MK254
JF-Expert Member
- May 11, 2013
- 32,408
- 50,809
Siwaelewi Watanzania, wanatupigia makelele kwa sisi kukopa, ilhali wao wanabembeleza kila taasisi iwape mikopo, japo bado hawajasklizwa.
-------------------------------
Waziri wa Fedha, Dkt. Philip Mpango, amekutana na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Barclays Kanda ya Afrika, Peter Matlare na kuiomba Benki hiyo kuangalia uwezekano wa kutoa mkopo nafuu wa ujenzi wa miradi mikubwa inayotekelezwa na Serikali ukiwemo ujenzi wa Reli ya Kati kwa viwango vya kimataifa (SGR) na Mradi wa Miundombinu ya Umeme wa Stieglar's Gorge ili kuharakisha maendeleo ya kiuchumi kupitia viwanda.
Amemweleza kiongozi huyo kuwa Serikali imeimarisha uchumi wake kwa kudhibiti mfumuko wa bei ambao uko katika kiwango cha tarakimu moja cha wastani wa asilimi 5.3 katika kipindi cha miezi 6 iliyopita.
"Tumewekeza kwenye miundombinu kama vile elimu, maji, kilimo, afya, madini na biashara na katika kipindi kifupi cha miaka miwili (2) zaidi ya viwanda 80 vimejengwa katika eneo la Mkuranga mkoani Pwani, kutokana na fursa za uwepo wa bomba la gesi na eneo hilo kuwa karibu na Bandari ya Dar es Salaam.
Dkt. Mpango ameelezea pia mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kati kwa kiwango cha Kimataifa utarahisisha usafiri na usafirishaji wa abiria na mizigo katika nchi zinazopakana na Tanzania hivyo kukuza biashara kwa kiwango kikubwa.
Akizungumzia kuhusu ujenzi wa mradi mkubwa wa umeme katika Bonde la mto Rufiji (Stiegler's Gorge), Dkt. Mpango amesema lengo la mradi huo utakaozalisha megawati 2,100 za umeme na utakuwa wa uhakika na bei nafuu ili kukuza viwanda.
Alisema kuwa mwelekeo wa Serikali kwa sasa ni kuhakikisha kuwa kila biadhaa zinazozalishwa nchini pamoja na madini, vinaongezwa thamani hapa nchini badala ya kuuzwa kama malighafi na kwamba nishati ya umeme ndiyo nguzo kuu ya kufikia malengo hayo.
Kwa upande wake, Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo ya Barclays anayehudumia kundi la benki za Barclays Barani Afrika na kwingineko Marekani na Ulaya, Peter Matlare, ameipongeza Serikali chini ya Rais Dkt. John Magufuli kwa kusimamia kikamilifu uchumi wa nchi unaokua kwa wastani wa asilimia 7.
Alisema hatua hiyo ni ya kupigiwa mfano katika nchi za Afrika na Duniani kwa jumla ambapo amesema Tanzania imekuwa ikifanya vyema katika kukuza uchumi jumuishi unaowafikia watu wengi zaidi wakiwemo waishio mijini na vijijini.
Peter Matlare amemhakikishia Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango kwamba Benki yake itayafanyia kazi mapendekezo ya kutaka ushiriki wake katika ujenzi wa miradi mikubwa iliyoainishwa na Serikali kuwa kipaumbele chake.
Dkt. Mpango amwangukia Bosi wa Barclays | Azam | Biashara | Swahili