Ndebile
JF-Expert Member
- Sep 14, 2011
- 7,745
- 11,267
Mkuu unaonaje ukisema kuwa "msukosuko wa kiafya uliotokana na dawa za kulevya....dini inawafanya watu kuwa wanafiki sijuhi kwanini!Kinachoniuma ni kuwa, baada ya Rose kupata misukosuko ya kiafya
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu unaonaje ukisema kuwa "msukosuko wa kiafya uliotokana na dawa za kulevya....dini inawafanya watu kuwa wanafiki sijuhi kwanini!Kinachoniuma ni kuwa, baada ya Rose kupata misukosuko ya kiafya
Hakuna shaka kwamba msanii nguli wa nyimbo za injili, Rose Muhando, ndiye malkia na gwiji wa nyimbo za injili Afrika Mashariki na Kati. Msaanii huyu alianza kuvuma kwa muda mrefu sana na kiwango chake kimebakia juu pamoja na kwamba umri wake kwa sasa umesogea. Album kali kabisa ya Rose Muhando nilianza kuisikia mwaka 2008 lakini kabla ya hapo naambiwa alikwishatoa album moja matata sana (ambayo nadhani ndio ilikuwa album ya kwanza). Na tangu nimfahamu sijawahi kuchoka kusikiliza nyimbo zake zenye upako:
Pamoja na umaarufu wa Rose, siku za karibuni ilionekana kama vile afya yake imetetereka na akawa kimya kwa muda bila kuingia studio kufyatua vibao vipya. Kwa mara ya kwanza nilimuona akiombewa na mchungaji mmoja kutoka huko Kenya na kweli afya yake haikuwa sawa:
Baada ya tukio lile baadhi ya watanzania wasiomtakia mazuri walianza kumzushia uzushi wa hapa na pale ilimradi kila mtu alisema lake. Wengine walisema yupo hoi taabani anaumwa na hata kumzushia kuwa anasumbuliwa na majini. Sio vizuri ndugu zangu. Toa kwanza boriti kwenye jicho lako ndipo utaona kibanzi kwenye jicho la mwenzako (Luka 6:41-45).
Mbaya zaidi, watu wengine wakamzushia kifo. Mmoja wa watanzania hawo wasiomtakia mema ni ndugu anayemtaja kwenye video hapa chini. Ukweli ni kwamba Rose sasa ameimarika kiafya na anaendelea kuihubiri injili ya Bwana wetu Yesu Kristo kuptitia uimbaji kama anavyokiri mwenyewe (sikiliza video). Tuache uzushi ndugu zangu, sio kitu kizuri:
Kinachoniuma ni kuwa, baada ya Rose kupata misukosuko ya kiafya, nilitarajia watanzania wawe wa kwanza kumtakia mema kiuzalendo zaidi lakini wao ndio wamekuwa mstari wa mbele kumnyali mitandaoni na kumtamkia maneno mbofumbofu. Hata wachungaji wa kitanzania nao hawakwepi lawama hizi kwani walishindwa kumuombea hadi ikabidi aende kuombewa nchini Kenya. Hii ni ishara mbaya sana kwa watanzania na ni kiashiria cha kuporomoka kwa uzalendo na umoja wa kitaifa tulioachiwa na mwasisi wa taifa hili, hayati Julius Kambarage Nyerere. Watanzania tunakwama wapi hasa? Kwanini hatupendani? Uzalendo na utaifa aliotuachia baba wa taifa umepotelea wapi?
Kitendo cha watanzania kumshit Rose ni kama vile waliamua kumtelekeza porini akaokotwa na wasamalia wema (Wakenya). Kama shukrani zake kwa wakenya waliomuokota baada ya kutupwa porini, Rose ametunga kibao hiki hapa kuisifu na kuiombea serikali ya Kenya kwa sababu ya watu wake kumpa sapoti ya kutosha:
Kama nilivyotangulia kusema, Rose ni mwanamuziki nguli na ni deal kubwa kwa promoter yeyote wa muziki anayejua kutumia vizuri vipaji vya wasanii. Hapa Tanzania kuna mtu mmoja anaitwa Alex Masama anayewapromote wanamuziki wa nyimbo za injili. Namulaumu sana kwa kumuacha Rose aende kujenga uchumi wa wakenya badala ya kumzuia abakie hapa hapa nchini. Ama kweli nabii hakubaliki kwao. Wakenya sasa hivi wanapiga hela ndefu mno kupitia Rose. Tazama jinsi anavyokusanya mtiti wakenya wanagema sadaka wanajenga uchumi wa nchi yao:
Uzembe wa watanzania kama huu tulioufanya kwa Rose ndio umepelekea wakenya wajitangazie kuwa Mlima Kilimnjaro upo kwao na sisi tumekaa kimya. Hatujui kuchangamkia fursa ndio maana tunaonekana vilaza hadi kumtelekeza msanii nguli akaokotwa na wakenya. Sisi tumekalia majungu na kutakiana mabaya badala ya kunyanyuana kama ndugu. Shame on us!
Watanzania ni shida sana hasa kwenye suala la kunyanyuana kwa hali na mali. Ifike mahali watanzania tujenge utamaduni wa kupendana na kusapotiana kwa kila jambo jema kwa maslahi mapana ya taifa letu. Kitendo cha kinyama alichofanyiwa Rose Muhando hakitaiacha nchi hii salama.
"Sijawahi kuchoka kusikiliza nyimbo za rose muhando"
Una roho ngumu sana kusikiliza nyimbo zake, bora ungesema Christina shusho na Martha mwaipaja.
Asante sana kwa taarifa hii muhimu mkuu. Watanzania wote tutakuwepo kumsikiliza malkia wa nyimbo za injili akiunguruma.Atakuwepo June 26, Tamasha la Vijana la Twenzetu kwa Yesu, Uwanja wa Uhuru jijini DSM, Tamasha linaandaliwa na Upendo Media, KKKT dayosisi ya Mashariki na Pwani. Ataimba nyimbo zake zote. Njooni mumuone.
Kama hukumsaidia wewe na ulikuwa karibu yake. Unataka sisi ambao hata hatujawahi kumuona laivu tutume hela au tungejuaje?Wamentupa mkuu. Hebu niambie msaada hata mmoja waliompa kipindi alipopatwa na misukosuko. Watanzania tuache unafiki. Tupendane.
Kuna wimbo unaoitwa " ndivyo ulivyo" haki ya nani wimbo nauelewa, ule pale Rose alimhusisha roho mtakatifu maana wimbo una mguso wa ndani.Nyimbo zake ni kelele tupu, sidhani Mungu anapenda makelele anayoimba Rose muhando...ndio maana hata watu wa madisko huthubutu kupiga nyimbo zake kwenye vigodoro
Cjaelewa tumemtupa vp Kwan kwenye matamasha yake walikua watu wanaingia bureHakuna shaka kwamba msanii nguli wa nyimbo za injili, Rose Muhando, ndiye malkia na gwiji wa nyimbo za injili Afrika Mashariki na Kati. Msaanii huyu alianza kuvuma kwa muda mrefu sana na kiwango chake kimebakia juu pamoja na kwamba umri wake kwa sasa umesogea. Album kali kabisa ya Rose Muhando nilianza kuisikia mwaka 2008 lakini kabla ya hapo naambiwa alikwishatoa album moja matata sana (ambayo nadhani ndio ilikuwa album ya kwanza). Na tangu nimfahamu sijawahi kuchoka kusikiliza nyimbo zake zenye upako: