Watanzania wamemtupa Rose Muhando porini, ameokotwa na Wakenya

Kinachoniuma ni kuwa, baada ya Rose kupata misukosuko ya kiafya
Mkuu unaonaje ukisema kuwa "msukosuko wa kiafya uliotokana na dawa za kulevya....dini inawafanya watu kuwa wanafiki sijuhi kwanini!
 
Mkuu unaonaje ukisema kuwa "msukosuko wa kiafya uliotokana na dawa za kulevya....dini inawafanya watu kuwa wanafiki sijuhi kwanini!
Mkuu nakusikiliza kama una taarifa sahihi kuhusu hili liweke hadharani watanzania waelewe.
 
Watanzania wamemtupa?
Au yeye mwenyewe kaingia mitini?
 
Watanzania wamemtupa?
Au yeye mwenyewe kaingia mitini?
Watanzania wamemtupa kwa kuwa alipopata misukosuko hapa nchini hawakumsaidia hadi alipoenda Kenya ndipo akapata msaada unaotakiwa mkuu.
 
Watanzania wamemtupa?
Au yeye mwenyewe kaingia mitini?
Wamentupa mkuu. Hebu niambie msaada hata mmoja waliompa kipindi alipopatwa na misukosuko. Watanzania tuache unafiki. Tupendane.
 
Atakuwepo June 26, Tamasha la Vijana la Twenzetu kwa Yesu, Uwanja wa Uhuru jijini DSM, Tamasha linaandaliwa na Upendo Media, KKKT dayosisi ya Mashariki na Pwani. Ataimba nyimbo zake zote. Njooni mumuone.
 
kiukweli kwa sasa gari limewaka upya rose mhando.

lakini tusilaumi sana,imawezekana kama amgeponea nyumbani kwao tz asingeinuka kisanii tena.tatizo tuna tabia ya kupuuza waimbaji wa muda mrefu kumbe ni lulu sehemu nyingine.

binafsi nimefurahi sana kumwona rose kwenye uimbaji tena.
 
"Sijawahi kuchoka kusikiliza nyimbo za rose muhando"

Una roho ngumu sana kusikiliza nyimbo zake, bora ungesema Christina shusho na Martha mwaipaja.

hata mond kuna nyimbo anaimba ni trash,lakini huwezi sema ni kila wimbo.

zipo nyimbo ziko poa sana tu.
 
Jamani ndugu zangu watanzania tujaribu kupunguza unafiki japo kidogo ili tuwe tunasaidiana ktk shida na raha za hapa na pale.
 
Atakuwepo June 26, Tamasha la Vijana la Twenzetu kwa Yesu, Uwanja wa Uhuru jijini DSM, Tamasha linaandaliwa na Upendo Media, KKKT dayosisi ya Mashariki na Pwani. Ataimba nyimbo zake zote. Njooni mumuone.
Asante sana kwa taarifa hii muhimu mkuu. Watanzania wote tutakuwepo kumsikiliza malkia wa nyimbo za injili akiunguruma.
 
Wamentupa mkuu. Hebu niambie msaada hata mmoja waliompa kipindi alipopatwa na misukosuko. Watanzania tuache unafiki. Tupendane.
Kama hukumsaidia wewe na ulikuwa karibu yake. Unataka sisi ambao hata hatujawahi kumuona laivu tutume hela au tungejuaje?

Wewe uliyeandika ukijua ana shida na haukufanya , sipangaratwike malafyale
 
Ni nani aliemtupa Rose muhando porini mkuu?

Mbona tunasingiziana?
 
Nyimbo zake ni kelele tupu, sidhani Mungu anapenda makelele anayoimba Rose muhando...ndio maana hata watu wa madisko huthubutu kupiga nyimbo zake kwenye vigodoro
Kuna wimbo unaoitwa " ndivyo ulivyo" haki ya nani wimbo nauelewa, ule pale Rose alimhusisha roho mtakatifu maana wimbo una mguso wa ndani.
 
Cjaelewa tumemtupa vp Kwan kwenye matamasha yake walikua watu wanaingia bure
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…