazo na promotions za bidhaa nyingi. Natumai alitumia kipindi chake kutengeneza mpunga wa kutosha. Sasa hivi hasikiki, na ninaamini anastahili kuwepo kwenye orodha hii. Je, jamaa anafanya nini sasa?

CHOLO
Cholo.jpg


KOMANDO MADAFU WA IKULU
Komando Mdafu.PNG

Mnamo tarehe 12 Machi, 2024 ambapo Rais Samia aliwaalika viongozi pamoja na makundi mbalimbali ya Kijamii kujumuika naye katika viwanja vya Ikulu kwa ajili ya kupata futari ya mwezi mtukufu wa Ramadhan, walionekana vijana wawili wakiwa wanauza madafu. Vijana hao walikuja kuzua gumzo sana; wengine wakihoji kama wale walikuwa wauza madafu halisi au walikuwa wanausalama waliojifanya wauza madafu. Hoja hizo zilisababisha mjadala mzito sana nchini. Walikuwa gumzo!

Siku chache baadaye, wakati wa kilele cha Sherehe za Miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam tarehe 26 Aprili, 2024, Askari mmojawa Kikundi Maalum cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) alionekana akishuka kwenye Helikopta kwa ajili ya kwenda kuelezea namna mbalimbali za kwata na mapigano ya mjini. Askari huyu alifananishwa sana na muuza madafu aliyedhaniwa hapo awali kuwa ni mwanausalama wa Jamhuri. Hii ilisababisha jamaa kupata umaarufu zaidi na kufanyiwa interview nyingi na vyombo vya habari serious na vya udaku.

Kilicholeta gumzo zaidi ni pale alipotumia mameno “Ukija bila gadi (guard) nitagawa wastani kwa idadi” ambayo yalisemekana ni kauli za watu waliopita kwata fulani. Hata hivyo, kwenye mahojiano yake alisema kuwa yupo fresh kwenye michezo ya kujihami, jambo lililosababisha wengi kuamini jamaa ni mwanausalama.

Mpaka muda huu Agosti 30, 2024, umaarufu wa jamaa umeshuka na hakuna anayemzungumzia tena kwa ukubwa wa miezi minne iliyopita. Huenda akapotea kabisa midomoni mwa watu siku zijazo.

Well, nitaendelea kuongeza kwa kadiri nitakavyokumbuka na kupata wasaa wa kuongeza hii orodha.

Next update
Magoma.jpg
 
Back
Top Bottom