Watanzania wasomi na wasio wasomi lakini ni wajasiriamali acheni kukodi fremu ili kufungua biashara

Watanzania wasomi na wasio wasomi lakini ni wajasiriamali acheni kukodi fremu ili kufungua biashara

Sijajua shida nini, sijui huwa wana mwapu wa kufanya biashara.

Ila wenye fremu kwetu ni raha tu, akishindwa huyu anakuja yule, na kama fremu zipo sehemu nzuri unapiga pesa vizuri tu.

Ni biashara ambayo unaweza funga msuli na ukacheza bao, mwisho wa mwezi unaokota tu.
Hana uzoefu huyu. Biashara na physical. Huwezi kuwapostia watu bidhaa kila siku, mwezi mzima mtu ananunua siku moja tu
 
Jamani eeh, kukodi fremu ufungue duka unapoteza hela zako. Somo hili kichwa cha habari hii kinahusika.

Hii tabia imekithiri sana hapa nchini. Utakuta mjasiriamali analipa pesa nyiiiingi kulipia chumba cha duka akitarajia kupata pesa nyingi, ni kosa kubwa sana.

Njia zifuatazo zinaweza tumika badala ya kumfadisha landlord's.

1. Tangaza biashara yako pelekea wateja wewe mwenyewe (huu mfumo door to door upo lkn kidogo sana)
2. Tumia social media kuuza bidhaa.
Sio biashara zote unaweza fanya na mtu hana ofisi.
 
Jamani eeh, kukodi fremu ufungue duka unapoteza hela zako. Somo hili kichwa cha habari hii kinahusika.

Hii tabia imekithiri sana hapa nchini. Utakuta mjasiriamali analipa pesa nyiiiingi kulipia chumba cha duka akitarajia kupata pesa nyingi, ni kosa kubwa sana.
Unachosema unaweza kuona ni jambo jema individually ila collectively ni gharama kwa nchi / jamii, kuwa na utitiri wa wachuuzi hata ulipaji kodi unakuwa ni wa kusuasua.....
Njia zifuatazo zinaweza tumika badala ya kumfadisha landlord's.

1. Tangaza biashara yako pelekea wateja wewe mwenyewe (huu mfumo door to door upo lkn kidogo sana)
Unajua kwamba delivery pia ni gharama ?; Ofcourse inaweza kuwa offset na gharama ya chumba; ila pia ni gharama na ukipata order za kutosha unajigawa vipi; Kama ni online kumejaa utapeli hence wengi kutoamini sana online..., na tunapoelekea kama kutakuwa na mfumo wa malipo directly online na hii nchi inayopenda tozo gharama itaongezeka....
2. Tumia social media kuuza bidhaa.
Huko napo competition ni ya nguvu....; unless una following (which makes it a different business altogether) na huko ukipatumia wala huitaji tena kufanya delivery unaweza ukatumia affiliates products (ila ndio hivyo building a community and selling without being seen to sell nayo ni changamoto) Unless utashangaa watu wanakukimbia kwenye hizo Social Media (Just another Seller)

To each their own / There is more than one way to Skin a Cat
 
Frame zimekuwa nyingi zimegeuka uchafu,moja ya kufahamu watu ni masikini ni hizo frame kila kona.
Mfano Dodoma sasa hivi kila moja akijenga anaweka frame nje,mpaka nyumba zinakuwa kama magofu.

Serikali lazama ije na mikakati ya kuondoa mambo ya frame zinasababisha miji inakosa mivuto.

Mfano mzuri ni Nairobi hakuna huo uchafu wa frame kila nyumba,watu hunua mahutaji katika supermarket & Min supermarket.
 
Wingi wa Frame wala sio mzizi wa Tatizo..., mzizi wa tatizo ni utitiri wa watu kukosa ujira hence kila mtu kujaribu na kugawana umasikini Supply ni kubwa kuliko demand (hata hao watu wakiamia online bado itakuwa ni utitiri wa high quantity and with online competition your competitor being a one click away bado watu wataendelea kugawana umasikini.

Anyway issue ya utitiri nilishawahi kwenda toe to toe na huyu mdau Lycaon pictus kwenye uzi wake

Kwa kumueleza anataka kuendelea na muendelezo wa mambo yasiyo na tija....
 
Jamani eeh, kukodi fremu ufungue duka unapoteza hela zako. Somo hili kichwa cha habari hii kinahusika.

Hii tabia imekithiri sana hapa nchini. Utakuta mjasiriamali analipa pesa nyiiiingi kulipia chumba cha duka akitarajia kupata pesa nyingi, ni kosa kubwa sana.

Njia zifuatazo zinaweza tumika badala ya kumfadisha landlord's.

1. Tangaza biashara yako pelekea wateja wewe mwenyewe (huu mfumo door to door upo lkn kidogo sana)
2. Tumia social media kuuza bidhaa.
Unaona umeongea jambo la maaaaaana? Umewaza mpaka mwisho. Nauza mchele na unga. So nitangaze mtu akitaka kilo 2 nampelekea. Akitaka kilo 5 nampelekea mwingine akitaka kilo 3 nampelekea?

Nauza chupi naishi kijitonyama. Nimetangaza mtu kaziona kapenda 3. Nimpelekee temeke? Unajua wanunuaji sehemu kubwa ni wapita njia? Ukiweka nyumbani kwako na kutangaza mitandaoni kuna vitu vidogo vidogo ambavyo gharama ya kupeleka ni nusu ya kununulia. Na suala la muda pia lipo.
 
Biashara ya Salon vipi, utawanyoa na kuwasuka watu online? Wanaupload vichwa au vipi bhana.
Actually hii inafanyika sana hata sasa kuna dada anachukua orders za kwenda kuwasuka watu au kuwanyoa (with an added fee ofcourse); na anapata zaidi kuliko angekuwa na premises (ana tenda mpaka nyingine ana vijana wake)..., So in that case its possible....

That said utitiri wa kila duka kila nyumba na zinauza vitu vilevile mitaa yote (afadhali kungekuwa na mitaa ya nyama, mitaa ya spare, mitaa ya stationery n.k.) ni mipangilio isiyo na tija.....
 
Unaweza ukamuona mjinga anauza vipodozi Ila biashara yake haswa sio vipodozi vipodozi geresha tu, Pesa utafutaji una Siri nyingi usimdharau mtu kwa kila Jambo unaloliona mfuate umuulize unalipa pango laki 4 kwa mwezi unauza vipodozi rejareja kwa mwezi hauingizi hata laki hio Pesa ya pango unalipaje atakachokuambia nahisi utabaki mdomowazi, analipa laki 4 anaingiza milioni 4 sasa laki 4 ni nini kwenye million 4?
Unajua wanapata sh ngapi??

Ni sawa na uende mahali unakuta kuna maduka hayana vitu vingi kwenye mashelf ukawacheka kua wanapoteza pesa kumbe wenzio wanakwepa kodi mzigo unauziwa store huko pale ni geresha tu.

Kama anapata hasara angefunga, kama bado anailipa hiyo laki 4 kila mwezi basi jua wanapiga pesa.

Tena hiyo biashara ya vipodozi ina uhuni mwingi kishenzi.
Wakuu hapa mimi na wewe hatujui, saa zingine tunaambiwa tusijifanye tunawajua watu kuliko wao wanavo jijua hii kauli ndiyo inajidhihirisha hapa.
 
Tatizi sio kukodi frem tatizo eneo fanya kwanza research makini mi mtu hajawai fika hata uo mtaa kisa dalali kampamba analipa miezi sita anakaa mwezi mzima wateja wawili watatu anaamua kuhama kapteza pesa na muda kuna biashara zingine unaweza deliver kama nguo .nk haina haja ya kufunguwa frem kama ndo unaanza anzia online na sehem za bure
Hata hizo nguo, wafungue tu ofisi tu maana Tz kizungumkuti, umeagiza shati umeliona online picha iliyowekwa na quality ya nguo utakayoletewa ni vitu viwili tofauti.

Wawe tu na ofisi kwa kweli, online wapatumie kama display. Uongo mwingi sana nchi hii, kwa wauzaji na wanunuaji.
 
Wakuu hapa mimi na wewe hatujui, saa zingine tunaambiwa tusijifanye tunawajua watu kuliko wao wanavo jijua hii kauli ndiyo inajidhihirisha hapa.
Ndivyo ilivyo, kwa akili ya kawaida tu huwezi fanya kitu kinachokupa hasara namna hiyo
 
Unamaanisha Vunjabei ile miduka yote sijui inafika 20 awe anabeba miguo yote mhongoni anatembeza ngongongo nauza nguo anazunguka nchi nzima maana maduka yake yamelenga nchi nzima

Au miguo yake yote kaiweka geto kwake tu anaposti online

Physical ofisi muhimu first target customers ni wapita njia ndio wanunuzi kwa 95% ndio maana maduka yanaa sehemu yenye mzunguko wa watu Online ni extra tu
 
😂😂😂hapo wewe ndo unaweza kujiona mjinga ukija kujua kias wanachoingiza kwa biashara mkuu mimi nafanya Hiyo biashara reja reja tu nalipa kodi mara mbili ya hiyo na nina uhakika wa net profit siyo chini ya 3.5M hapo gross profit inacheza kwenye 4.5 mpka 5.5M
 
Jamani eeh, kukodi fremu ufungue duka unapoteza hela zako. Somo hili kichwa cha habari hii kinahusika.

Hii tabia imekithiri sana hapa nchini. Utakuta mjasiriamali analipa pesa nyiiiingi kulipia chumba cha duka akitarajia kupata pesa nyingi, ni kosa kubwa sana.

Njia zifuatazo zinaweza tumika badala ya kumfadisha landlord's.

1. Tangaza biashara yako pelekea wateja wewe mwenyewe (huu mfumo door to door upo lkn kidogo sana)
2. Tumia social media kuuza bidhaa.
Finally hao hao wateja watakuuliza "SAMAHANI DUKA LAKO LINAPATIKANA WAPI"

BUSINESS IS ALL ABOUT TAKING RISKY,THEN DON'T COMES WITH EXCUSSES.
 
Frame zimekuwa nyingi zimegeuka uchafu,moja ya kufahamu watu ni masikini ni hizo frame kila kona.
Mfano Dodoma sasa hivi kila moja akijenga anaweka frame nje,mpaka nyumba zinakuwa kama magofu.

Serikali lazama ije na mikakati ya kuondoa mambo ya frame zinasababisha miji inakosa mivuto.

Mfano mzuri ni Nairobi hakuna huo uchafu wa frame kila nyumba,watu hunua mahutaji katika supermarket & Min supermarket.
Aise Nairobi watu wengine...kuna hyo supermarket inaitwa cafo watu wananunua na kufanyiwa delivery hadi nyumbani...hakuna maduka kama huku nilishangaa na bei za supermarket ni affordable hata mtu wa chin anaweza kumudu...utamaduni wa kununua vitu kwa njia hyo huku hamna.
 
Back
Top Bottom