kwakweli huu ndio ukweli mchungu, asilimia kubwa sisi ni wezi na kila mmoja huiba kwa nafasi yake,
mimi nimefanya hata kazi kwenye mashirika ya kimataifa wenye vyeo vya juu kule ni watu wa kenya, uganda, zimbabwe na nchi zingine vyeo vya chini wamewapa watanzania wanaogopa kuwapa vyeo vya juu wataiba,
nimefanya kazi mashirika ya wakimbizi kambi za kigoma kwenye yale mashirika wanaogopa kuwapa vyeo watanzania wakiwatilia mashaka asiyeamini akaangalie mashirika yote yaliyopo kwenye kambi za wakimbizi watanzania wana nafasi gani,
Nimepata kuishi kwenye wilaya flani walikua wanajenga barabara kwa kiwango cha Rami, ndugu zangu watanzania walineemeka kwa wizi wa cement, nondo, mafuta na kokoto, wizi ulikua mkubwa sana watu walijenga mijengo kwaajili ya wizi mpaka mchina alinyoosha mikono, ulikua hata ukiitaji cement ya elfu tano unapata
maofisini kwetu ndio kabisaaa haina haja ya kuuliza, ilifika hadi hatua madereva wa halimashauri wanaenda kupiga nyoka mafuta ya serikali yananyonywa vichochoroni tubadilike tuache wizi,
hebu angalia hii video hapo chini hao Raia nao wana uhalali gani wa kuhoji serikali ilihali nao ni wezi?
Wizi umeanzia serikalini. Sisi vibaka wadogo wadogo tumejifunza kutoka huko juu. Kama rais ni mwizi, waziri mwizi, mbunge mwizi, unategemea nini kifanyike?
mimi nimefanya hata kazi kwenye mashirika ya kimataifa wenye vyeo vya juu kule ni watu wa kenya, uganda, zimbabwe na nchi zingine vyeo vya chini wamewapa watanzania wanaogopa kuwapa vyeo vya juu wataiba,
kuna shirika flani linaitwa la msalaba mwekundu lilinaendeshwa na watanzania 100% lilipewa kazi ya kusimamia mambo ya afya kwenye kambi za wakimbizi likawa liko funded na mashirika ya nje UNHCR, UN, NK wao ikawa kila mwaka hesabu zao ni loss wakat mashirika mengine hayana loss, mpaka masponsor wakajitoa, shirika likaanza kua linawalipa mishahara wafanyakazi wake kwa kusua sua hadi inapita miez miwili kapa,
hapo ndo nilijua mtanzania haaminiki
Kweli kabisa mkuu, WIZI na UBABAISHAJI.
Haya mambo mawili yatatusumbua sana kwa muda mrefu tusipojirekebisha na kubadilika.
Cha ajabu pia ni kwamba wezi ndiyo tunawaona mashujaa kwenye jimii yetu!
..... na nchi hii, mtu akipata nafasi ya juu anawaza kuiba tu.
... wananchi nao wanashabikia wizi tu.
... usipoiba Ukiwa na nafasi, wanakushangaa sana.
..... utasikia, fulani alikuwa na nafasi fulani ya juu, ona anavyoishi kimasikini, wanadiriki kusema ni maskini kutokana na ujinga wake.
....wizi, wizi, wizi, wizi kila mahali.
..... na nchi hii, mtu akipata nafasi ya juu anawaza kuiba tu.
... wananchi nao wanashabikia wizi tu.
... usipoiba Ukiwa na nafasi, wanakushangaa sana.
..... utasikia, fulani alikuwa na nafasi fulani ya juu, ona anavyoishi kimasikini, wanadiriki kusema ni maskini kutokana na ujinga wake.
....wizi, wizi, wizi, wizi kila mahali.
Pia mishahara inatofautiana Sana. Kulikuwa FM mtanzania alkuwa akilipwa 1.5 m akaajirwa mhindi akawa analipwa $3000 na tsh 400000 Kama allowance. Ukimlipa hiyo hela mtz ataiibia kweli hiyo kampuni?
Nadhani Wana wasiwasi na uwezo wetu vichwani