kifupi kirefu
JF-Expert Member
- Oct 29, 2018
- 539
- 3,507
Mtanzania yuleyule anayeandika kwenye barua, kwenye mtandao wa kijamii au anayezungumza kutoa pole na kuomba dua anaposikia msiba ndiye huyohuyo anayekuona upo kwenye hatari ya kifo asiseme kitu.
Hakuna Mtanzania kiongozi wa kitaifa aliyesimama nakusema kuwaweka mahabusu watu bila sababu za msingi nikuwaweka kwenye tishio la maambukizi ya corona. Hakuna kiongozi wa kisiasa aliyewauliza polisi kwamba taarifa za kushindwa kupumua za Heche huko Mwanza ni za kweli? Kama si za kweli akanushe adharani. Lakini kiumbe huyohuyo akitutoka leo utashangaa barua za maombolezo na uwakilishi wa vyama wakikimbilia msibani bila kujua wao ndio chanzo au walikuwa na nafasi yakuokoa uwahi wake.
Leo hii kwa bahati mbaya Mbowe akiugua UVIKO na akatutoka utashangaa watu wale wale waliomweka mahabusu bila sababu kwa siku zaidi ya nne kinyume cha sheria wakitoa salamu za pole. Watu hao hao wataunda tume na kuwasimamisha kazi Askari wa juu na chini kupisha uchunguzi hata Kama awatamaanisha.
Watu hao hao watatokea kwenye msiba kutoa sifa nzuri za Marehemu. Huu ni unyama, ni roho za kikatili tunazijenga kwa Taifa letu.
Bora usitoe pole kuliko kutoa pole kwa kifo ulichokuwa unaweza kukidhuia.
Huko Mwanza wizara ilikaa kimya kuhusu mitungi ya gesi, watu wakafa na habari zikaenea mitandaoni mara tunaona mitungi Tena na camera juu pamoja na pongezi. So tulisubiri watu wakose oxygen wafe ndipo tuchukue mitungi tupeleke?
Kilimanjaro tumesikia Hali ilivyo kwa Sasa, wizara ile ile iliyoelezwa tatizo la Mwanza haina uwezo wakutatua tatizo sehemu nyingine Hadi watu wafe? Waziri wa afya kazi yako Nini? Waziri wa Mambo ya Ndani unafanya Nini? Kwanini mnaona rahisi Sana kushuhudia watu wanapoteza uhai mikononi mwenu? Kwanini msisimae nakutekeleza wajibu?