Watanzania wengi sio watanashati

ntuchake

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2024
Posts
408
Reaction score
1,549
Watanzania wengi hawana utanashati. Wengi wao wanavaa nguo bila kunyoosha pasi. Nguo inatolewa kwenye kamba inavaliwa ivo ivo unakuta mtu anavaa nguo imejikunja mpaka unajiuliza huyu nyumbani kwake ata kioo hana hakujiangalia wakati anatoka?

Nguo utfikiri imetoka kwenye tumbo la ng'ombe! Watanzania kueni wasafi nyoosheni nguo pasi mweh mnatia aibu.

Afu tabia ya kujipulizia pafyumu zenu za mia mia muache mnatuumiza pua.
 
Hilo ni kweli mkuu, mpaka imefikia hatua ukivaa kitanashati watu wanahisi upo kikazi
 
Usafi ni kufua, kupiga pasi mwembwe tu.

Watu maskini ndio wenye muda wa hayo makorombwezo ya kunyoosha.

Tajiri hana hizo time
 
Ndege wafananao huruka pamoja, upo kundi hilo hilo la maskini
 
Acha utoto.
 
Waambie wapambanie katiba mpya na tume huru
 
Huo muda hatuna babu, tuwaze pesa au utanashati?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…