Watanzania wengi ni waoga wamebaki kuilaumu CHADEMA

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
21,470
Reaction score
40,593
Sehemu kubwa ya watanzania ni waoga sana kwenye kupambana hadharani na CCM.

Lakini watanzania hao hao ni mafundi wabobevu kwenye kuilaumu CHADEMA.

Na watanzania wengi sana ni rahisi na wanaona ni salama kwao kushabikia propaganda za CCM dhidi ya CHADEMA kuliko kuunga mkono ukweli unaosemwa na CHADEMA dhidi ya CCM.

CCM inafanya dhuluma na hujuma lukuki dhidi ya watanzania, lakini watanzania hao hao badala ya kuiona CCM ndiyo chanzo cha matatizo yao wenyewe huishia kuilaumu CHADEMA kwa matendo mabaya wanayotendewa na CCM.

Watanzania waoga hawawezi kuitoa CCM madarakani. Na wale wenye ndoto ya kizazi kingine kije kupambana na CCM, niwaeleze tu kuwa huu uoga na uzembe wetu, tunawarithisha na watoto wetu.
 
watanzania wengi
1-wanauwezo mdogo wa kufikiri
2-wanaogopa mabadiliko
3- wamezoea shida/dhiki .maisha ya shida ndo imekua furaha yao.

proof tembelea maisha ya vijijini uone 90% ni maskini wa kutupwa.
 
Siyo tu wamezoea, bali pia wamekubali kuwa ni Mungu ndiye aliyeamua wawe hivyo. Na ndiyo maana utawasikia wakisema "kwani ukiichagua CHADEMA ndiyo itakuletea ugali mezani kwako?".
 
Sehemu kubwa ya watanzania ni waoga sana kwenye kupambana hadharani na CCM.

Lakini watanzania hao hao ni mafundi wabobevu kwenye kuilaumu CHADEMA.

Na watanzania wengi sana ni rahisi na wanaona ni salama kwao kushabikia propaganda za CCM dhidi ya CHADEMA kuliko kuunga mkono ukweli unaosemwa na CHADEMA dhidi ya CCM.

CCM inafanya dhuluma na hujuma lukuki dhidi ya watanzania, lakini watanzania hao hao badala ya kuiona CCM ndiyo chanzo cha matatizo yao wenyewe huishia kuilaumu CHADEMA kwa matendo mabaya wanayotendewa na CCM.

Watanzania waoga hawawezi kuitoa CCM madarakani. Na wale wenye ndoto ya kizazi kingine kije kupambana na CCM, niwaeleze tu kuwa huu uoga na uzembe wetu, tunawarithisha na watoto wetu.
Chadema ilitumia mkakati wa ovyo wa kutaka madaraka(ukabila na ukanda) ,nani alaumiwe?Watanzania hawako tayari kugawanywa Mkuu,badilisheni jina la chadema na pia uongozi wa chama ,hakuna namna hata kidigo wakuu.
 
watanzania wengi
1-wanauwezo mdogo wa kufikiri
2-wanaogopa mabadiliko
3- wamezoea shida/dhiki .maisha ya shida ndo imekua furaha yao.

proof tembelea maisha ya vijijini uone 90% ni maskini wa kutupwa.
Wewe ambae umekuwa tajiri ulitumia mbinu gani?wasaidie watanzania wenzako mkuu ili waweze kufikia uwezo wako mangi
 
Chadema ilitumia mkakata wa ovyo wa kutaka madaraka(ukabila na ukanda)
Unaposema ukabila na ukanda unamaanisha nini?
Watanzania hawako tayari kugawanywa Mkuu,
Kati anayesema bila ya ushahidi kuwa CHADEMA ni chama Cha ukanda na ukabila na wanachadema wenyewe ni nani anayetaka watanzania wagawanyike?
badilisheni jina la chadema na pia uongozi wa chama ,hakuna namna hata kidigo wakuu.
Jina la CHADEMA linahusiana vipi na CCM kuongoza nchi hovyohovyo?
 
Sidhani kama watu wanailaum CHADEMA kwa madhila ya CCM,Kutokana na ukweli kwamba ndo chama kikubwa cha Upinzani Tanzania ilitegemewa kiwe kimbilio la watu. Kinalaumiwa kwa kushindwa kuwa chama mbadala wa CCM kilichobeba sura ya kitaifa .CHADEMA inabaki kuwa mali ya watu wa kaskazini.
 
Unaposema ukabila na ukanda unamaanisha nini?

Kati anayesema bila ya ushahidi kuwa CHADEMA ni chama Cha ukanda na ukabila na wanachadema wenyewe ni nani anayetaka watanzania wagawanyike?

Jina la CHADEMA linahusiana vipi na CCM kuongoza nchi hovyohovyo?
Huitaji akili kubwa kuona yanatokea chadema ,hiki chama kinao wasemaji wakuu ambao ni ;Lema,Mrema na Mzee Mbowe ,hapo bado unaona kuwa ni sawa ?
 
Hebu thibitisha hii hoja kuwa CHADEMA ni chama Cha watu wa Kaskazini.

70% ya viongozi wa CCM Taifa ni waislamu. Hiyo inaifanya CCM kuwa chama Cha waislamu?
Mangi kwa hiyo Chadema mmelipiza kwa kuweka wachagga watupu kwa misingi ya kwamba viongozi wa ccm wengi ni waislam?🙆‍♂️🙆‍♂️🙆‍♂️
 
Unaposema ukabila na ukanda unamaanisha nini?

Kati anayesema bila ya ushahidi kuwa CHADEMA ni chama Cha ukanda na ukabila na wanachadema wenyewe ni nani anayetaka watanzania wagawanyike?

Jina la CHADEMA linahusiana vipi na CCM kuongoza nchi hovyohovyo?
Leo
Ni upuuzi kujitoa kwenye kundi la waoga ilihali wewe ni mmoja wapo!
Anshangazi kweli kweli ,siku ya maandamano hatukumwona aisee
 
Sehemu kubwa ya watanzania ni waoga sana kwenye kupambana hadharani na CCM.

Lakini watanzania hao hao ni mafundi wabobevu kwenye kuilaumu CHADEMA.

Na watanzania wengi sana ni rahisi na wanaona ni salama kwao kushabikia propaganda za CCM dhidi ya CHADEMA kuliko kuunga mkono ukweli unaosemwa na CHADEMA dhidi ya CCM.

CCM inafanya dhuluma na hujuma lukuki dhidi ya watanzania, lakini watanzania hao hao badala ya kuiona CCM ndiyo chanzo cha matatizo yao wenyewe huishia kuilaumu CHADEMA kwa matendo mabaya wanayotendewa na CCM.

Watanzania waoga hawawezi kuitoa CCM madarakani. Na wale wenye ndoto ya kizazi kingine kije kupambana na CCM, niwaeleze tu kuwa huu uoga na uzembe wetu, tunawarithisha na watoto wetu.
Kuna jamaa mmoja wa Njombe anaitwa Inocent Mushi, yeye huwa anajikuta ni mzee wa Neutral. Na hiyo ni sample ya watz wengi wakiwa wanakwepa uwajibikaji wanajifanya wapo neutral.
 
Back
Top Bottom