Watanzania waomba Barclays mkopo kwa ajili ya SGR na Stieglar's Gorge

MK254

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2013
Posts
32,408
Reaction score
50,809
Siwaelewi Watanzania, wanatupigia makelele kwa sisi kukopa, ilhali wao wanabembeleza kila taasisi iwape mikopo, japo bado hawajasklizwa.
-------------------------------
Waziri wa Fedha, Dkt. Philip Mpango, amekutana na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Barclays Kanda ya Afrika, Peter Matlare na kuiomba Benki hiyo kuangalia uwezekano wa kutoa mkopo nafuu wa ujenzi wa miradi mikubwa inayotekelezwa na Serikali ukiwemo ujenzi wa Reli ya Kati kwa viwango vya kimataifa (SGR) na Mradi wa Miundombinu ya Umeme wa Stieglar's Gorge ili kuharakisha maendeleo ya kiuchumi kupitia viwanda.

Amemweleza kiongozi huyo kuwa Serikali imeimarisha uchumi wake kwa kudhibiti mfumuko wa bei ambao uko katika kiwango cha tarakimu moja cha wastani wa asilimi 5.3 katika kipindi cha miezi 6 iliyopita.

"Tumewekeza kwenye miundombinu kama vile elimu, maji, kilimo, afya, madini na biashara na katika kipindi kifupi cha miaka miwili (2) zaidi ya viwanda 80 vimejengwa katika eneo la Mkuranga mkoani Pwani, kutokana na fursa za uwepo wa bomba la gesi na eneo hilo kuwa karibu na Bandari ya Dar es Salaam.

Dkt. Mpango ameelezea pia mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kati kwa kiwango cha Kimataifa utarahisisha usafiri na usafirishaji wa abiria na mizigo katika nchi zinazopakana na Tanzania hivyo kukuza biashara kwa kiwango kikubwa.

Akizungumzia kuhusu ujenzi wa mradi mkubwa wa umeme katika Bonde la mto Rufiji (Stiegler's Gorge), Dkt. Mpango amesema lengo la mradi huo utakaozalisha megawati 2,100 za umeme na utakuwa wa uhakika na bei nafuu ili kukuza viwanda.

Alisema kuwa mwelekeo wa Serikali kwa sasa ni kuhakikisha kuwa kila biadhaa zinazozalishwa nchini pamoja na madini, vinaongezwa thamani hapa nchini badala ya kuuzwa kama malighafi na kwamba nishati ya umeme ndiyo nguzo kuu ya kufikia malengo hayo.

Kwa upande wake, Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo ya Barclays anayehudumia kundi la benki za Barclays Barani Afrika na kwingineko Marekani na Ulaya, Peter Matlare, ameipongeza Serikali chini ya Rais Dkt. John Magufuli kwa kusimamia kikamilifu uchumi wa nchi unaokua kwa wastani wa asilimia 7.

Alisema hatua hiyo ni ya kupigiwa mfano katika nchi za Afrika na Duniani kwa jumla ambapo amesema Tanzania imekuwa ikifanya vyema katika kukuza uchumi jumuishi unaowafikia watu wengi zaidi wakiwemo waishio mijini na vijijini.

Peter Matlare amemhakikishia Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango kwamba Benki yake itayafanyia kazi mapendekezo ya kutaka ushiriki wake katika ujenzi wa miradi mikubwa iliyoainishwa na Serikali kuwa kipaumbele chake.

Dkt. Mpango amwangukia Bosi wa Barclays | Azam | Biashara | Swahili
 
Nadhani watu wengi hawajaulewa huu mradi, na kusini pia Mtwara - Nyasa unaaza kuivishwa.
Wakenya wengi ni Wajinga na wapumbavu sana, ukizungumza naowanatia hasira,
Siku moja nlikaa na mademu Fulani Bar Pale westlands, yaani unatumia nguvu nyingi kuwaelewesha vitu vidogo kabisa hadi unapata hasira,
Mfano, huyu mleta mada pamoja na kujinasibu humu kujifanya anaijua Tz Leo anakuja na kituko kama hiki, si Kubwajinga hili?
 
Siwaelewi Watanzania, wanatupigia makelele kwa sisi kukopa, ilhali wao wanabembeleza kila taasisi iwape mikopo, japo bado hawajasklizwa.
-------------------------------
Waziri wa Fedha, Dkt. Philip Mpango, amekutana na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Barclays Kanda ya Afrika, Peter Matlare na kuiomba Benki hiyo kuangalia uwezekano wa kutoa mkopo nafuu wa ujenzi wa miradi mikubwa inayotekelezwa na Serikali ukiwemo ujenzi wa Reli ya Kati kwa viwango vya kimataifa (SGR) na Mradi wa Miundombinu ya Umeme wa Stieglar's Gorge ili kuharakisha maendeleo ya kiuchumi kupitia viwanda.

Amemweleza kiongozi huyo kuwa Serikali imeimarisha uchumi wake kwa kudhibiti mfumuko wa bei ambao uko katika kiwango cha tarakimu moja cha wastani wa asilimi 5.3 katika kipindi cha miezi 6 iliyopita.

"Tumewekeza kwenye miundombinu kama vile elimu, maji, kilimo, afya, madini na biashara na katika kipindi kifupi cha miaka miwili (2) zaidi ya viwanda 80 vimejengwa katika eneo la Mkuranga mkoani Pwani, kutokana na fursa za uwepo wa bomba la gesi na eneo hilo kuwa karibu na Bandari ya Dar es Salaam.

Dkt. Mpango ameelezea pia mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kati kwa kiwango cha Kimataifa utarahisisha usafiri na usafirishaji wa abiria na mizigo katika nchi zinazopakana na Tanzania hivyo kukuza biashara kwa kiwango kikubwa.

Akizungumzia kuhusu ujenzi wa mradi mkubwa wa umeme katika Bonde la mto Rufiji (Stiegler's Gorge), Dkt. Mpango amesema lengo la mradi huo utakaozalisha megawati 2,100 za umeme na utakuwa wa uhakika na bei nafuu ili kukuza viwanda.

Alisema kuwa mwelekeo wa Serikali kwa sasa ni kuhakikisha kuwa kila biadhaa zinazozalishwa nchini pamoja na madini, vinaongezwa thamani hapa nchini badala ya kuuzwa kama malighafi na kwamba nishati ya umeme ndiyo nguzo kuu ya kufikia malengo hayo.

Kwa upande wake, Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo ya Barclays anayehudumia kundi la benki za Barclays Barani Afrika na kwingineko Marekani na Ulaya, Peter Matlare, ameipongeza Serikali chini ya Rais Dkt. John Magufuli kwa kusimamia kikamilifu uchumi wa nchi unaokua kwa wastani wa asilimia 7.

Alisema hatua hiyo ni ya kupigiwa mfano katika nchi za Afrika na Duniani kwa jumla ambapo amesema Tanzania imekuwa ikifanya vyema katika kukuza uchumi jumuishi unaowafikia watu wengi zaidi wakiwemo waishio mijini na vijijini.

Peter Matlare amemhakikishia Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango kwamba Benki yake itayafanyia kazi mapendekezo ya kutaka ushiriki wake katika ujenzi wa miradi mikubwa iliyoainishwa na Serikali kuwa kipaumbele chake.

Dkt. Mpango amwangukia Bosi wa Barclays | Azam | Biashara | Swahili
Ina maana nyuzi zote zimefunguliwa humu tukikuhubiria kuwa tunajenga kwa fedha za ndani SGR Dar-Moro-Makutupora ilikuwa ni kupigia Mbuzi gitaa?
Kwamba huelewi hii Reli ya Kati inatakiwa kufika Kigali, Northern DRC hadi Kampala?
 
Tutajenga kwa pesa zetu nyef nyef nyef...serikali imetoa 3.5b USD blah blah blah [emoji23]
 
Ina maana nyuzi zote zimefunguliwa humu tukikuhubiria kuwa tunajenga kwa fedha za ndani SGR Dar-Moro-Makutupora ilikuwa ni kupigia Mbuzi gitaa?
Kwamba huelewi hii Reli ya Kati inatakiwa kufika Kigali, Northern DRC hadi Kampala?

Hehehe umeguswa penyewe, mapovu yatakupa presha bure, hizi hapa ni taarifa nine copy paste na kuweka chanzo kabisa.
Mnasaka mikopo na kubembeleza kila taasisi, halafu unanipigia makelele.
 
Hizo ni pesa za phases zijazo sgr haishii Dodoma inaenda Tabora, Shinyanga, Mwanza, Kigoma, Katavi,

Phase nyingine inaenda Mtwara, Lindi, Arusha na Musoma sasa unataka hizo pesa tuzitoe wapi?
 
Hehehe!! Mnafurahisha jinsi mnavyotumia nguvu nyingi, unaniuliza mtoe wapi pesa, kwani si nyie ndio huwa mnasema mnazo na haitokuja siku mkope, ilhali mnamfuata Zuma awatafutie mikopo, mara mnafuata Barclays, mnafuata kila sehemu.
Mnatunisha misuli na kupambana kuonyesha ubabe msiokua nawo.
 
Angalau sisi SGR phase I &II tunajenga kwa fedha zetu,,siyo mbaya kwa phase zingine tukatafuta mkopo,,anyway ni mara kumi huu mkopo tunaotafuta kuliko ule mliopewa wenye masharti magumu ya kummilikisha SGR Mchina.!
 
Hehehe!! Mnafurahisha jinsi mnavyotumia nguvu nyingi, unaniuliza mtoe wapi pesa, kwani si nyie ndio huwa mnasema mnazo na haitokuja siku mkope, ilhali mnamfuata Zuma awatafutie mikopo, mara mnafuata Barclays, mnafuata kila sehemu.
Mnatunisha misuli na kupambana kuonyesha ubabe msiokua nawo.
Basi jinyonge. Mbona povu zito hivyo kama pesa tunatoa kwenu. By the way hata mkopo tunaomba Barclays Tanzania.
 
Hehehe umeguswa penyewe, mapovu yatakupa presha bure, hizi hapa ni taarifa nine copy paste na kuweka chanzo kabisa.
Mnasaka mikopo na kubembeleza kila taasisi, halafu unanipigia makelele.
Mara ilianza na fununu za Dar asks turkey for 400km rail loan.. Alafu baadae tukaambiwa it was only contract, Dar to fund 100%, next tukaskia world bank hold talks, haukupita muda tukaambiwa AfDB to fund Central rail loan, punde si punde Tukaskia loan inatafutwa ndani ya BRICS kupitia SA, sahii imegeuka sasa Barclays bank holding talks.
Seems to me like hawa jamaa wakiamua kutegemea loan watangoja sana, afadhali waamue kutumia robo ya bajeti kwa huu mradi kila mwaka hadi ujenzi ukamilike manake loan hazitakuja leo wala kesho
 
Utasikia hata CHINA wanataka kukopesha kwa ajili ya SGR.

Tanzania SGR ni zaidi ya 2,100 kilometres
 
Nakumbuka tuliambiwaga na mkuu kwamba upo mzigo wa kutosha kwa ajili ya made stieglar's gorge,sasa sijui mie ndio nimesahau au?
 
Back
Top Bottom