Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
Mpo Salama!
Watanzania wengi wametoka na kulelewa kwenye jamii nyingi zinazomini na kufundisha kuwa MKUBWA HAKOSEI.
Watanzania wengi wanaamini ukishakuwa Mzazi wewe tayari ni Mungu hivyo hukosei na hupaswi kuambiwa umekosea.
Watanzania wengi wanaamini ukishakuwa kiongozi Mkubwa labda Rais, Waziri, Mkurugenzi, Boss au Padri au Sheikhe basi huwezi Kukosea. Hao ni Watanzania.
Unajua sababu ni nini?
Sababu ni kuwa Watanzania wengi ni Watumwa, kama sio watumwa WA kiuchumi basi Watumwa Kifikra.
Mtanzania ukimwambia mzazi Fulani kamdhuru Mtoto wake atakukatalia katakata Mpaka uwe na ushahidi WA wazi. Lakini mtanzania huyohuyo ukimwambia mtoto kamdhuru mzazi wake Wala hatahitaji ushahidi atasadiki.
Pia soma: Erick Kabendera kupitia Kitabu chake: Ben Saanane aliuawa na Rais Magufuli na maiti yake ikatupwa Mto Rufiji
Kuna wadau wamenichekesha kweli kwenye Hili sakata la kitabu cha Kabendera, mtu Mmoja akasema ati JPM hawezi kushika bastola na kummwaga mtu ubongo. Ukimuuliza kwa nini anaamini hivyo utashangaa Sana.
Watanzania, mtu ni mtu tuu bila kujali jinsia yake, umri wake, cheo chake, Elimu yake n.k.
Kuwa Mzazi hakumfanyi mtu asitende uovu au uhalifu.
Kuwa Rais au Waziri au mfalme hakuondoi ubinadamu wa Mtu.
Ogopa watu ambao hawataki kukosolewa. Ogopa Sana.
Hakunaga watu waovu na mashetani kama watu wanaopinga kukosolewa.
Iwe ni Mzazi, iwe ni kiongozi, iwe ni Mume, mtu yeyote anayejifanya kwa vile ni Mkubwa au anasifa Fulani ndio anajifichiemo humo asikosolewe ukifuatilia ni mbaya Sana kuliko wale ambao wanaruhusu kukosolewa.
Mtu muovu hataki kukosolewa ili ukweli wake ujulikane. Hataki vazi la Kondoo alilovaa liondolewe huku yeye ni mbwa mwitu. Hataki kuumbuka.
Sisi watibeli hatuwapi watu heshima kwa Jinsia Zao, kwa umri wao, kwa cheo chao,kwa mali Zao, Bali tunawapa watu heshima kwa matendo Yao.
Ndio maana Sisi wengine tunapokutana na aina Fulani ya watu waliozoea heshima za Watumwa wanatuona tuna dharau.
Uongozi wako, pesa zako, umri wako, Jinsia yako hauna maana yoyote kwa Watibeli ikiwa haujiheshimu na kuheshimi watu wengine.
Nawatakia jioni Njema