Watanzania wengi wana tatizo la uelewa na ufahamu (upeo mdogo). Hii inawapa mwanya wajanja kuwatapeli kirahisi

Watanzania wengi wana tatizo la uelewa na ufahamu (upeo mdogo). Hii inawapa mwanya wajanja kuwatapeli kirahisi

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
WATANZANIA WENGI WANATATIZO LA UELEWA NA UFAHAMU(UPEO MDOGO). HII INAWAPA MWANYA WAJANJA KUWATAPELI KIRAHISI.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

Hakuna Jambo rahisi kama kuwapotosha Watañzania waliowengi. Yàani katika Jambo rahisi Kabisa unaloweza ukalifanya kwèñye nchi ya Tanzania basi kuwapotosha Watu Kwa sababu watanzania wengi na Wala siô wôte upeo waô WA ufahamu na uelewa upo chini Kabisa. Na ili uubust inahitajika Ñguvu ya ziada.

Nitaeleza màtukio kadhaa yanayothibitisha ufinyu wa upeo mdogo wa Watañzania wengi;

1. Mama wa Kigoma kuzaa Kuku aliyekufa.
Tukio hili lilitokea Mwaka Jana mwishoni. Tukio hili Kwa Mtu mwenye Akili ya kawaidà Moja Kwa Moja atajua ni njama, hila, uongo au drama. Lakini Huwezi Kuamini watanzania wengi waliamini kuwa Mtu anaweza kuzaa Kuku, tenà kuku aliyekufa.

NI Watu wajinga pekee au weñye Akili ndogo wanaoweza kukubali hadithi hiyo.

2. Tukio la kiroba cha mahindi kunata kwèñye mgongo wa Kijana Mwizi.
Tukio hili lilitokea 2019 Huko Kibaha. Tukio lile niliwabishia Watu kuwa Ile NI drama,wakabisha. Sisi watunzi wa simulizi, drama na scene ya filamu tunaelewa mambo ya maigizo na propaganda. Tunajua Ipi NI Stori ya kweli na Ipi NI fiction stories.

Watu waliamini Ile hadithi ya uongo lakini Kwa Bahati mbaya au nzuri wiki Moja baadaye Yule kijana alikuja kusema UKWELI kuwa ule ulikuwa mchongo waliouchonga. Lakini baàda ya kutolipwa Pesa ya onyesho Hilo akaona aseme UKWELI. Màtukio hayo huchezwa na waganga ili kuaminiwa. Lakini pia huchezwa na Watu Fulani kwèñye Mtaa ili kuwatisha wezi na maadui zào wasijaribu kuiba kwèñye Nyumba zào.

3. Tukio la kuanguka Mchawi juu ya Nyumba ya Mchungaji Huko Iringa Mwaka Juzi, 2022 mwanzoni.
Tukio lile pia wàpo tuliobisha na kusema lile tukio NI uongo àmbao hata Mtoto wàngu Yule WA darasa la Kwanza Huwezi kumdanganya. Lakini Huwezi Kuamini kûna maelfuna maelfu ya watañzania walisadiki na ikawa ni case study.

4. Tukio la Babu wa Loliondo.
Hili tukio ndîo lilikuwa kûbwa zaidi na àmbalo lilihusisha Mpaka Watu wakubwa. Tukio hili lilitokea 2008.
Watu wengi walibisha lakini walionekana wajinga lakini Leo hii ukweli upo wazi. Watanzani wengi Wanatatizo la Kuamini amini hovyo na hiyo NI dalili ya upeo mdogo. MTU mwenye upeo mdogo kama Mtoto NI rahisi Kuamini amini hovyo na kurubuniwa.

MTU dio Daktari, Hana Elimu ya udaktari, anakuambiaje Dawa ya ukimwi, au Corona au Malaria, au Saratani NI hii na wéwe unakubali.

Kûna kijana mmoja alikuja kijiweni akiwa na Dawa, alikuwa anauza Dawa za kwèñye vichupa, akawa anainadi Dawa inayotibu Kisukari, alafu hiyohiyo Shinikizo la damu, alafu hiyohiyo CD4.
Nikamuuliza embu elezea Kwa ufupi shinikizo la damu ni nini na hatua za shinikizo la damu? kijana chali.

5. Uwèpo wa Manabii na Mitume wa UPAKO.
Ni ngumu Kwa Watu weñye upeo Mkubwa kuwa wafuasi wa Mitume na Manabii wa UPAKO.
Ukimwona Mtu mwenye Akili NI mfuasi WA Nabii au Mtume WA UPAKO Jua naye anamgao wake au kûna biashara anaifanya. Yàani hawezi kuwa Mhanga Bali yeye pia ni sehemu ya wanaowapiga weñye upeo wa chini.

Nabii tuu wa kwèli lazima apate challenge akiwa mbele ya Watu weñye Akili. Nakumbuka Yesu mwenyewe alichalenjiwa alipokutana na tabaka tawala yàani tabaka la juu. Kuwa Afanye muujiza wowote ili Kupima huduma yake. Moja ya vitu vilivyosababisha asulubiwe NI kitendo cha yeye kushindwa kuthibitisha huduma yake kiliongeza Mashaka ya watawala na weñye Akili katika Baraza.

Nabii Musa alithibitisha Unabii wake mbele ya Farao na weñye Akili WA Misri. Eliya naye vivyohivyo. Akili huhusisha uthibitisho yàani kitu chenye mantiki na sio Kutumia IMANI. Akili ndîo inajenga Imani na ísiwe kinyume chake. Lakini weñye upeo mdogo hutumia Imani kujenga Àkili.

Akili huhusisha milango ya fahamu inayotawaliwa na ubongo. Imani Huja Kwa kuona na kusikia, lakini Taikon naongeza hili, Imani Huja Kwa Kusikia, kunusa, kugusa, kuona na kuhisi Kwa kutumia ngozi Kisha kutafakari, kuchambua na kuchanganua Kwa kutumia ufahamu.

Kusikia pekee haijengi Imani. Kusikia pia inahitaji uthibitisho, kuona tuu haijengi Imani, kuona pia inahitaji uthibitisho. Uthibitisho tunamaanisha Uhakiki, uhariri, ukaguzi, uhakikisho.

Unaweza ukaona Jambo lakini siô vile ulionavyo, ndîo maana Imani haiishii kuona tuu Bali kuhakikisha Kile ulichokiona NI kweli kipô kama unavyokiona, Kile unachokinusa au kugusa, au kûsikia lazima ukithibitishe, uhakikishe Je NI halisi au kûna hila, njama, janjajanja imefanyika kukupumbaza?

Maandiko yanasema, Msiamini kîla Roho Bali zichunguzeni Roho hizô. Pia lipo àndiko kusema, yachunguzeni maandiko.

Taikon nakupa hatua za Kuamini yàani kuwa na Imani;
1. Kupata tàarifa Kwa kutumia milango ya ufahamu, yàani kuona, kusikia, kuonja, kuhisi, na kunusa.

2. Kutafakari
3. Kufanya uchunguzi, kupeleleza, kuhakikisha, kuthibitisha, kukagua.
4. Kuijenga Imani.

Upelelezi au uchunguzi, au ukaguzi NI sehemu kuu ya Imani au Kuamini.
Imani inahusu Akili. Yàani Imani inategemea zaidi Akili Kwa sababu msingi wa Imani NI AKILI/Ufahamu.

Ukisikia Watu wanamila potofu au Imani potofu lazima ujue kuwa kûna hatua àmbayo imerukwa katika kufikia hatua ya Watu au jamii Kuamini kuhusu Jambo au Mila Fulani. Hatua àmbayo jamii nyingi zenye Mila potofu hurukwa NI hatua ya Uchunguzi au kufanya upelelezi kuhusu Jambo Fulani.

Uvivu, uzembe na upeo mdogo WA ufahamu au kufikiri NI Moja ya mambo yanayochangia Watu Kuamini Vitu visivyo KWELI.

Na Kuamini Jambo ambalo siô kwèli ndîo tunaita upeo mdogo wa Kufikiri, uzembe au uvivu WA kutoshughulisha ubongo.

Hii inaenda sambamba na suala zima la utapeli katika biashara. Mtu anayetaka kukutapeli atahakikisha anakuaminisha kuhusu Jambo Fulani lakini katika hatua za Kuamini kûna hatua Moja muhimu atahakikisha unairuka ili akupige vizuri. Hatua hiyo NI uchunguzi na upelelezi.

Kumbuka Upelelezi na uchunguzi unahitaji mambo yafuatayo muhimu;
1. Tatizo au habari unayoipeleleza.
2. Tàarifa za msingi kuhusu tatizo au habari Husika.
3. Muda wa kutosha kufanya upelelezi
4. Ujuzi na umahiri katika kufanya upelelezi
5. Kujua sehemu zote muhimu na Watu utakaofanyia upelelezi. Vyanzo vya uhakika.
5. Kufanya uchanganuzi na tathmini ya Uchunguzi baàda ya kufanya
6. Kuhitimisha.

Matapeli watakunyima Muda wakutosha kufanya uchunguzi au upelelezi. Matapeli watakupa na kukuelekeza vyanzo vyao àmbavyo utaenda Huko kufanya upelelezi yàani wataseti mfumo au mazîngira ya wewe kwenda kumuuliza Nyani habari za ngedere. Mwishowe utaingia kwèñye mfumo.

Matapeli pia huwa wajanja, wakikuona unaupeo Mkubwa na siô rahisi kukuibia. Wanaweza kuwatumia Watu wako wakaribu weñye upeo mdogo kukuchukulia Pesa zako au kukulaghai.

Nakupa Mfano halisi ulionitokea Mimi mwenyewe;

Ninaofisi ya uandishi na uchapaji wa vitabu vyangu binafsi àmbavyo nauza hardcopy na Softcopy. Lakini ofisi hii Wakati mwingine naitumia kuandika Makala kama wengi mnavyozisoma mitañdaoni. So Muda mwingi Nipo mitañdaoni.

NI kawaida kupigiwa Simu, Kwa shughuli mbalimbali kuhusu huduma ninazofanya. Na napata Pesa za kuendesha Maisha yàngu binafsi na familia. Asilimia 99% ya wateja wàngu hatujawahi kukutana uso Kwa uso. Kwani biashara NI mtandaoni.

Sasa Siku Moja mteja mmoja akanipigia Simu, akanisalimu Kwa majina yàngu, Kwa sababu Majina yàngu Yapo Public. Kisha akaniambia anahitaji Kitabu cha WAKALA WA SIRI na Kitabu cha MLANGO NAMBA 77 "DOOR 77" Nikamwambia bei Kwa vyote NI Tsh 30,000/= akaniambia Sawa. Nikamwambia anakuja kuchukua au nimfanyie delivery, akaniambia nimfanyie delivery, nikamwambia delivery utalipia wewe. Akasema siô Case.

Akaniambia Tafuta Boda aje Hapa Magomeni Karibu na kanisa la wasabato. Nikamwambia napajua. Nikatafuta Boda wakaongea, wakapatana elfu Tano. Mimi nikampa mzigo wa vitabu huku nikimwambia boda kuwa ukifika mpe hii yeye atakupa elfu 30 na elfu tano yako. Jumla elfu 35.

Mimi nikaendelea na shughuli zangu nikijua dakika 30 zijazo kûna elfu 30 inaingia. Baàda ya dakika 15 boda anapiga Simu kuwa amefika lakini yule Mshikaji hapokei Simu. Nikamwambia awe na Subira huku Mimi nami nikimpigia, akapokea akasema anatoka, kumfuata Boda.

Baàda ya dakika 10 nikiwa najua biashara imefanyika na Kwa Hamu nasubiri mshiko wàngu. Nashangaa boda anapiga tenà. "Boss Mtu wako hapokei Simu, napiga inatumika. Hapa kûna bodaboda nimewauliza wamesema Mimi NI MTU WA tano Mtu kutapeliwa na huyo jamaa" Nikamuuliza, kwani kuna Pesa umemtumia?
Akasema aliniambia nimsaidie elfu sita ya Luku alafu nikifika atanirudishia.

Nikasema tayari kimemlamba, nikamwambia Kwa hîyo umemnunulia umeme wa elfu sita? Akasema ndîo.
Akaongeza akiniuliza kwani simjui. Nikamwambia simjui.

Nikamwambia haina shida Rudi kama umemnunulia umeme tutajua namna ya kumkamata. Boda akarudi, nikamwambia leta hiyo Luku uliyomnunulia umeme ili nifuatilie hiyo Nyumba Iko Wapi na inamilikiwa na Nani.

Boda ananiambia alimtumia elfu sita Yule tapeli kwenye Simu. Nikabaki namwangalia tuu.
Nikampa elfu tano Yake ya nauli akanipa vitabu vyangu. Tukaachana. Huo ni utapeli kupitia Mtu Mwingine. Yàani unaweza kuwa genius lakini ukaliwa Pesa zako kupitia Mtu Mwingine ASIYEWEZA kufikiri Sawasawa.

Ni vizuri kama Mtu anakupa fursa kuhusu Jambo Fulani àmbalo wewe sio mjuzi, mtaalamu nalo NI Bora utafute watu unaofahamiana nao uwaulize. Mfano unanunua gari, Huna uelewa na mambo ya Magari, NI Vizuri utafute Mtu mwenye ujuzi na anayefanya Kazi hizô unayemjua akusaidie

Taikon amechoka kuandika, Acha nipumzike sasa.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Serana Hotel, Dar es salaam
 
Yale ya Gwajima kufufua mfu, misukule kuanguka kanisani kwa Mama Rwakatare, viwete kutembea na vipofu kuponywa kwenye mahubiri ya akina Moses Kulola na manabii au mitume wengine, wapenzi waliochepuka kunasana wakiwa kitandani guest n.k. yote ni maigizo tu.
 
Zile NI drama na propaganda Kwa Ajili ya vitoweo(preys) wasio na uwezo WA kufikiria
 
Yule Tiss alaiyetaka kunitapeli mwisho wa siku nikamtapeli yeye na kumgongea demu wake juu........
 
Hapa duniani kama hujawahi kupata changamoto ya yafuatayo maradhi,uchumi,depression ni rahisi sana kuropoka jambo lolote tu hasa ukiwa umeshiba.

Ikiwa watu walisafiri mpaka loliondo na kisha kulipa gharama mbali mbali za ziada wakiwa pale ili tu kwenda kulipa 500,kupata kikombe,unafikiri ni ujinga wao ndio ulisababisha hayo??NO, ni matatizo tena yalikuwa naradhi mbali mbali.

Leo hii nikitangaza nasawazisha ndoa za watu zirudi 100% kama zilivyokuwa siku ya kwanza,nikapata na ushuhuda wa watu 3 tu,kesho njia ya kuja ninapoishi itahitajika polisi kusimamia magari na idadi ya watu.

Msifanye mzaha na matatizo ya watu,watu wana shida mbali mbali nyie.
 
Wajanja hutumia matatizo ya Watu wajinga na weñye upeo mdogo kujinufaisha.

Wakati huohuo hao weñye matatizo unaowatetea kûna àmbao walikuwa na matatizo hayohayo na uwezo WA kwenda lakini hawajaenda Kwa sababu walijua NI utapeli na uongo.

Kutumia matatizo kama kisingizio au kinga ya kufanya ûjinga ni utetezi Usio na Ñguvu na unachukuliwa kama utetezi pia WA Watu weñye upeo mdogo.

Utapeli unasababishwa na Moja ya mambo yafuatayo;
1. Upeo mdogo WA wahanga.
2. TAMAA ya kutaka Vitu Kwa harakaharaka
3. Uvivu wa Kufikiri

Matatizo siô chanzo cha Mtu kutapeliwa
 
Hapa duniani kama hujawahi kupata changamoto ya yafuatayo maradhi,uchumi,depression ni rahisi sana kuropoka jambo lolote tu hasa ukiwa umeshiba.

Ikiwa watu walisafiri mpaka loliondo na kisha kulipa gharama mbali mbali za ziada wakiwa pale ili tu kwenda kulipa 500,kupata kikombe,unafikiri ni ujinga wao ndio ulisababisha hayo??NO, ni matatizo tena yalikuwa naradhi mbali mbali.

Leo hii nikitangaza nasawazisha ndoa za watu zirudi 100% kama zilivyokuwa siku ya kwanza,nikapata na ushuhuda wa watu 3 tu,kesho njia ya kuja ninapoishi itahitajika polisi kusimamia magari na idadi ya watu.

Msifanye mzaha na matatizo ya watu,watu wana shida mbali mbali nyie.

Shida siô sababu ya kutapeliwa. Na haijawahi kuwa sababu ya Mtu kutapeliwa.

Ndio maana matapeli hudanganya weñye shida na wasio na shida. Lakini Kamwe tapeli hawezi kumdanganya Mtu mwenye Akili, asiye na TAMAA na asiye mvivu
 
Maisha tunayoishi Sasa wenzetu walishapita miaka mingi sana...wakati mwingine si kuzidiwa upeo au akili bali ni kuzidiwa ujanja ujanja... Sir. Isaac Newton alishawahi kupigwa pesa zake na wajanja wa stock market miaka hiyo, watu walishauziwa Eiffel Tower huko Paris, Kuna viongozi wakubwa nchi hii walishapiga kikombe cha babu huko loliondo, wapo wengine waliingiza nchi kwenye shimo kubwa la mikataba ya hovyo nk.
 
Naunga mkono hoja.

Je, ndivyo tulivyoumbwa? Au hii ugali maharagwe tunaokula tangu utotoni unatudumaza akili?
 
Hapa duniani kama hujawahi kupata changamoto ya yafuatayo maradhi,uchumi,depression ni rahisi sana kuropoka jambo lolote tu hasa ukiwa umeshiba.

Ikiwa watu walisafiri mpaka loliondo na kisha kulipa gharama mbali mbali za ziada wakiwa pale ili tu kwenda kulipa 500,kupata kikombe,unafikiri ni ujinga wao ndio ulisababisha hayo??NO, ni matatizo tena yalikuwa naradhi mbali mbali.

Leo hii nikitangaza nasawazisha ndoa za watu zirudi 100% kama zilivyokuwa siku ya kwanza,nikapata na ushuhuda wa watu 3 tu,kesho njia ya kuja ninapoishi itahitajika polisi kusimamia magari na idadi ya watu.

Msifanye mzaha na matatizo ya watu,watu wana shida mbali mbali nyie.
Unachanganya mada, matatizo yameumbiwa binadamu na hayatokaa yaishe. Sasa ujinga anaouzungumzia mtoa mada ni jinsi watu wanavyopambana na matatizo yao ndiyo kipimo cha akili. Kupitia sayansi imethibitisha kwamba UKIMWI au KANSA STAGE YA JUU hazina tiba, anakuja nabii au babu wa Loliondo anakwambia anaitibu. Cha ajabu ni kwamba humuoni akienda hospital na kuombea watu wakapona na kupimwa na kuonekana hawana maradhi. Yeye anakuambia njoo kwa nabii ukuwa na sadaka,tena unaambiwa dau laki tano!! Kumbuka wakati tunapata uhuru Nyerere alisema moja ya maadui wakubwa mwaka 1961 ilikuwa ni UJINGA, miaka 60 baadae adui UJINGA ndiyo kwanza kujichimbia mizizi yake kwa raha zake.
 
Back
Top Bottom