Watanzania wengi hatuna biashara, bali "TUMEJIAJIRI". Biashara ya kweli huendelea hata mmiliki asipokuwepo.

Watanzania wengi hatuna biashara, bali "TUMEJIAJIRI". Biashara ya kweli huendelea hata mmiliki asipokuwepo.

mkata uzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2025
Posts
3,253
Reaction score
9,736
Kuna tofauti kubwa kati ya kujiajiri na kumiliki biashara, lakini mara nyingi tunavitumia kana kwamba ni kitu kimoja.

Wabongo wengi hatuna biashara bali tumejitengenezea ajira (tumejiajiri).

Biashara ya kweli haimtegemei mmiliki kwa kila uamuzi. Ina mfumo wa uendeshaji, watu wenye majukumu, taratibu za kazi na uwezo wa kuendelea kuzalisha mapato hata mmiliki akiwa safarini, mgonjwa au amestaafu.

Kwa Tanzania, mifano rahisi tunaiona kwenye baadhi ya biashara za familia zinazomilikiwa na Wahindi, Waarabu na Wasomali. Mara nyingi biashara hizo hazimtegemei mtu mmoja pekee. Hata mmiliki mkuu asipokuwepo, shughuli zinaendelea kwa sababu kuna mifumo ya uendeshaji, mgawanyo wa majukumu na wanafamilia wengine wanaoendelea kuzisimamia kutoka kizazi hadi kizazi.

Nchi za nje zilizoendelea hata kama mtu hana familia anaiweka biashara kwenye mfumo wa hisa na kuajiri memeneja, ceo, n.k. hata asipokuwepo mwaka mzima biashara inaendelea

Hili ndilo eneo ambalo wafanyabiashara wengi bado wanahitaji kulifanyia kazi. Tunafungua biashara, lakini hatujengi mifumo. Tunakuwa kila mahali, kununua bidhaa, kupokea fedha, kufanya maamuzi, kusimamia wafanyakazi na hata kutatua kila tatizo. Mwisho wake, biashara haiwezi kuishi bila mmiliki.

Ndiyo maana wengi wanapofikisha umri wa kustaafu hawana sehemu ya kupumzika. Hawawezi kuacha kufanya kazi kwa sababu mapato yao yanategemea uwepo wao kila siku.

Kujiajiri ni hatua nzuri ya kuanza. Lakini mafanikio ya kweli ni pale unapojenga biashara inayoweza kuishi, kukua na kukutunza hata pale ambapo huna uwezo wa kuisimamia kila siku.
 
Wazazi wameingiwa na hofu sababu watoto wanasubiri wazazi wafe ili wagawane mirathi
 
Back
Top Bottom