Watanzania wengi ni wajinga sana.

Safi sana mkuu God bless you.
Asante sana
Watoto lazima hata wakienda kwa jirani au Ndugu wajue mipaka yao
Sio toto linasumbua watu mpaka kero
Tuwalee Watoto kwa maadili hata mimi nimepitia huko
Eti upite kikombe bila kukiondoa utakula kofi enzi hizo
 
umendika kwa hisia kama Mbaga Jr
 
Kariakoo , msasani sio ushuan.
Osterbay , Upanga na Mbezi beach ya wap inayonuka?.

Hasa hasa nitajie eneo la Osterbay maana mm nafanya kaz osterbay.
Mkuu mimi nimeishi Oysterbay miaka 2 na sio Osterbay unayo isema wewe unafanya kazi.

Pia sina time yakuanza kuvutana na wewe hapa itakuwa ni kituko kama bado upo kwenye ujinga huu wakutetea Jiji la Dar es salaam kuwa ni safi.

Maeneo ya Oysterbay mengi yananuka mfano ni mitaa ya Buzwagi, Ubalozi wa Nigeria upo hapo Haile Selassie Road, Ali Hassan Mwinyi Road, Chole Road, Ghuba Road, Maeneo ya ubalozi n.k

Jiji la Dar ni la hovyo yani hata hizo sehemu prime nazo ni chafu hata ukienda oysterbay,masaki,mikocheni bado hauwezi kukosa mavifurushi ya uchafu.
 
Nimesemea culture kwa sababu.
Kuna weng hawajasoma.

hawa je?.
Ila ukiingiza hili liwe kwenye tamaduni. Basi hata mtu ambaye hajasoma ataona yuko na obligation ya kutunza na kuweka mazingira yanayomzunguka safi na salama.
Of course ndiyo maana yangu pia mkuu wewe uliyesoma inatakiwa utengeneze utamaduni mzuri katika jamii. Na jamii itaufuata tu ikielimishwa.
 
Asante sana
Watoto lazima hata wakienda kwa jirani au Ndugu wajue mipaka yao
Sio toto linasumbua watu mpaka kero
Tuwalee Watoto kwa maadili hata mimi nimepitia huko
Eti upite kikombe bila kukiondoa utakula kofi enzi hizo
Malezi ya hovyo yanachangia kwa kiasi kikubwa sana jamii kuendelea kuzama kwenye shimo la uchafu.
 
Hii ni dalili kwamba elimu ya darasani pekee haijasaidia watu wetu ndiyo maana wabunge wa Dar, Wakuu wa Wilaya za Dar, Wakurugenzi wa Manispaa, Mkurugenzi wa Jiji, Meya na Wenyeviti Jiji na Manispaa, Mkuu wa Mkoa na watendaji wengine wote hawafanyi kazi yao mpaka wasukumwe, wakumbushwe au wafokewe.
Watu wetu wana uwezo mdogo wa kufanya kazi.
Jiji linahitaji watu wabunifu kuweka na kusimamia mipango ya usafi.
Hawa tulionao kwa sasa ni mzigo kwa wakazi wa Dar es salaam waondolewe.
 
Nikweli katika hilo lakini hilo halikufanyi wewe Raia kuwa mchafu kwenye jamii yako.
Usafi ni mlolongo wa vitu vingi mkuu watu wanatupa taka hovyo unakuta mtu anaendesha gari anatupa kopo la maji alilolitumia ni juzi tu usafi wa abiria wa ma bus wameanza kuwekewa vitu vya kutupa taka ndani ya bus pamoja na vyoo watu walikua wanashuka kuchimba dawa porini vituo vya mafuta hawana vyoo vya kuweka wateja wao wakiwa wengi Usafi sio kitu kimoja ni mololongo..
Japan walipoenda WC mechi ilipoisha waliokota makopo yote ya ule Uwanja bila kujali nani katumia ile ni tabia yao wamengeka hivyo na sisi inatakiwa kwanza kuwajenga watu wapende usafi wasione ni adhabu..
 
Tena wafutwe wote wao wanajua kupokea mishahara tu kula, kutita na kulala.
 
Lini hao watu watajegwa mkuu?

Nani atawajenga hao watu?

Tuendele kuwa wachafu mpaka pale hao watu watakapo jengwa?
 
Haya yote yanasababishwa na umasikini
 
Havipo ndiyo maana nimesema Watanzania ni wajinga sana.
Sio watanzania wote... Aina ya viongozi tulionao ni kutaja jina la Rais kila pahala Rais Samia Rais Samia ...huku kumsaidia kazi hawawezi
 
Basi hujaona jukumu la manispaa au Halmashauri.

Wewe ni mwanaume? Kama sio unaweza kukagua huyu kapiga mswaki au huyu lah?

Bado huoni tatizo kwa kuruhusu watu kupanga biashara na kujenga vibanda vya uchuuzi kwenye njia za watembea kwa miguu?

Bado huoni tatizo la uholela kuanzia makazi, viwanda, ufugaji ila wewe unaona vitu petty issues.

Sishangai na wao wakiona sio jukumu lao, kama unavyoona wewe
 
Sio watanzania wote... Aina ya viongozi tulionao ni kutaja jina la Rais kila pahala Rais Samia Rais Samia ...huku kumsaidia kazi hawawezi
Ndiyo watanzania hao.

Viongozi ni Raia kama wewe wanatoka kwenye jamii unayotoka wewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…