Watanzania wameamua kuwa wamoja kulinda Rasilimali zao. Hii haijawahi kutokea

Bush Dokta

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2023
Posts
24,831
Reaction score
45,154
Tangu mimi binafsi nimezitambua na kuzionja siasa za Vyama vingi hapa Tanzania tangu ianzw rasmi 1992 nakiri kabisa hakujawahi kuwa na umoja kama huu.

Vyama mbali mbali vya siasa na asasi za kiraia mbali mbali zimekuwa zikielimisha wananchi kuhusu elimu ya kiraia na kutanabaisha ipo siku watanzania wataelewa.

Kiukweli asasi hizo na taasisi mbali mbali hazikuchoka. Japo watawala miaka yote wamekuwa wakitumia itikadi za kuwagawa yaani Devide and Rule.

Walitumia mbinu mbali mbaki ikiwemo vyama vya siaaa, wanasiasa mamluki na wakati mwingine ikilazimika walitumia itikadi za kidini huku wakitisha wananchi kuwa Nchi itagawanyika.

Huku wakihidhatiti kuwahawa na kule wakiendelea kutafuna mkate wa Taifa wao na genge lao.

Mwaka 2023 huenda ndio ukawa mwisho kwa watawala kuwadharau watanzania.

Kila kona ya nchi mitaani na mikutanoni tumeshuhudia sasa Watanzania wakidai haki zao kwa umoja wao bila kujali Dini, vyama, kabila wala kanda zao.

Hili limewatisha watawala.

Wasipobadilika basi itakuwa ni Sikio la Kufa.
 
20230821_133253.jpg
 
Wafia DP world na wafaidika wa kundi la kifisadi watakuja kukuuliza... Watanzania gan hao? Means wanaamini watanzania bado ni wale wa 1977!!
 
Back
Top Bottom