Watanzania wameshauriwa kuondoa hicho kituko cha nyungu kilicho Muhimbili na waanze kufuata mbinu za sayansi

MK254

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2013
Posts
32,408
Reaction score
50,809
Kuna huyu mbunge wa Tanzania ambaye ni CCM kindakindaki anayeitwa Hamis Kigwangalla, ameshauri waondoe hicho kitu walichoweka kwenye hospitali ya taifa ya Muhimbili na kuanza kukumbatia mifumo na mbinu za kisayansi ili kukabiliana na corona.

Inachekesha sana maana hawa waliimba sana mapambio, ni kama wamepata uhuru wa kuanza kutumia ubongo ghafla......

Kuna yule mwingine anayeitwa Jaffo ambaye ndiye alikua kiongozi wa nyungu, siku hizi ni full barakoa

 
Kinachonishangaza siyo kauli ya huyu mbunge ila ni kwa nini Waziri wa Afya na msaidizi wake bado wapo ofisini, baada ya nchi kupitia kilichotokea kutokana na ushauri mbovu, walipaswa kuonyeshwa mlango wa kutokea.

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
 
Bila picha ni sawa na utumbo bila harufu ya nanihii....
Ni kweli, Dr. Kigwangwalla kasema hivyo.
Ni audio nimemsikia imewekwa hapa JF na inasambaa mitandaoni.
Amesema lile dubwasha la kujifukiza pale Muhimbili linapaswa kuondolewa haraka.

Nasikia kuna wasela wamesema kama itaisha wiki mbili kutoka sasa na lile dubwasha la kujifukiza halijaondolewa pale Muhimbili basi watajipanga kwenda kuliondoa wao kinguvu. Wanasema kama mabango ya picha ya Magufuli ambaye alikuwa mtetezi wa wanyonge yanang'olewa kwa kasi mitaani, kwanini lile limtambo (mradi wa watu fulani wanaopiga dili) libakie pale Muhimbili ? Mambosasa bado hajatoa tamko.
 
The legacy ....!!!
Your browser is not able to display this video.
 
Huyu mbunge aliunga mkono mbinu za Kinjekitile alizoamini mwendazake sasa amebadilika kama kinyonga.

Haya maneno yalifaa yatamkwe na Dr Nfmdungulile, daktari wa ukweli aliyetueleza madhara ya kujivukiza katika mfumo wa hewa.
 
Hii Muhimbili ambayo tunapigiwa kelele humu eti best in East and Central Africa? 🤣 🤣 🤣
 
Tujikumbushe
 
Kigwa mnafki tu kwanini hakusema wakati wa uhai wa jiwe
 
Hayo yaliwekwa kwa ajili ya kampeni. Na kampeni zilishaisha, sasa yaendelee kuwepo kwa ajili ya nini tena? Ni sahihi kuyaondoa.
Jombaa, wewe ndio ulikuwa balozi mkubwa wa 'tiba'/'chanjo' yenu asili ya kupiga nyungu humu kwenye jukwaa hili. Vipi leo unajitia hamnazo na hutoi maoni yako kuhusu mada halisi ya uzi huu? Ndio maana muda huu wa pasaka tukimkumkumbuka Masiya huwa hatumsahau msaliti wake Judas. [emoji1]
 

Hakuna kitu ambacho nimebadirisha katika maisha yangu.
Pia nyumbani hali ni ileile.
Mimi namlilia tu mwamba wetu kuondoka katika kipindi tunachomuhitaji.
😭 😭 😭
 
Hakuna kitu ambacho nimebadirisha katika maisha yangu.
Pia nyumbani hali ni ileile.
Mimi namlilia tu mwamba wetu kuondoka katika kipindi tunachomuhitaji.
[emoji24] [emoji24] [emoji24]
Akili za kuambiwa..... jaza pengo na poleni tena kwa msiba.
 
To hell with lockdown, tutaishi na corona kama tunavyoishi na mafua-uk
Vipi mkuu mnaiga lini toka kwa vidume wenu?
 
Hayo yaliwekwa kwa ajili ya kampeni. Na kampeni zilishaisha, sasa yaendelee kuwepo kwa ajili ya nini tena? Ni sahihi kuyaondoa.
Kampeni ziliisha lini? Kwanini yaondewe sasa na si wakati ule?
 
Akili za kuambiwa..... jaza pengo na poleni tena kwa msiba.

Nilisha changanya na zangu,
pia JPM atafuatwa daima.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…