Watanzania wengi ni wezi, hatuna uhalali wa kuihoji Serikali

Pia mishahara inatofautiana Sana. Kulikuwa FM mtanzania alkuwa akilipwa 1.5 m akaajirwa mhindi akawa analipwa $3000 na tsh 400000 Kama allowance. Ukimlipa hiyo hela mtz ataiibia kweli hiyo kampuni?
Nadhani Wana wasiwasi na uwezo wetu vichwani
mafisadi ya sisiemu yalikua yanalipwa hela nyingi tu ila yalikua bado yanaiba
 
Watanzania waaminifu ni wachache sana wengi ni waizi Ila hawajapata nafasi
 
Hii ni mindset iliyojengeka kwenye kizazi,kwahiyo ukitaka kuondokana na hii hali inabidi ipite miaka kama 30 ya kubanana ili watu warudi tena kwenye mstari,imefikia mahali usipokuwa mwizi unaonekana mshamba,na hii sio kwa jamii tu ya mtaani,ni mpaka kwenye familia unayotoka...
 
Tanzania sio wezi ni vibaka, maana hatujafikia international level.
 
+Ubabaishaji mwingi na maneno zaidi ya yale ya kwenye kanga.
 
True kama watawala ni wezi Kwann watawaliwa wasiwe wezi.
 
Mtawala anaiba kodi ya watawaliwa anaficha ulaya,baba anaiba kazini analeta nyumbani mama nae anamuibia baba anawalisha viporo watoto hali baba kaacha pesa kisha anatuma kwao, dada wa Kazi nae anaiba Vyakula au chochote anauza kwa jirani Ili apate ziada atume kwao.Wizi upo toka juu hadi chini.
 
Unakuta mtu akipewa kazi labda ya udereva wa Lori,anaambiwa na wenzake "Ushindwe kujenga tu! Hapo wana maanisha amuibie tajiri,

Fisadi anayeendesha Gari la kifahari anasifiwa ila muungwana anayepanda Daladala na mwenye maadili mema na kutokua na tabia ya wizi anadharaulika!

Wizi ni tabia,na solution ya hii tabia inatakiwa ianzie kwenye malezi kuanzia utotoni,kumbadili mtu mzima kuacha wizi sio kazi rahisi.
 

Kwahiyo hata wazazi wako pia ni wezi?
 
Mara ya mwisho tutakuja tuiibe na Tanzania yetu kabisa! Sijui tutaishi wapi tukishaiiba 😁
 
Sasa serikali ni nani kama sio haohao watanzania.
 
Ni kweli kabisa na hiyo inadhihirka pale wanapopandishiwa bei za vitu kama mafuta, mbolea, sukari, tozo mbalimbali kama za miamala, majengo, watanzania hutawaona wakilalamika kwa uwazi (maandamano) ili kuonesha mshikamano ya kuwa wanaumia. Kila mtu anatazama maisha yake, kama ana njia kama hizo za wizi, haoni maana ya kulalamika.
 
πŸ˜€πŸ˜€
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…