The Sheriff
JF-Expert Member
- Oct 10, 2019
- 747
- 2,112
- Thread starter
- #21
Dah!Dk Shika kafanana sana na Milard Ayo
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Dah!Dk Shika kafanana sana na Milard Ayo
Na yule Injiniaa Soma iyooooUmemsahau na Mbunge mstaafu Mh. Bwege na kauli yake "Wee ulisikia wapi"
Well, sina hakika kama alikuja Bongo kwa passport. Na hadi kufika Dar na kuwa maarufu hatukusikia kuwa si Mtanzania. Tulijua tu anatokea Tunduma, ambayo ni sehemu ya Tanzania. Hata hivyo, kwa vyovyote vile, umaarufu wake uliwagusa Watanzania zaidi.lakini chikumbalaga sio Mtanzania
Dah nilisikia sikia kuwa alikatwa mguu huyu mwamba Kwa sababu ya sukariUmemsahau na Mbunge mstaafu Mh. Bwege na kauli yake "Wee ulisikia wapi"
Huwa naona kama ni mataahira tu,sijui wanachekesha kitu ganiHawa kina kunze ile ilitokea ajali tu, si wachekeshaji, umaarufu ule watumie kwa maendeleo ila wasikimae na uchekeshaji.
Yuko songea anapiga debe standChollo boy yule mwamba alipotelea wapi? Bichwa komwe yaan appearance yake tu lazma ucheke.
Ndugu waandishi wa habariChollo boy yule mwamba alipotelea wapi? Bichwa komwe yaan appearance yake tu lazma ucheke.
Af mwamba alikua na glass of water pemben na miwani yake kubwa 🤣🤣Ndugu waandishi wa habari
Steve hajapotea isipokuwa kapata kazi ya kumkeep busy ndio anayefanya matangazo na Azam tv, hasa ya michezoMitandao ya kijamii imetoa fursa kubwa sana kwa mtu yeyote ‘kwenda mjini’ chap. Hii ni orodha ya baadhi ya watu ambao kusingekuwa na intaneti, wasingepata umaarufu walioupata.
DKT. LOUIS SHIKA
View attachment 2965126
Dkt. Louis Shika alijipatia umaarufu baada ya kutangaza dau la kununua nyumba za mfanyabiashara Said Lugumi. Alifahamika zaidi kwa msemo wa “900 itapendeza” baada ya kupiku watu wengine waliokuwa kwenye mnada huo. Shika alifikia hatua ya kuwa balozi wa makampuni kadhaa na stori yake ya kutekwa Urusi ilikuwa ni moja ya mada muhimu katika mahojiano mengi aliyofanya na vyombo vya habari.
Kwa sasa Dkt. Shika ni marehemu. Alifariki Agosti, 2020.
PIERE LIQUID
View attachment 2965127
Konki Liquid. Pierre. Mama nakufa. Chii. Ni utambulisho wa jamaa aliyeishika mitandao ya kijamii wakati fulani. Huyu jamaa jina lake halisi ni Peter Gumbo, na amejizolea umaarufu baada ya video iliyomuonesha akisema “mama nakufa” kuzagaa mitandaoni mwishoni mwa mwaka 2018. Katika wakati wake akiwa juu ya kilele cha umaarufu, Liquid amebahatika kuwa balozi wa suehemu za starehe na kutumika kupromote baadhi ya bidhaa.
CHIKUMBALAGA
View attachment 2965128
Jamaa huyu alikuja kuwa maarufu sana kwenye mitandao ya kijamii. Chikumbalaga, aka Sukariyao, alitokea nyumbani kwao huko Tunduma Mkoani Mbeya hadi kufika Dar es Salaam ambapo umaarufu ulizidi kukua. Umaarufu wake ulitokana na muonekano wake na namna alivyokuwa akijibu maswali kwenye interviews mbalimbali. Katika moja ya mahojiano na Millard Ayo TV, Chikumbalaga aliulizwa ana miaka mingapi akajibu, “Sabini na tano” na alipoulizwa amezaliwa lini alijibu “2005”.
Sukariyao pia alpata umaarufu kwa njia ya wasanii kumtumia kwenye upande wa kuchekesha pale anaposhea video na audio akizisapoti kwa kucheza au kuimba nyimbo za wasanii hao kisha kupost mitandaoni.
Jamaa hayupo sana kwenye spotlight kwa sasa. Je, yupo wapi?
MZEE WA MJEGEJE
View attachment 2965130
Unakumbuka msemo wa"kata simu, tupo site"? limekuwa maarufu sana kwenye majukwaa ya mtandaoni nchini Tanzania ambapo watumiaji mara nyingi walilitumia. Katika video iliyosambaa sana, Mzee wa Mjegeje alionekana akiongea kwenye simu ndogo, akisema "Kata simu, kata simu, tupo site."
Tangu wakati huo, maneno hayo ya kuchekesha kutoka kwenye video hiyo yamekuwa yakitumiwa sana katika vichekesho, na baadhi ya wasanii hata wameyajumuisha katika nyimbo zao. Mzee Mjegeje, aliyejulikana pia kama "Raisi wa Bagamoyo," alikuwa mkazi wa Bagamoyo katika mkoa wa Pwani. Umaarufu wake ulivuka mipaka, ukifikia umaarufu wa kimataifa, haswa nchini Kenya mnamo 2022 wakati video yake "Kata simu, tupo site" ilipovuma kwenye mitandao ya kijamii. Sasa hivi Mzee wa Mjegeje ni marehemu.
MZEE MPILI
View attachment 2965139
Shabiki na mwanachama mwandamizi wa Yanga SC Mzee Haji Omary Mpili ni mkazi wa Rufiji Pwani katika kijiji cha Ngomboloni. Mzee Mpili ajipatia umaarufu mkubwa siku za karibuni baada ya kauli yake ya ‘Sisi Tuna Watu, Hatuwezi Kufungwa na Simba’ kutafsiriwa kama kauli iliyowapa nguvu Wana Yanga kuibuka na ushindi katika pambano la ligi kuu bara Julai 3, 2021. Mzee Mpili huonekana kama mzee mtata na mwenye uchu wa mafanikio kwa timu yake (Yanga).
STEVE “KULIALIA”
View attachment 2965143
Wakati Yanga ilipofungwa na Simba mabao 5-0 wakati fulani Steven alilia sana, akapigwa picha mbalimbali, akahojiwa na redio na televisheni huku akiwa anabubujikwa machozi, akawasimanga waamuzi kuwa ndiyo chanzo cha klabu yake kufungwa. Alipata umaarufu baada ya video zake kuzagaa mitandaoni. Leo hii Steven ni shabiki mkubwa wa Azam.
KUNZE NA DOTTO
View attachment 2965145
Hawa bwana waliotrend mtandaoni na video yao moja ambapo mmoja anajichukua video akisema, "Oya, Jafe! Mbona hujatokea, sisi tunamaliza mjomba!”. Inaonekana walikuwa wakimpigia mshikaji wao ambaye hakutokea kwenye gradu, hivyo wakawa wanamuonesha mambo yalivyokuwa yamenoga. Hawa jamaa walikuja Dar kutoka kwao huko na wakajaribu kuingia kwenye uchekeshaji. Sina hakika kama walitoboa.
Well, nitaendelea kuongeza kwa kadiri nitakavyokumbuka na kupata wasaa wa kuongeza hii orodha.