Watanzania wengi ni waoga wamebaki kuilaumu CHADEMA

Kuna jamaa mmoja wa Njombe anaitwa Inocent Mushi, yeye huwa anajikuta ni mzee wa Neutral. Na hiyo ni sample ya watz wengi wakiwa wanakwepa uwajibikaji wanajifanya wapo neutral.
Ogopa sana ukikutana na mtanzania anakwambia kwamba yeye hana chama, hiyo ni dalili kuwa anaiogopa CCM.
 
Hebu thibitisha hii hoja kuwa CHADEMA ni chama Cha watu wa Kaskazini.

70% ya viongozi wa CCM Taifa ni waislamu. Hiyo inaifanya CCM kuwa chama Cha waislamu?
Usiumize kichwa kubishana wavaa vinjunga mkuu. Hawa hawajui hata maana ya political base. Muulize tanga mkoa mzima una madiwani wangapi wa upinzani??
 
Chadema ilitumia mkakata wa ovyo wa kutaka madaraka(ukabila na ukanda) ,nani alaumiwe?Watanzania hawako tayari kugawanywa Mkuu,badilisheni jina la chadema na pia uongozi wa chama ,hakuna namna hata kidigo wakuu.
Unaweza kueleza bila kuacha shaka yoyote kwa nature ya Tanzania na it's ethnic diversity ni namna Gani Chadema ilitumia mkakati wa ukabila kutaka madaraka?

Hii nadhani ni propaganda au nadharia iliyotumiwa na CCM kuwagawa watanzania kwa kuhubiri kwamba chama kinataka kutwaa madaraka kwa kutumia mkakati wa ukabila au ukanda!

Nasema ni propaganda ambayo unakosa technical proof kutokana na statement Yako ya mwisho ya kuzungumzia uongozi! Kwamba uongozi umeshikiliwa na Wachaga kitu ambacho sio kweli!

Ukiangalia top form ya viongozi sio kwamba Iko dominated na Wachaga. Tuna watu kama akina mashinji, Mwalimu, lissu mnyika, sugu msigwa sakaya.

Kwa mantiki hiyo agenda ya ukabila ilishanirishwa na swala la serikali za majimbo inakosa nguvu Kwa sababu ya mtawanyiko wa watu! Tanzania Ina mwingiliano mkubwa wa watu kwahiyo Haina mashiko!
 
Sema Ile hama hama ya kiongozi wa upizani kwenda CCM na badae ukubali nafasi mbalimbali za uongozi walizopewa, kumechangia Kwa sehemu kubwa watu kuwa disappointed na hawa ambao walio jaribu kuaminisha watu kuwa CCM ni mbaya .Hii imeiosha kwamba viongozi wa upizani wapo pale Kwa maslahi binafsi na sio kama wanavyojaribu kuaninisha wananchi.
 
Hebu thibitisha hii hoja kuwa CHADEMA ni chama Cha watu wa Kaskazini.

70% ya viongozi wa CCM Taifa ni waislamu. Hiyo inaifanya CCM kuwa chama Cha waislamu?
Utabisha ila hilo liko wazi,miaka nenda rudi mwenyekiti ni Mbowe baada ya ba mkwe wake.CCM unaweza observe hvyo leo,lakini miaka 5 iliyopita viongozi asilimi 70% walikuwa wakristo si ajabu miaka mitano ijayo pia ikabadilika.Utatumia nguvu nyingi hila kwenye hilo CHADEMA imefeli period.
 
Kipindi cha magufuli wengi walilazimishwa haikua hiyari yao
 
Chadema imefeli wapi huku nchi inazaidi ya miaka 60+ Inaongozwa na ccm na bado iko kwenye umaskini wa kutupa
Watanzania kama wewe hamshindwi kusema nchi hii ni maskini kwa sababu ya chadema
 
Nani anapaswa kukifanya kiwe na uwezo wa kuitoa CCM madarakani?
 
Utabisha ila hilo liko wazi,miaka nenda rudi mwenyekiti ni Mbowe baada ya ba mkwe wake.
Mbowe kapokea uenyekiti toka kwa msukuma Hayati Mzee Bob Nyange Makani ambaye pia alikuwa ni Muislamu.

Mambo ya kukaririshwa na CCM uongo halafu ndiyo uufanye ni uhalisia, yatakuja kukuaibisha siku moja.

CCM watu wa ajabu Sana. Mlikuwa mnasema CUF ni chama cha waislam kisa viongozi wake wengi walitoka Zanzibar.

Mkazusha mpaka kusema eti CUF ikishinda Zanzibar itageuka kuwa paradiso ya waislamu wenye siasa Kali. Na alieandika hayo kwenye Jarida la The Hill la Marekani ni aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wenu Taifa na ambaye ni muislamu, Abdulrahman Kinana.

Kumbe kwa CCM linapokuja suala la kuzusha hata wale usiowatarajia huzusha. Hivi huko Kaskazini hakuna CCM? Mbona tangu kuanzishwa kwake CHADEMA haijawahi kushinda kwenye Kanda ya Kaskazini hata Kwa asilimia 50 tu?
 
Watanzania wengi ni wajinga na huo ni mtaji wa ccm
 
Sema Ile hama hama ya kiongozi wa upizani kwenda CCM na badae ukubali nafasi mbalimbali za uongozi walizopewa, kumechangia Kwa sehemu kubwa watu kuwa disappointed na hawa ambao walio jaribu kuaminisha watu kuwa CCM ni mbaya .
Hivi Kwa nini wasilaumiwe CCM wanaotuhumiwa kutumia Dola kuwatisha wapinzani na kutuhumiwa kutumia hela za umma kuwashawishi watu kwa rushwa kuhamia CCM?
 
hawailaumu chadema bana gentleman,

wanaidharau sana na kuishangaa kwa jinsi inavyojikaanga na kujivuruga yenyewe kwa yeyewe kwa vita vya maneno miongoni mwa waandamizi wake πŸ’
 
hawailaumu chadema bana gentleman,

wanaidharau sana na kuishangaa kwa jinsi inavyojikaanga na kujivuruga yenyewe kwa yeyewe kwa vita vya maneno miongoni mwa waandamizi wake πŸ’
Fomu ya Urais CCM mtatoa moja au vipi? Maana nyie ni waoga sana wa uchaguzi hata wa ndani ya chama chenuπŸ˜†πŸ˜ƒπŸ˜€
 
Fomu ya Urais CCM mtatoa moja au vipi? Maana nyie ni waoga sana wa uchaguzi hata wa ndani ya chama chenuπŸ˜†πŸ˜ƒπŸ˜€
Gentleman?
umeahamishia hoja CCM tena 🀣

mbona ghafla sana na hatujahitimisha hoja ya msingi?🀣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…