Watanzania wengi tuna uraibu wa kukopa

Hela za mkopo Zina hatari Sana, sio za kuchezea zile
 
Weye naye akili zako utadhani umezikalia.Sasa,nini kinachokushangaza masikini kukopa?
 
Bro Kuna ubaya kukopa ili usome,au ujenge nyumba au Kununua usafiri.
Shida Ni malengo unakopa ya Kazi gani ,Mimi naamini nyumba ni asset,kusoma Ni asset na ATA biashara ikiferi pia itakuwa umepata elimu Namna Bora ya kuendesha biashara,sema ukiwa hujachukua mkopo unakuwa na Akili nyingi sana na ukishakopa pesa IPO Akili zinaisha na unakuwa Kazi yako kutembea na ATMCARD Ni rahisi kupoteza malengo.
Kuna msemo kwamba pesa ya mkopo inaitaji kabla hujaenda kuitoa uwe umeshapanga rout kutokana na maitaji yako kabla ya mkopo.
Ukikopa Kununua tv itaungua,redio itaungua,sofa zitaliwa na Panya na kuisha,gari itaitaji mafuta,Ila nyumba itakuifadhi.
 
Hakuna ulichogundua Bali Kuna watafiti walisema hivyo mapema wiki hii na wakopajo wengi wanakopa kujikimu basic needs
 
Kwa kiswahili Assets na liabilities msaada
 
Tanzania hakuna wakopaji bhana nchi za wenzetu huko mtu anafanya kazi kila kitu amekopa kabla nyumba gari vitu vya ndani.

Ni hatari.

Hapa bongo hatuna utaratibu mzuri wa watu kukopa ila kungekuwa na utaratibu wa kurleweka tungekopa sana.
 
Kukopa ni kawaida tu
Sema serikali yetu haiwajali wananchi kwa kuweka utaratibu mzuri wa kukopa
Wananchi wenyewe no defaulters wazuri ndo maana riba imewekwa kubwa kufidia
 
Kuna taasisi Fulani inakopesha inaitwa OYA microcredit....wanatembelea vi IST. Wanadai haooo. Yaani ukichelewesha rejesho, vinaongozana vigari hata sita kuja kukudai mtu mmoja
Nimeiona mara kibao Tegeta
 
Tatizo si kukopa,ila mfumo wa kibepari uliopo kwenye hiyo mikopo.Riba, retention fee,bima and processing charge. Huu mfumo umekua chanzo Cha kuendeleza umaskini kuliko kumkwamua mkopaji. Serikali inapaswa kuweka utaratibu sawia kwa Kila taasisi kuhusu mikopo. Mf.Benk zetu riba ni 16%-17%. Kwenye biashara halali yaani mtu asikwepe Kodi yeyote hawezi kurejesha na apate faida zaidi ya benk. Hivyo kama riba ingekua 3%-4%. Mikopo ingesha tajirisha watu wengi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…