Watanzania wengi hizi dini zipo kujisafisha tu, watu wengi bado wanaendelea kwenda kwa waganga na kuendeleza matambiko ya mizimu

NetMaster

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2022
Posts
1,454
Reaction score
4,925
Ndiyo asili ya Waafrka wengi, huwezi kumtoa mtu asili yake kirahisi rahisi.

Watu kibao nimewaona na chale za kwenye matambiko, niliwahi kuifanya kazi fulani iliyoweza kunipa access ya kuwaperuzi wanaume kwa wanawake wakiwa vifua wazi, ysani ni wengi tu wanazo chale za matambiko ama waganga.

Kuna watu wanarogwa na kuzunguka makanisani na misikitini hasa hii feki feki ya kuigiza, mtu haponi kabisa, hapo kinachobaki huwa ni kwenda kwa waganga tu.
 
Wanajilisha upepo, kimsingi wanaendeshwa na hao walozi, waganga na mizimu.......huko kanisani wanaishia kwenda kuzuga tu au kumpigia Mungu kelele.
 
Dini ni taasisi km taasisi zingine usijisahaulishe ndio maana huwezi kuanzisha kanisa km huna vibali, kwa hio kaa mkao wa kutoa Sadaka na kuchangia ujenzi wa kanisa hayo mengine waachie wenyewe
Waambie hao
 
Karibuni kwa mashahidi wa yehova mjifunze kweli za biblia
 
Waganga ni binadamu kama wewe na viongozi wa dini ni binadamu kama wewe. Kama utashindwa kujua unayemuabudu ni nani, tatizo litaendelea kuwa kwako wala si dini au waganga.
 
Ndiyo asili ya Waafrka wengi, huwezi kumtoa mtu asili yake kirahisi rahisi.

Watu kibao nimewaona na chale za kwenye matambiko, niliwahi kuifanya kazi fulani iliyoweza kunipa access ya kuwaperuzi wanaume kwa wanawake wakiwa vifua wazi, ysani ni wengi tu wanazo chale za matambiko ama waganga.

Kuna watu wanarogwa na kuzunguka makanisani na misikitini hasa hii feki feki ya kuigiza, mtu haponi kabisa, hapo kinachobaki huwa ni kwenda kwa waganga tu.
Ukisikia hospitali wanakwambia huyo mgonjwa mrudishe nyumbani hapa imeshindikana elewa wanakwambia katumie namna "yenu".

Ukisikia unaambiwa huyo mtoto amewhindwa kukaa hapa kutulia kila siku hatumuelewi apelekwe kwa mabibi na mababu zake wakamwangalie, akili kumkichwa.

Ukisikia wewe unatakiwa urudi kwenu wakusaidie maana huku mjini mipango yako inafeli, jua unarudi kwenye asili yetu tuliyoikimbia.

Dunia hii ina asili na misingi yake, haitakaa ibadilike. Asili iko pale pale
 
Dini ni taasisi km taasisi zingine usijisahaulishe ndio maana huwezi kuanzisha kanisa km huna vibali, kwa hio kaa mkao wa kutoa Sadaka na kuchangia ujenzi wa kanisa hayo mengine waachie wenyewe

Mwamba

Ulichoandika ni "misuse" ya Dini.

Ukipata wasaa, hebu tafiti kidogo kuhusu nadharia ya kuabudu humu Duniani. Tafiti kuhusu historia ya uumbaji (kuna theories 3); theories za kuabudu (Mungu mmoja Vs miungu wengi); faida na hasara za kuabudu Mungu mmoja Vs miungu wengi.

Ukipata data zaidi ujazie habari za Yesu Kristo, mwamba aliyelazimisha Dunia ianze kuhesabu kalenda upyaaaàaa.

Hapa nidokeze kidogo. Waisrael walitarajia Messiah Mfalme. Aje na jeshi atawale Dunia kibabe. Messiah Yesu alitokea kinyonge. Matendo aliyotenda yote yalikuwa yanatimiliza unabii wa manabii watangulizi e.g. Isaah 53.

Waisrael wakaona aah, huyu jamaa mbona ni kama Messiah? Kwa vile ilishaandikwa kwamba Messiah atakufa na kufufuka, ndio wakampa kesi wamuue, waone kama atafufuka. Yesu akafa na akafufuka kweli kama ilivyoandikwa. Wakapigwa butwaa.

Baadhi ya Waisrael waliamini baada ya kufufuka. Baadhi bado hawaamini
kiasi kwamba Hilo andiko la Isaah 53 hawalitambui maana liliandikwa 700 yrs before Yesu kuzaliwa.

Well, nisikuchoshe.

Nikushauri Tu, ukipata wasaa Fanya utafiti kuhusu concept nilizoainisha hapo juu.

Best wishes 👍🏾
 
Baadhi ya Waisrael waliamini baada ya kufufuka. Baadhi bado hawaamini
kiasi kwamba Hilo andiko la Isaah 53 hawalitambui maana liliandikwa 700 yrs before Yesu kuzaliwa.
Mkuu hukunielewa nilichokiandika, Dini uanzilishi wake na muendelezo wake sio tatizo nakumbuka kipindi cha miaka ya 90 wachungaji walikua wanakuja mitaani na pazia jeupe na projector kuja kuonyesha picha ya Yesu watoto wakimaliza kucheza mpira uwanjani picha ya Yesu unawekwa wanaangalia picha ya Yesu (video) baada ya hapo mchungaji anahubiri kidogo anaenda zake, kesho hivyo hivyo na ilikua bure bila malipo Wala sadaka Wala kiingilio

Siku hizi my brother umekua tofauti, umenipeleka Israel mimi nimekuleta bongo hapa kwenye uhalisia wenyewe dini ni zaidi ya taasisi ingawa wana msamaha wa Kodi Ila ni taasisi vibari vyote walivyopewa na serikali wanavilipia na kanisa likienda kinyume na Serikali linapigwa kufuli lisiendeshe ibada refer Seguye wa MVR amepigwa komeo asiendeshe ibada, refer Kakobe alishawahi kupigwa komeo na Serikali asiendeshe ibada

Nadhani utakua ushanielewa nilimaanisha nini ninaposema Dini ni Taasisi ndio maana kanisa la Kakobe lina hadi Bendera yake,

Wewe andaa sadaka nenda kanisani ukachangie maendeleo ya ujenzi wa kanisa lako, Waisrael pamoja na kwamba hadi leo wanaitumia Bible ila wanatambua Agano la Kale tu na Agano Jipya hawalitambui hio unamaanisha kwamba Waisrael hawamtambui Yesu Mesiah unaemtambua wewe km mwokozi na mkombozi wa ulimwengu wao wanamngoja Mesiah wao wanaomjua wao, acha niishie hapa mkuu
 
Okay

Ok

Nimeona tupo kwenye ukurasa unaofanana.

Religion misuse na mgongano wa Imani (faith crisis) ndio Dunia imefika kuelekea ujio wa pili wa Emmanuel.

Nikutakie heri
 
Ndiyo asili ya Waafrka wengi, huwezi kumtoa mtu asili yake kirahisi rahisi.

Watu kibao nimewaona na chale za kwenye matambiko, niliwahi kuifanya kazi fulani iliyoweza kunipa access ya kuwaperuzi wanaume kwa wanawake wakiwa vifua wazi, ysani ni wengi tu wanazo chale za matambiko ama waganga.

Kuna watu wanarogwa na kuzunguka makanisani na misikitini hasa hii feki feki ya kuigiza, mtu haponi kabisa, hapo kinachobaki huwa ni kwenda kwa waganga tu.
Kuna mchizi wangu mmoja alinipa story, kwao walikuwa na ndinga kadhaa, sasa ndinga ya dada yake ikaharibika.

Mchizi kwa ubarubaru wa kaka mkubwa akaamua kumpa ndinga yake dada yake, yeye akaenda kuitengeneza ile ndinga ya dada yake.

Sasa baada ya siku chache akamaliza ile kazi. Akachujua ndinga yake. Akawa karudi chuoni kwao.

Kufika chuoni, machizi wake wakambana.

Bwana tabia za kwenda kwa waganga wa kienyeji umeanza lini?

Jamaa akawa anawashangaa. Kwa waganga wa kienyeji nimeenda wapi, lini?

Machizi wakamwambia tumeiina gari yako ime park kwa mganga wa kienjeji Kinondoni.

Jamaa akaukiza lini?

Akatajiwa siku.

Kuja kucheki, hiyo siku ndiyo ioe siku aliyomoa dada yake gari.

Sister du boomba, mtoto wa mjini, kasoma, kwao friji open, ila bado anazunguka kwa waganga wa kienyeji.

Jamaa aliona aibu sana kwamba dada yake anakwenda kwa waganga wa kienyeji.
 
Okay

Ok

Nimeona tupo kwenye ukurasa unaofanana.

Religion misuse na mgongano wa Imani (faith crisis) ndio Dunia imefika kuelekea ujio wa pili wa Emmanuel.

Nikutakie heri
Amen mkuu 🙏 bless bless
 
Back
Top Bottom